Tulonge

Sina mengi ya kusema, ila kifupi ni kwamba; mfuko wa jamii wa PPF ambao umekuwa kwa kipindi chote ukitoa mafao kwa wafanyakazi walioacha au kuachishwa kazi, wamesitisha fao la kujitoa kwa madai kuwa wanatekeleza sheria ya mifuko ya hifadhi ya jamii nchini na ile ya Mamlaka ya Udhibiti na Uendeshwaji wa mifuko hiyo, SSRA. Kwamba ili uchukue pesa yako basi ni lazima ufikishe miaka 55 au sitini (umri wa kustaafu kwa hiari au lazima). Lakini wakati PPF wakifanya haya huku wakidai wanatekeleza sheria; mifuko mingine kama vile NSSF, LAPF na mingineyo, inatoa pesa kwa wanachama wake kama kawaida.

Maswali ya kujiuliza hapa ni haya: Kama PPF ipo Tanzania, na kama SSRA ndiyo Mamlaka inayosimamia na kudhibiti mifuko yote nchini, PPF wanapata wapi uhalali wa kuzuia pesa za watu kwa madai kuwa wanatekeleza sheria hiyo? Je, mifuko mingine kama NSSF, LAPF etc. wao ndiyo kusema wanavunja sheria ya Mamlaka?

Watanzania wengi vijana tunaoambiwa kuwa ili tuchukue pesa zetu basi tunalazimika kuishi mpaka umri wa miaka 55 au miaka 60. Yaani wewe na ka-umri kako hako ka miaka thelathini, ili uchukue pesa yako huko PPF ambako itakuwa ikizalisha mifaida ambayo kimsingi haufaidiki nayo, utalazimika kuishi tena miaka kati ya 25 au 30 ndipo uruhusiwe kuchukua pesa yako. Kumbuka kuwa, mazingira ya kazi katika sekta binafsi si rafiki hapa Tanzania, kwa sababu mishahara ni kiduchu kiasi kwamba ni ngumu kuweka akiba benki kutokana na maisha kuwa a ghali, pia ajira zetu hazieleweki, kwa sababu ya kufilisika kwa kampuni au kutokuwa na security kwenye ajira hizi zilizopo sekta binafsi. Yaani leo upo kazini, kesho haupo.

Akili ndogo tu inajua kuwa maisha yanajengwa kwenye umri wa ujana, na ukifika uzeeni ni kupumzika tu, kwa sababu nguvu inakuwa imepungua kupambana na mikikimikiki ya hapa na pale. Sasa kama PPF watazuia hela zetu hizi ambazo ndiyo msingi wetu wa kujiajiri wanataka kujenga tabaka gani? Isitoshe muda huo ukifika wa miaka 55 ama 60 pesa hiyo haitatolewa kwa thamani ya pesa ya wakati huo, na itakuwa ni pesa ambayo haina msaada wowote kutokana na faida yake kuwa ndogo.

Binafsi, nasema hii si sawa, ungana nami kusema hii si sawa, na kilio chetu lazima tukipaze sisi kama wafanyakazi tusisubiri wabunge waje kutupazia sauti. Maana wabunge ambao ndiyo tunaowategemea wapo kimya, na si kwamba hawajui haya. Wanayajua ispokuwa muda wa uchaguzi uko mbali kwa hiyo hawana time na sisi.

............HII SI SAWA........PPF TUNATAKA PESA ZETU MLIZOZIZUIA.........NI HAKI YETU............

Views: 395

Reply to This

© 2023   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*