Tulonge

Bwana Toto Kassi ambaye ni Afisa Mistu wilaya ya Same mkoa wa kilimanjaro alisimamishwa kazi na Mh. anayejiita Maige tangu 23/12/2010 na Mkurugenzi alimwandikia kutekeleza agizo la bosi wake kuhusu kusimamishwa trh. 7/1/2011. Bwana toto anasema kuwa kosa la kusimamishwa kwake ni kuhusu kuzuia uvunaji haramu wa mistu na uchimbaji haramu wa madini katika mstu wa Same wa asili ambao una maslahi na Maige mwenyewe na Mkuu wa wilaya hiyo.

Kwa hali hiyo hadi leo uvunaji wa mistu na madini unaendelea kwa kasi ya ajabu kwani kizuizi hakipo tena na huyu bwana anaendelea kulipwa mshahara bila kazi. ni haki yake kikatiba kufanya kazi. Bwana toto amepeleka malalamiko yake sehemu zote husika lakini wote wanamwogopa Maige na wengine wamashaathirika kikazi kwa sababu ya kutaka kumsaidia kwani wanamwogopa Maige.

Je hii ndiyo Tanzania tunayoitaka/

Je huyu ndiye Maige aliyenunua nyumba ya dola 700,000?

Je huyu ndiye aliyedai justice bungeni kuwa hakuhojiwa na kamati kuhusu madudu ya wizara yake?

Au hii ni haki kweli?????????????????????

Views: 419

Reply to This

Replies to This Discussion

Hivyo ndivyo Tz inavyoendeshwa, ukiongea ukweli lazima wakufukuze kazi au wakuue kabisa. Ushirikiano wa karibu sana unahitajika kwa sisi watanzania kupinga hili. Tatizo watanzania tulio wengi ni waoga sana na hatuna ushirikiano.

sidhani kama, una uhakika sana na ulichoandika, ni mtazamo  wangu tu, 2010 maige hakuwa Waziri bali alikwa naibu waziri,  nyumba ya maige kanunua kwa mkopo kama una uwezo waweza kwenda CRDB bank unaweza ukakutana na uongozi watakuonyesha hati ya nyumba ya Maige, na mkataba walioandikiana na Bank nusu ya pesa imelipwa na Bank ya crdb, na atarejesha kutokana na mshahara wake pia ana kampuni ya usafirishaji ambayo pia atalipia mkopo aliokopa.na wachimbaji madini pale wengi ni wazawa wala siyo wawekezeji wa nje na wengi wanatoka maeneo hayohayo, wazee wa pale wanamizengwe balaa, hivyo watu wengi wa nje ya same wanashindwa kuchimba madini pale, hili la misitu sijalifuatilia sana.

Manka, hebu tafuta katika wavuti.com ili uione barua au maelezo sahihi ya bwana Toto Kessi. Labda kama una ubia na Maige but nnachodisplay hapa ni "je haki ya mtumishi ipo wapi?" Yeye ndo katajwa na mhusika kumsimamisha na aidha ndo anatajwa kwa matumizi mabaya ya fedha za serikali tena kwa taarifa za kamati za bunge, Sijapinga mkopo lkn ukumbuke viongozi wetu wengi wametumia migongo ya benki tu kama sababu ili kukinga maovu yao. Hata wewe naamini huna uhakika ila umefuata maelezo yake ya press alofanya na naamini huna uhakika na unachokisema.

Manka ni mara ngapi viongozi wetu wametaja kusingiziwa na mara zote wanakutwa ni kweli wanahusika? Mfano mzuri hata press alofanya alisema amenunua kwa dola 410,000 wakati Mh. Lembeli ambaye wote wanatoka Kahama alikanusha na kudai ni kwa dola 700,000 na hajayakanusha hayo madai. Wewe una ushahidi gani?

Pili nimeuliza maswali mengi mbona umejikita kwa jambo moja?

Reply to Discussion

RSS

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*