Tulonge

Hiki ndicho kizazi chetu, na huu ndio muziki wa kizazi chetu

Kila naposikiliza muziki wa kizazi changu yaani "bongo fleva" huwa napatwa wazimu. Yaani mashahiri ya muziki huu asilimia 99.9 ni mashairi ambayo kwa kweli hayana MAANA kwa kiasi hicho. Wanachojua kuimba hawa jamaa ni kuhusiana na mapenzi, kujisifia kuwa wanamiliki magari ya kifahari wakati wengine hata bajaji hawana, kusifia pombe eti mtu na akili zake anaimba "nani kamwaga pombe yangu" na mbaya zaidi wengine (waimbaji wanaume) wanavaa mavazi mithili ya yale ya akina dada. Wengine wanapaka nywele zao dawa ili ziwe kama za kisomali kama si za kizungu! Na mbwembwe nyingine nyingi ambazo kwa ujumla hazina maana. Ukija kwa waimbaji wa kike nao ni balaa tupu, mavazi wanayovaa ni nusu uchi.
Kwa kweli kuna kazi kubwa ya kufanya kama kweli tuna nia ya kusonga mbele katika sanaa hii ya muziki. Lawama hizi vilevile zitabebwa na wale wanaoendesha vipindi aidha vya radio, ama tv. Yani wanashindwa kuchambua kati ya mchele na pumba. Inasikitsha sana!

Wito wangu kwa wasanii wa muziki, ni kuwa mbadilike kwa kutunga mashairi yanayoweza kuleta manufaa kwa Tanzania au taifa letu. Kuna mambo mengi sana ya kuimba tofauti na mapenzi na kazi zenu bado tukazipenda. Mambo ya kuimba mapenzi, binafsi naweza kutafsiri kuwa ni kukosa uwezo wa kufikiri.

Imbeni nyimbo ili baada ya hata vifo vyenu muweze kusifiwa na kuheshimiwa na hata mashairi yenu kutumika katika masomo vyuoni na hata mahuleni kama ilivyo kwa akina Bob Marley na wengine wanaojulikana.

Views: 443

Reply to This

Replies to This Discussion

-Ila na jamii pia inawachochea wasanii kuimba pumba kwa kununua kazi zao.

-Kama ni kweli hatutaki aina ya nyimbo ziimbwazo na wasanii wa kizazi kipya kwa nini tunaendelea kununua kazi zao? Mfano Diamond, nyimbo zake karibu zote zimebeba ujumbe wa mapenzi. Kwa sasa ni mmoja kati ya wasanii wenye mafanikio makubwa kutokana na hizo hizo nyimbo zake za mapenzi.

-Kama ni kweli tunaona wanapotosha jamii basi inabidi tusiwa-support kwa kununua kazi zao.Lazima na wao watabadilika

Reply to Discussion

RSS

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*