Tulonge

JE, TOZO LA KODI KWA WATUMIAJI WA LAINI ZA SIMU NI HALALI?

Hivi karibuni serikari yetu ilitangaza utozwaji wa kodi kiasi cha 1000/= kwa kila line kwa watumiaji wa simu za mikononi, sheria hii ilio pitishwa na kuridhiwa haraka tofauti na sheria zingine imezua hoja na hisia tofauti miongoni mwa makundi tofauti kama vile wananchi wa kawaida na wana siasa, ikiwa hili lilipitishwa bungeni basi ni dhahiri kuwa wapo walio ridhia, ila cha kujiuliza je kodi hii ni halali? embu tujiulize kwa haya machache;

                    Je, ni haki mtanzania anae pata chini ya dola moja kwa siku kama vile wafanya biashara ndogondogo, wafanyakazi wa ndani wakulima n.k, kuchangia sawa na wenye pato kubwa kama vile wabunge, mawaziri na hata mh. Rais?

                  Je, ni haki kuwatoza kodi jamii ya watu tegemeziwa kipato kama vile wazee, walemavu, na hata wanafunzi?

                 Ikiwa wenye makampuni hutozwa kodi, hii ina maanisha kua laini hizi pia hotolewa kodi na makampuni hayo, Je, ni haki kutoza kodi mara mbili kwa bidhaa moja?

                Embu tuone yupi ana changia asilimia kubwa kati ya mwenye pato dogo na pato kubwa katika mfano huu;

          PATO DOGO = 100000/= KODI= 1000/=

          ASILIMIA = 1000sh mara 100%  gawanya 100000sh= 1%

        PATO KUBWA=1000000Ssh, kodi= 1000sh

ASILIMIA=1000sh mara 100/% gawanya 1000000sh =0.1%

hapa tunaona mwenye pato dogo anachangia asilimia kubwa zaidi ya mwenye pato kubwa, je huu sio unyonyaji? HII INAUMA SANA  na wenye kulalamika wala hawakosei.

Views: 1509

Reply to This

Replies to This Discussion

Kuna kahesabu kadogo hapa. Mbunge 1 analipwa 11Mil kwa mwezi. Zidishs kwa wabunge 357.. utapata BOMU hapo . Kila kikako wanajilipa 350,000 Kwasiku kwa kila mbunge.. chukua hiyo 350,000 zidisha mara idadi ya wabunge 357.. utapata pesa wanaya jipatia kwa siku. Kikao kilicho isha kilikuwa cha siku 90.. Endelea kupiga hesabu utaniambia hizo diku 90 wamejipatia kiasi gani.. na hapo niwabunge tu.. kuna wakuu wamikoa.. na viongozi mbali mbali amba huudhuria vikao na kulipwa posho. SAMAHANI NIMEJARIBU KUFANYA HESABU LAKINI KIKOKOTOA CHANGU KIMESHINDWA KUSOMA HIZO NAMBA.
Mh. Zitto alitoa wazo.. akasema FUTA posho za KUKAA "seating allowance" zote za wabunge, mawaziri , wakurugenzi na viongozi wengine utapata pesa zaidi ya tozo ya line ya simu.

Ngoja niishie hapa. hasira!

Kahesabu kako Dixson nimekapenda natamani mkubwa mmoja wa nchi akapitie kisha kaingie akilini halafu halafu afute wazo la kutaka kutudai buku zetu, ila nataka kujuwa kwani haya makampuni ya cm za mikononi hayalipii kodi? na kama yanalipa si kwasababu ya mauzo ya line tunazozitumia au wanalipia kwa mauzo gani?

ukiangalia kiundani hii ni dhuluma maana unatotwa kodi mara 2 kwa kitu kimoja unaponunuwa muda wa maongezi lazima ulipie kodi ukinunuwa cm lazima ulipie kodi haya tuache kununuwa cm ni mara moja kwa mwaka ila muda wa maongezi kwa mwezi mtu wa hali ya chini anaweza kutumia 20,000 au hata 10,0000 tufanye buku 5000 kwa mwezi bado kalipia kodi so kuna haja gani ya kumtoza kodi mara mbili? dah! hii inaumiza vichwa ila hatuna lakufanya wameshafanya maamuzi sisi ni kama kelele za mlango hazimnyimi usingizi mwenye nyumba so tumuachie Mungu kwa hili maana sauti yetu haiwafikii na hata ikiwafikia haisikilizwi yaani inauma, na inapouma zaid nipale wewe mtowa kodi unaumizwa kisha watu wanatumia vibaya pesa zako wanatembelea magari mazuri wanapeana posho bila kuzihurumia pesa za mvuja jasho wanazifanya haki yao yaani kesho kwa Mungu kuna moto unawasubiri kwa kila kiongozi alietumia uongozi wake vibaya.

