Tulonge

HIVI WAAFRIKA HATUWEZI KUJIENDESHA BILA WAZUNGU?

Nauliza pole-pole kama Sagatti---Ni swali moja tu lina maneno sita tu. Kuwa: HIVI WAAFRIKA HATUWEZI KUJIENDESHA BILA WAZUNGU?

Nauliza hivyo kwa sababu ya misaada ambayo kila siku tumekuwa tukipewa, na misaada hiyo imekuwa inakuja sambamba na masharti magumu sana. Wengine wanapanda ndege ndege kwenda Amerika (USA) eti kufuata msaada wa vyandarua vya Mil. 90.

Ni hayo tu Waungwana.

Views: 930

Reply to This

Replies to This Discussion

Ni kubweteka tu, na pengine ni zile 10% zinazoambatana na hiyo "misaada".

tuwarudishie magari yao yote tutumie nyumbu zetu

na tufanye hivyo secta zote ndipo tutafanikiwa bana

Tutawezaje kujiendesha wakati tuko mabwanyenye, hatujiamini twapenda kusukmwa na hata huko kwa offices wengi waenda ili mradi tu kuzogoa?? Bado viongozi wetu hawana uzalendo ni mabinafsi na waroho kupindukia. Nimekuwa nakuja Africa nafanya kazi za muda (projects) baadhi ya nchi za kati na kusini mwa Africa. Yaani watu (viongozi) hawako makini kusema wakupe ushirikiano mwepesi kwani kazi ufanyayo ni kwa ajili ya taifa lao na watu wao lakini huwezi amini akili yao yote wanaangalia watapataje 10% iingie mifukoni mwao. Africa bado tuna safari ndefu sana ili tufikie hatua ya kujiendesha wenyewe.

africa kujitegemea mpaka mungu aje

Ten percent--ha ha ha Mama M dada yangu huwa najiuliza................."hivi wao wanaweza kwa nini sisi hatuwezi"........? articles au maandiko mengi ya kuhusu uchumi yanasema miaka ya sistini nchi nyingi za bara Asia, tulikuwa nazo level moja kiuchumi. La kushangaza hivi leo wao kwetu ni maboss!!! Au tulishamkosea Sir God? Nauliza tu.

<3

“Our deepest fear is not that we are inadequate.
Our deepest fear is that we are powerful beyond measure.
It is our light, not our darkness that most frightens us. 

We ask ourselves, 'Who am I to be brilliant, gorgeous, talented, and fabulous?' Actually, who are you not to be? 
You are a child of God. 

Your playing small does not serve the world.
There is nothing enlightened about shrinking 
so that other people won't feel insecure around you. 

We are all meant to shine, as children do. 
We were born to make manifest the glory of God that is within us.
It's not just in some of us; it's in everyone. 

And as we let our own light shine,
we unconsciously give other people permission to do the same. 
As we are liberated from our own fear, our presence automatically liberates others.”

- Marianne Williamson.

****Tafakari.

Hakuna kinachoshindikana but fukuza wazee wote wa 10% kisha itungwe sheria kali ya kulinda fedha za serikali atakaesababisha hasara jera atakaekula rushwa jera au bunduki hadharani tena sheria hiyo ikitekelezwa bila kusita wala kuogopa ianze na vigogo wa ngazi za juu hawa dagaa wote wataogopa nyokozao.

Reply to Discussion

RSS

© 2023   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*