Wote tunaelewa fika kuwa Tanzania ni moja kati ya nchi masikini sana hapa Duniani japokuwa ina lasilimali za kutosha. Hivi karibuni kiongozi wetu wa nchi alishindwa kuueleza umati wa watu uliokusanyika katika ukumbi wa Mlimani City kwenye 'World Economic Forum' kwa nini nchi yake ni masikini wakati ina lasilimali za kutosha. Jibu lake la kutojua kwa nini nchi yake ni masikini lilishangaza wengi ukizingatia yeye ndiye kiongozi mkubwa wa nchi. Sasa kama hajui kwa nini nchi yake ni masikini, anaweza kufanya mikakati yoyote ili kuikwamua nchi yake na umasikini?
Naomaba tujumuike pamoja na kumsaidia kiongozi wetu sababu zinazo sababisha nchi yetu kuwa masikini wakati ina lasilimali za kutosha.
Tags:
Yani mm nashangaa kabisa,pa1 na kutojua kwa nn nchi yake ni masikini lkn majitu (baadhi ya watz) bado wanamng'ang'ania tu. Ngoja nimuachie Cha aje kumaliza kazi hahaahaaa.
Matatizo ya msingi Nchi kukosa mipango yake na kurukia ya kupewa.
Tulipoimba UJAMMA NA KUJITEGEMEA kujiuliza hili tumetoa wapi na kwanini ilishinda utekelezaji wake - then mtanzania akawa chakula cha simba kwenye kijiji cha ujamaa kilichoanzishwa kwa nguvu za mkono wa chuma.
UBINAFSISHAJI ( privatisationation) tuwetoa wapi na leo tunafaidi nini.
MTANDAWAZI ( GLOBALISATION) tumetoa wapi na tunafaidi nini.
Ninachotaka kusema - HII life style ya copy/paste haiwezi kusaidia kutuvusha safari kwa MTANZANIA.
Pili kwa kukosekana hilo la kwanza, linazaa hili ya KIBURI CHA WANASIASA kupigana na WATAALAMU wetu wa ndani pale wanavyoshauri na kuelekeza vitu.Hili nilgaie mfano ingawaje there is thousand of...
Pale, nchi kabla ya kurukia Mfumo wa Vyama vingi - tafiti zilifanyika kwa kupitia - Tume za wanasheria - what its return- Nyalali, kasanga- tumbo n.k Walikejeli na kupuuza kazi nzuri iliyofanyika, basi hili nalo ni kivutili cha mambo.
Nisiwachoshe ikawa hotuba ya kuaga Mwezi wa Mei -kwa ufupi UMASKINI WETU SI LAANA YA KUMKOSEA MUUMBA - LAAA!! UCHAFU WA ROHO ZETU...
© 2023 Created by Tulonge.
Powered by