Swedi unahasira kama umemwagiwa maji ya bettry lol  Waalaikum slaam Kaka sante swaumu ndio tunaendelea nayo. Ila sasa ni jukumu la watanzania kuona kinachowauma hasira zetu ni bora kuzipeleka kwenye uchaguzi unahakikisha hufanyi makosa na usikae nyumbani kususia kupiga kura nenda kapige kura hakikisha unampa mtu sahihi na yeye akiboronga mwaka mwengine mnamtowa mnampa mtu mwengine tukifanya hivi yataisha ila tusipoenda kupiga kura matokeo yake ndio haya tunaumizwa tunabaki kulalamika.

Swedi said:

Kaka Omary Kwanza Asalam Alykum, Hongera kwa Swaumu.....

Hawa Jamaa nadhani wakijadili njia za upatikanaji wa kodi hua wanafikiria vitambi vyao zaidi hawafikirii TZ na Wa TZ. Maana Kwa akili ya kawaida tu haingii akilini kuweka kodi kama hiyo.. wakati bado watu tuna donda la ongezeko za nauli...

Mi nadhani hawa kuna mahali wanataka sasa tufike ili heshima haki na usawa vichukue nafasi yake Nyambafuuuuuuuuuu

Shocking! Kwa GDP gani hadi Tanzania wabunge walipwe pesa hiyo yote? Hiyo posho ya siku 350,000 ni sawa na £140 ya mwingereza. GDP ya Uingereza (per purchasing power) na ukubwa wake wa 1.503 trillion sterling pounds bado mbunge hajagikia hata £100, na siku ikifikia £90 kwa siku kwa mbunge basi wapiga kura wa Ungereza wataandamana na kuchoma moto offices, banks, maduka, etc. kama kawaida yao. Hawana utani inapokuja mambo ya public fund. Na hata hivyo bado watu kima cha chini wana hali nzuri kwani mtu akipata £10,000 or less kwa mwaka halipi income tax, na hapo kwa mfanyakazi mwenye watoto aongezewa posho (child benefit, child care allowance, etc.) haijalishi uko public sector or private sector. Wana siasa wa Tanzania wanapasa kuishi kwenye real world, salary & allowance ya viongozi & wabunge zitolewe kufatana na GDP &Gin.

Nilisoma kwenye the Telegraph & sunday Time kuhusu posho za wabunge Africa nilichoka kuona hizo figures, Nigeria ndio nchi inayoongoza duniani (in terms of US$) kwa wabunge kupewa hela nyingi, Nigeria yazidi nchi zote za G8. Kenya imo kwenye list ya nchi 10 zinazoongoza duniani, UK, Germany na nchi zote za Ulaya magharibi wako chini ya jirani zetu Kenya. Wazungu wamekashifu kyandika gazetini kuwa nchi za Africa ingawa tunaongoza kwa Malipo ya wabunge inapokuja kwenye huduma ya maji machafu na maji safi ndio bara linaloshika mkia duniani, hadi kushika mkia huduma mbaya ya afya. Viongozi wakiugua wakimbilia nchi za magharibi. Aibu sana ukizingatia viongozi wetu wanarandaranda kutwa kuomba omba nchi wafadhiri utasema vishada.

Dixon Kaishozi said:
Kuna kahesabu kadogo hapa. Mbunge 1 analipwa 11Mil kwa mwezi. Zidishs kwa wabunge 357.. utapata BOMU hapo . Kila kikako wanajilipa 350,000 Kwasiku kwa kila mbunge.. chukua hiyo 350,000 zidisha mara idadi ya wabunge 357.. utapata pesa wanaya jipatia kwa siku. Kikao kilicho isha kilikuwa cha siku 90.. Endelea kupiga hesabu utaniambia hizo diku 90 wamejipatia kiasi gani.. na hapo niwabunge tu.. kuna wakuu wamikoa.. na viongozi mbali mbali amba huudhuria vikao na kulipwa posho. SAMAHANI NIMEJARIBU KUFANYA HESABU LAKINI KIKOKOTOA CHANGU KIMESHINDWA KUSOMA HIZO NAMBA.
Mh. Zitto alitoa wazo.. akasema FUTA posho za KUKAA "seating allowance" zote za wabunge, mawaziri , wakurugenzi na viongozi wengine utapata pesa zaidi ya tozo ya line ya simu.

