Tulonge

Kumbuka kuwa hata chungwa moja tu
ukila lina kidhi yale mahitaji muhimu ya mwili ya kila siku (daily
requirement), iwe chungwa lenyewe au juisi yake halisi.
1. UKOSEFU WA CHOO

Kutokana kuwa na kiwango kikubwa cha
kirutubisho aina ya kambalishe (fibre), chungwa husaidia usagaji wa chakula
tumbuni na hutoa ahueni kwa mtu mwenye matatizo ya ukosefu wa choo. Aidha,
kambalishe huondoa kolestro na huimarisha kiwango cha sukari mwilini, hivyo
chungwa ni zuri kwa wagonjwa wa kisukari.
2.UGONJWA WA MOYO

Kiwango kikubwa cha Vitamin C na
virutubisho vya ‘flavonoids’, ‘phytonutrients’ vilivyomo kwenye chungwa,
huondoa kwa mlaji hatari ya kupatwa na magonjwa ya moyo (Cardiovascular
disease)!


3. SHINIKIZO LA DAMU

Virutubisho vya Magnesi (Magnesium)
na ‘hesperidin’ vilivyomo kwenye chungwa, husaidia kuondoa tatizo la shinikizo
la damu la juu (high blood pressure), hivyo machungwa ni mazuri kwa wagonjwa wa
presha.


4. UGONJWA WA MAPAFU

Chungwa pia lina kiasi kikubwa cha
Vitamin B6 na Madini ya Chuma (iron), virubisho ambavyo ni muhimu kwa
uzalishaji wa seli nyekundu za damu, ambazo hufanya kazi ya kusafirisha hewa ya
oksjeni mwilini, hivyo kuwa muhimu kwa kujikinga na ugonjwa wa mapafu.5. MIFUPA NA MENO

Chungwa lina kiasi kingi cha madini
ya kalisi (calcium) ambayo ni muhimu kwa uimarishaji wa mifupa na meno.
6. AFYA YA NGOZI

‘Anti oxidants’ iliyomo kwenye
chungwa, hutoa kinga kwenye ngozi ili isiharibike au kushambuliwa na magonjwa
ya ngozi yanayoweza kujitokeza kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa. Pia
huifanya ngozi ‘isizeeke’.
 

7. KOLESTRO

Virutubisho vilivyomo kwenye
chungwa, hasa kwenye maganda yake, hupunguza kiwango cha mafuta mabaya mwilini
(bad cholesterol). Hivyo kwa wenye tatizo la lehemu wanashauriwa kula machungwa
pamoja na nyama zake.8. UKUAJI WA UBONGO

Chungwa moja lina kiasi cha asilimia
10 ya ‘folic acid’ inayohitajika mwilini kila siku. Madini haya ni muhimu kwa
afya ya ngozi na ukuaji wa ubongo kwa ajili ya kuimarisha kumbukumbu na uwezo
wa mtu wa kufikiri.


9. KINGA YA MWILI

Vitamin C iliyomo kwenye chungwa
huimarisha uzalishaji wa seli nyeupe ambazo ni muhimu kwa uimarishaji wa kinga
ya mwili. Unapokuwa na kinga imara, huwezi kusumbuliwa na magonjwa mara kwa
mara, yakiwemo malaria.10. UGONJWA WA FIGO

Ulaji wa machungwa mara kwa mara,
ukusaidia kujiepusha na ugonjwa wa figo kwa kiasi kikubwa.


11. UGONJWA WA MAFUA

Kutokana na wingi wa virutubisho vya
kinga vilivyomo kwenye chungwa, ulaji wake mara kwa mara utakuepusha na
magonjwa ya kuambukiza na vairasi (virus), kama vile mafua ambayo hivi sasa
yanawasumbua watu wengi. Hivyo kula machungwa mengi kadii uwezavyo ili
ujiepushe na mafua.

 

12. KINGA YA MAGONJWA MENGI

Chungwa, siyo tu linatoa kinga kwa
magonjwa yaliyoainishwa hapo juu, bali pia hutoa kinga hata kwa magonjwa mengine
kama vile baridi yabisi (arthritis, rheumatism), pumu, kikohozi, kifua kikuu,
nimonia na kisukari. Nakushauri kula machungwa au juisi yake halisi kuanzia leo
ili kupata faida hizo
Via: manyandahealthy.blogspot.com

Views: 1054

Replies to This Discussion

hapo nakubali tuko pamoja hata mimi natumia sana machungwa, nikiwa na mafua hasa machungwa yale machachu, ni mazuri hata ukijisikia na homa, kama ukiwa na maleria halafu umekunywa dawa za maleria kula chungwa utajisikia fresh kabisa, machungwa ni mazuri sana sana,

Asante sana ku-share. Nakula sana nikiwa na mafua

RSS

© 2023   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*