Tulonge

Jamani watanzania tumsaidie kiongozi wetu ambaye alikiri kutojua sababu ya nchi yake kuwa masikini wakati yeye ni kiongozi mkubwa hapa nchini. Toa maoni yako.

Wote tunaelewa fika kuwa Tanzania ni moja kati ya nchi masikini sana hapa Duniani japokuwa ina lasilimali za kutosha. Hivi karibuni kiongozi wetu wa nchi alishindwa kuueleza umati wa watu uliokusanyika katika ukumbi wa Mlimani City kwenye 'World Economic Forum' kwa nini nchi yake ni masikini wakati ina lasilimali za kutosha. Jibu lake la kutojua kwa nini nchi yake ni masikini lilishangaza wengi ukizingatia yeye ndiye kiongozi mkubwa wa nchi. Sasa kama hajui kwa nini nchi yake ni masikini, anaweza kufanya mikakati yoyote ili kuikwamua nchi yake na umasikini?

 

Naomaba tujumuike pamoja na kumsaidia kiongozi wetu sababu zinazo sababisha nchi yetu kuwa masikini wakati ina lasilimali za kutosha.

Views: 758

Reply to This

Replies to This Discussion

Hayuko madarakani kwa ajili ya kujua kwanini nchi ni masikini na kipi kifanyike kuikwamua...bali yupo pale kwa maslahi binafsi tu hasa biashara zake na familia yake!!!!!I hate him.......
Toka lini jino lenye tundu lililooza, linalokuuma na kukukosesha uzingizi usiku na mchana likaponyeka? Hata kama doctor ataliziba juu kwa lisasi bado litauma tu sababu huko ndani lilishaoza, wahenga wanasema dawa kubwa ya jino bovu ni kung'olewa.

Hivyo hata kujumuika kumsaidia kiongozi (jino lililooza) hakutotosha. Katika tembeatembea yangu kuna nchi Ulaya masikini sana wa rasilimali (e.g Denmark, Netherlands, etc.) lakini serikali za nchi hizo zatumia kodi ya wananchi wake kutoa matibabu ya bure, elimu ya bure, nyumba za bure kwa masikini, chakula, etc. Tanzania ina migodi mingi, inachimba gas, utalii, etc. lakini bado serikali ya Denmark na Netherlands zinatoa misaada kwa Tanzania. Kipindi cha Nyerere hatukuwa na migodi yote hii ya sasa lakini nilisomeshwa kwa korosho, pamba, kahawa, etc. na bado matibabu nilipata bure.

Mungu ibaraiki Tanzania
Yani mm nashangaa kabisa,pa1 na kutojua kwa nn nchi yake ni masikini lkn majitu (baadhi ya watz) bado wanamng'ang'ania tu. Ngoja nimuachie Cha aje kumaliza kazi hahaahaaa.
Tatizo kubwa sana tunalo. Alipokuwa anaomba kura mwaka 2005, moja ya malengo yake ni kutatua matatizo ya Watanzania, sasa haingii akilini kusikia mtu huyohuyo akisema hajui kwa nini nchi yake ni masikini. Kwa sababu ili mtu aweze kutatua tatizo, ni lazima ajue chanzo cha tatizo hilo. Hapo ndipo naposema siku zote kuwa "RAIS WA TANZANIA WA SASA WA NECK ALIYEPATIKANA KWA KURA ZA KUCHAKACHUA, UWEZO WAKE NI MDOGO SANA KWA NAFASI HIYO, LABDA ANGEBAKI KUWA MKUU WA WILAYA TU". Ni hayo tu wadau.
Ha ha ha ha ha! Dismas, wajua kuna watu wanafiki nchi hii, wanajifanya hawaoni wakati wanaona, wanajifanya hawasikii wakati wanasikia....Najitahidi sana huku mitaani kuelimisha mijitu kama hii na kuna wakati naishiwa na busara kiasi kwamba huwa nawatukana ilimradi wanielewe. Ila tutafika tu

Tulonge said:
Yani mm nashangaa kabisa,pa1 na kutojua kwa nn nchi yake ni masikini lkn majitu (baadhi ya watz) bado wanamng'ang'ania tu. Ngoja nimuachie Cha aje kumaliza kazi hahaahaaa.

Matatizo ya msingi Nchi kukosa mipango yake na kurukia ya kupewa.

 

Tulipoimba UJAMMA NA KUJITEGEMEA kujiuliza hili tumetoa wapi na kwanini ilishinda utekelezaji wake - then mtanzania akawa chakula cha simba kwenye kijiji cha ujamaa kilichoanzishwa kwa nguvu za mkono wa chuma.

UBINAFSISHAJI ( privatisationation) tuwetoa wapi na leo tunafaidi nini.

MTANDAWAZI ( GLOBALISATION) tumetoa wapi na tunafaidi nini.

Ninachotaka kusema - HII life style ya copy/paste haiwezi kusaidia kutuvusha safari  kwa MTANZANIA.

Pili kwa kukosekana hilo la kwanza, linazaa hili ya KIBURI CHA WANASIASA kupigana na WATAALAMU wetu wa ndani pale wanavyoshauri na kuelekeza vitu.Hili nilgaie mfano ingawaje there is thousand of...

Pale, nchi kabla ya kurukia Mfumo wa Vyama vingi - tafiti zilifanyika kwa kupitia - Tume za wanasheria - what its return- Nyalali, kasanga- tumbo n.k Walikejeli na kupuuza kazi nzuri iliyofanyika, basi hili nalo ni kivutili cha mambo.

 

Nisiwachoshe ikawa hotuba ya kuaga Mwezi wa Mei -kwa ufupi UMASKINI WETU SI LAANA YA KUMKOSEA MUUMBA - LAAA!! UCHAFU WA ROHO ZETU...

Reply to Discussion

RSS

© 2023   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*