Ngoja niishie hapa. hasira!
Dixon....... Tukiacha hiyo posho ya 350,000tsh kwa siku (yanipa hasira), nimeamua kuangalia kwenye monthly salary. kwa hiyo 11million tsh kwa mbunge mmoja wa TZ nimepiga hesabu ni sawa na £4,400 (Sterling pounds) or US$6,600 kwa exchange rate ya leo (CRDB). Ina maana wabunge wa Tanzania wanapata sawa na Kenya? Jasho lanitoka maana hiyo figure yafanana na ya mbunge wa Kenya ambayo yashutumiwa kwa mbunge kupokea karibu mara 2 ya mbunge wa Germany. Haya nimepiga hesabu ya annual salary ya wabunge 357 wa Tanzania nimepata staggering amount of $28.275mil.... As an economist (myself), that's beyond belief, especially kwa total GDP (ppp) ya Tanzania ilivyo ndogo ambayo haifikii hata robo ya GDP ya Germany ambako mbunge apata karibu nusu ya mshahara wa mbunge wa Tanzania na Kenya. Katiba ya nchi Tanzania yapaswa badilishwa haraka sana

Jamani mi naombeni nisiendelee kusoma hizi poast maana natamani niweze kufika mahali niwaambie hawa wahusika kama hizo figure ni sawa na kulinganisha na shida wanazopata wananchi huko barabarani angalia jioni au asbh mda wa kwenda kazini!! Watu kibao wanatembea kwa miguu ambao wana afadhali kidogo ndio wanapanda gari la kugeuka nalo ni mzigo mwingine huo ambao hauangaliwi kwa mtu wa chini.... Mungu tunusuru hebu tujitahidini kubadilisha hii hali sisi wenyewe kwa kura zetu kama alivyogusia bwana Omary hapo awali..

Mama Malaika said:

Dixon....... Tukiacha hiyo posho ya 350,000tsh kwa siku (yanipa hasira), nimeamua kuangalia kwenye monthly salary. kwa hiyo 11million tsh kwa mbunge mmoja wa TZ nimepiga hesabu ni sawa na £4,400 (Sterling pounds) or US$6,600 kwa exchange rate ya leo (CRDB). Ina maana wabunge wa Tanzania wanapata sawa na Kenya? Jasho lanitoka maana hiyo figure yafanana na ya mbunge wa Kenya ambayo yashutumiwa kwa mbunge kupokea karibu mara 2 ya mbunge wa Germany. Haya nimepiga hesabu ya annual salary ya wabunge 357 wa Tanzania nimepata staggering amount of $28.275mil.... As an economist (myself), that's beyond belief, especially kwa total GDP (ppp) ya Tanzania ilivyo ndogo ambayo haifikii hata robo ya GDP ya Germany ambako mbunge apata karibu nusu ya mshahara wa mbunge wa Tanzania na Kenya. Katiba ya nchi Tanzania yapaswa badilishwa haraka sana

CCMsio imechoka imeoza,sahizi wanavutana Raisi anaongea chake,waziri mkuu,januari makamba,nape,nk kila mtu anazingumza kivyake kama wanajenga mnara wa baberi. unajua kodi hii ilipitishwa bungeni wabunge wa chadema wako arusha kwenye mripuko wa bomu nilisikiliza ck ile kulikua hakuna hata ubishi bungeni wote walikubali ipite wangekuwepo chadema ingetokea vurugu navyojua wanavyo wapenda wanyonge.

Hii ni balaa........ni unyonyaji na si halali hata kidogo. Serikali yapasa kuangalia hili kwa jicho la pili.

Mliwachagua wenyewe, kelele za nini sasa.

I love the country, but I hate the system.
Aliwahi kusema Freeman Mbowe kuwa "maisha bora kwa kila Mtanzania, hayatoletwa na chama kilekile, cha mafisadi walewale, kwa sera za nguvu mpya, hali mpya na kasi mpya". Huwa naishangaa mijitu inayoshabikia CCM, huwa nasema siku zote kuwa hata akitokea ndugu yangu anagombea nafasi yoyote kupitia CCM, kura yangu simpi. Haya yote yanasababishwa na CCM tuache utani. Mwenye macho aone, mwenye akili atafakari, na mwenye masikio asikie.

Ha ha ha ha ha ha ha ha ha! Swedi, nilikuwa sijayashtuakia maoni yako--sasa ndio nayaona. Yaani unataka ufukuzwe---tehe tehe tehe tehe.

Mimi sikubali, atakayenifukuza awe wa kwanza kujifukuza. Vinginevyo, vinginevyo...(still loading---please wait while the page is opening).......

Swedi said:

Naona Hii nchi Haitupendi wala haina Haja na sisi walala hoi.. Wangetuambia au watufukuze tukatafute hifadhi huko duniani.. Haiwezekani wanatukandamiza kila kukicha ili wafaidi wao zaidi. I hate this situation

Reply to Discussion

RSS

© 2023   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*