Ni jambo la kushangaza kwa kura tisa za wabunge kuharibika katika uchaguzi wa spika wa bunge uliofanyika leo mjini Dodoma. Katika uchaguzi huo Mh Anne Makinda alichaguliwa kuwa Spika. Kwa nini kura ziharibike? Inamaana kuna baadhi ya wabunge wasiofahamu umuhimu wa kura zao? Au ndo wale waliopita baada ya mchakachuo wa kura?
Matokeo yalikuwa hivi:-
Anne Makinda alipata kura 265 - 74.2%
Mabele Marando alipata kura 53 - 16.2%
Jumla ya kura 327
Kura zilizoharibika 9