Tulonge

Jamaa mmoja aliyejulikana kwa jina la Zovuta aliyechukuliwa kutoka kijiji cha Mtakayo, Kisarawe na kuletwa Dar kuuza duka, hivi karibuni alitoa kali ya mwaka baada ya kukataa noti ya dola aliyotoa mteja mmoja kwa bahati mbaya akiwa na lengo la kununua sigara.
Tukio hilo lilitokea maeneo ya Machimbo Bwawani ambapo alikuja mteja huyo katika duka alilokuwa akiuza Zovuta, akiwa amelewa, aliingiza mkono mfukoni na kutoa noti ya Dola 100, akidhani ni shilingi 500, akitaka apewe sigara zenye thamani ya fedha hiyo.
Zovuta aliipokea noti na alipoitazama na kugundua kuwa haikuwa ya shilingi 500, alianza kupiga mayowe kwamba jamaa alikuwa tapeli na ndipo watu kibao walipokusanyika kwenye duka hilo.
Baada ya mashuhuda kuitazama noti ile na kugundua kuwa ni dola, jamaa mmoja alitoa noti ya shilingi 500 na kumpa Zovuta akimtaka ampe sigara ndipo baadaye alikwenda kwenye duka la kubadilishia fedha akaichenji ile dola na kujipatia zaidi ya shilingi 140,000 ikiwa imekula kwa Zovuta muuza duka mshamba.

Views: 285

Replies to This Discussion

Hahahaahahha! Dola mnazijua nyie tu wa mjini sisi wa vijijini tumekariri hela zetu za madfu tu wala msituchanganye kabisa...lol

RSS

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*