Tulonge

Ukiwa kama mwanaume unaishi katika nyumba yako peke yako mara wahisi kuna mtu anakuwa aingia nyumbani kwako na kula chakula ndani friji lakini hujawahi kumkuta/muona au kumshika na hiyo imekutokea karibu yafikia mwaka. Iwapo siku ya siku unamkuta mwanamke ndani ya hiyo nyumba yako kajificha ndani ya kabati (kubwa za kujengelea) ambayo ndio kageuza makazi yake utamfanya nini?????? Utaendelea kumkarimu kumsaidia??? Kumuachia huru aende zake au kudai malipo yako???????

 

Kuna kisa kimetokea huko nchini Japan miaka 4 iliyopita homeless woman alijipatia hifadhi kisiri siri kwenye nyumba ya mtu (mwanaume) bila ya mwenye nyumba kujua.

 

Kwa habari zaidi soma hapa chini...

http://www.telegraph.co.uk/news/newstopics/howaboutthat/2054057/Hom...

Views: 1305

Reply to This

Replies to This Discussion

Tutaenda elewana naye polisi kudadeki zake. Hawezi kunifilisi hv hv, maisha yenyewe magumu haya.

mie naoa kabisa mama ha ha ah ah

nitamuuliza kwanza kwanini ameamua kufanya hivyo, kisa chake kikinitia huruma namsaidia tu aendelee kuishi huru nymbani kwangu.

Duh.. hapa naungana na chaoga moja kwa mojo.. hahahaaa.. kama analipa.. najichukulia bila mahari kabisaa HAHAHAHAA

Mmh! hii sasa kazi utajikuta unaoa jini.

 

Mkwe asante sana kwa swali lililoshiba kama hili.Haya ndio maswali yatakayobahatika kupendwa zaidi na mimi mwaka huu.

Kwa ufupi bila kupoteza muda ikiwa ni mimi nikakumbana nae kwa nyumba tena mtu mwenyewe ndio kama hivyo mwanamke,kusema ukweli lazima tumalizane hapo hapo hakuna kupelekana polisi au nyumba kumi kumi,maana nikimpeleka huko atafungwa na mimi sitafaidi wakati nishapata hasara ya misosi yangu mwaka mzima.

Hivyo lazima twenda sawia kwanza then baada ya hapo tunaangalia utaratibu mwingine unaofuata.Na akiwa ni mwanamke kiwango zaidi basi hiyo misosi aliyokula muda huo wote itakuwa ndio mahali yake,kwa maana inabidi awe wife ukizingatia mtu mwenyewe niko bachela bado.

Hii ni akiwa mwanamke,ama akiwa dume nadhani hapo dunia nzima inatambua nitamfanya nini,yaani huyu nikimtia mikononi tu tena ndani ya nyumba yangu,zile dakika tano za mwanzo nisha mla vichwa vya usoni kama 70 hivi na vipepsi visivyokuwa na idadi.

Baada ya muhtasari kama huo wa kumgeia maumivu ya kiwango cha juu yale tunayoyaita form six,hapo ndio naweza kuchukua uamuzi wa kumfikisha mbele ya vyombo vya sheria akiwa katika hali ya kuota manundu usoni.

Huyu inavyoonekana atakuwa na bahati mbaya sana na ukizingatia mtu mwenyewe dume,lakini yule wa kwanza (mwanamke) naweza kukumbana na huruma yangu na tukazungumza zaidi.

Wapenda totoz utawajua tu hapa, kama huamini ngoja Alfan na Kunambi waje.

Olivia Lyatuu@ mbona unanilet down dada,yaani unaanza kumuuza mtu ulikuwa unamsaka mwaka mmoja sasa umepita na ashakutia hasara ?!!!

Mtu kama huyo bila shaka unajua tu alikuwa na mitatizo na  ndio maana akamendea misosi yako,cha kufanya ambacho nakiona kinaweza kikaenda sawa na hasara yenyewe baada ya kumtia mikononi ni kumalizana kwanza kabla ya kila kitu , halafu maswali mengine baadae kama yale ya unaitwa nani,unatatizo gani,sijui unaishi mtaa gani, na .....maswali mengine kibao.

sasas bahati mbaya huyu mrembo ni muathirika  wa HIV na ww umeshamalizana nae katika kukueleza matatizo yake linajitokeza hilo kuwa ameathirika  hana msaada akaona aje kwako apate chakula  utafanyaje? me naona bora ukae nae chini ongea nae nini? kimemsibu mpaka akaja kwako huenda nimatatizo ya kibinaadam ambayo yanaweza kumkuta kila mwanaadam katika huu ulimwingu so tusitumie uwezo tulionao kama fimbo ya kumchapia mnyonge MUNGU hapendi hivyo.

 

nitarudi tena.

Chaoga wewe chiboko, huhitaji gharama ya ubani wala kumwita sheikh.. Ha haa haa haaaa

 

Dixon nilijua tu.... Ha haa haaa

Uamuzi wako ni mzuri ila huko police hsa hizi za wenzetu wakisha maliza andika maelezo kituoni anaachiwa.


Tulonge said:

Tutaenda elewana naye polisi kudadeki zake. Hawezi kunifilisi hv hv, maisha yenyewe magumu haya.

Omary..... HIV Test Kit kwa wenzetu (most developed countries) siku hizi wanazo majumbani unanunua hivyo Chaoga na Dixon wangekuwa Japan wangempima wao wenyewe huyo mwanamke na majibu ni dakika hiyo hiyo kama vile unavyofanya unapokuwa na Malaria Test Kit. Hivyo Chaoga na Dixon wala wasingekuwa na mashaka. Ha haaa haa haaaa.....

 

Ila usemayo ni kweli... ni bora ukae naye chini uongee naye na kumwambia kuwa alichofanya ni kosa bora angeomba au angekuja kwa gear ya kuomba kazi nyumbani kwako ya kusafisha bustani na kumlipa. Tatizo akija kuomba kwa ustaarabu siajabu hatosaidiwa....

Omary said:

sasas bahati mbaya huyu mrembo ni muathirika  wa HIV na ww umeshamalizana nae katika kukueleza matatizo yake linajitokeza hilo kuwa ameathirika  hana msaada akaona aje kwako apate chakula  utafanyaje? me naona bora ukae nae chini ongea nae nini? kimemsibu mpaka akaja kwako huenda nimatatizo ya kibinaadam ambayo yanaweza kumkuta kila mwanaadam katika huu ulimwingu so tusitumie uwezo tulionao kama fimbo ya kumchapia mnyonge MUNGU hapendi hivyo.

 

nitarudi tena.

Reply to Discussion

RSS

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*