Tulonge

Ukiwa kama mwanaume unaishi katika nyumba yako peke yako mara wahisi kuna mtu anakuwa aingia nyumbani kwako na kula chakula ndani friji lakini hujawahi kumkuta/muona au kumshika na hiyo imekutokea karibu yafikia mwaka. Iwapo siku ya siku unamkuta mwanamke ndani ya hiyo nyumba yako kajificha ndani ya kabati (kubwa za kujengelea) ambayo ndio kageuza makazi yake utamfanya nini?????? Utaendelea kumkarimu kumsaidia??? Kumuachia huru aende zake au kudai malipo yako???????

 

Kuna kisa kimetokea huko nchini Japan miaka 4 iliyopita homeless woman alijipatia hifadhi kisiri siri kwenye nyumba ya mtu (mwanaume) bila ya mwenye nyumba kujua.

 

Kwa habari zaidi soma hapa chini...

http://www.telegraph.co.uk/news/newstopics/howaboutthat/2054057/Hom...

Views: 1304

Reply to This

Replies to This Discussion

Asante sana kaka yangu nilishapoa...  eddie said:

Pole sana dada, mimi nilipofika huku nilishangaa kwanini watanzania wanakimbiana. Baadae nilipata jibu kwamba wengi ni matapeli! Inabidi umjue mtu in and out umkaribishe.


Mama Malaika said:

Kama ulikuwepo kaka Eddie, kuna mchungaji wa kanisa la mji (Bristol-southwest England) si mbali nasi hapa kwetu kauawa na homeless nyumbani kwake kisa alimkaribisha homeless kipindi cha baridi kali ampe hifadhi ya usiku siku hiyo kulikuwa baridi nje minus 12 (-12C), kumbe homeless ni drug addict na pia aliwahi tiwa ndani miaka 2 kwa kosa la kutaka kum-baka binti wa umri wa Secondary School. Basi kamchoma kisu cha tumbo mchungaji wa watu na kachukua pesa na kukimbia, lakini uzuri wa hawa wenzetu waingereza huyo homeless kashikwa alikuwa kakimbilia north England akiwa mbioni kuingia Scotland na hapo ni baada ya police hunting na kutangazwa kwenye vyombo vya habari na kutolewa sura yake.

 

Wema umemponza mchungaji wa kanisa, na hicho ndio kinachotuogopesha sana nchi hii kusaidia homeless. Wengi homeless wa hapa si wema kwani ni drug addicts, wahalifu na wengine ni vichaa waliopata nafuu na kukimbia makazi yao (vituoni).

 

OMARY ndugu yangu na mie nilipokuwa Tanzania nilikuwa mwema sana tu kama wewe, lakini kuishi miaka karibu 20 nchi hii nimejifunza na kusikia mengi kiasi kwamba hata kusaidia mtu nakuwa naogopa. Kuna watanzania tu wenyewe walishaniibia kwa roho yangu ya huruma. Wakuta mtu anakuja wamsaidia sababu ni mtanzania mwenzio kakwama ugenini kumbe mwenzio ni tapeli unakujua kusikia kwa watu baada ya kulizwa (tapeliwa).

Sasa hao ndio wanahalibia watu wengine wakose misaada kumbe wapo hivyo?! bc hawahitaji msaada hao wakimbizeni mwanzo mwisho, Mama Malaika nisamehe Mamaangu kwa kukuona huna huruma kumbe ni watu wenyewe hawahitaji kuhurumiwa

Nimekusamehe Omary....

Omary said:

Sasa hao ndio wanahalibia watu wengine wakose misaada kumbe wapo hivyo?! bc hawahitaji msaada hao wakimbizeni mwanzo mwisho, Mama Malaika nisamehe Mamaangu kwa kukuona huna huruma kumbe ni watu wenyewe hawahitaji kuhurumiwa

Reply to Discussion

RSS

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*