Tulonge

Jee,W'Tanzania tumejipangaje na HABARI HII MBAYA YA HAKI ZA MASHOGA ??

UK yataka Tanzania itambue haki za mashoga

Written by Mrfroasty (Ufundi)  //  31/10/2011  //  Habari  //  26 Comments

PERTH, Australia UINGEREZA imetoa shinikizo la kutambua haki za mashoga kwa nchi zinazoendelea na kutishia kusitisha misaada yake kwa nchi zinazokiuka agizo hilo. Waziri Mkuu David Cameron amesema Uingereza ina mpango ya kusitisha misaada yake kwa nchi ambazo sheria zake hazitambui ndoa za jinsia moja na mashoga.
“Nimeshawajulisha baadhi ya wakuu wa nchi kuhusu suala hilo kwenye mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Madola unaofanyika jijini Perth, Australia,” alisema Cameron kupitia BBC.Nchi 41 kati ya nchi 54 wanachama wa Jumuiya ya Madola, zina sheria zinazopinga ndoa za jinsia moja.
Suala la haki za binadamu ni moja ya agenda ambazo viongozi kadhaa walishindwa kuafikiana katika mkutano huo ambao rais Kikwete pia alihudhuria. Cameron alisema: “Tunasema hii ni moja ya vitu vinavyoongoza sera yetu ya misaada kwa mataifa mbalimbali na tayari tumeanza kuitekeleza katika maeneo kadhaa,” alisema.
Aliendelea: “Nchi zote zinazopata misaada kutoka kwetu (Uingereza), zinapaswa kukubaliana kikamilifu na sera hii ya haki za binadamu,” alisema. Cameron alisema ameshazungumza na nchi mbalimbali za Afrika kuhusu suala hilo na utekelezaji wake utafanywa na Waziri wa Mambo ya Nje ya nchi hiyo, William Hague.
Kukomesha vizuizi vya ndoa ya jinsia moja, ilikuwa moja ya mapendekezo yaliyomo katika ripoti ya ndani ya matarajio ya baadaye ya Jumuiya za Madola. Katika mkakati huo, Uingereza imetishia kusitisha sehemu ya misaada ya bajeti kuu kwa nchi zisizokubaliana na msimamo huo lakini imeahidi kwamba haitaondoa bajeti yote.
Nchi ya Malawi imeshaathirika na mpango huo wa Uingereza kwa sehemu ya misaada yake kusitishwa kutokana na misimamo yake kuhusu haki za mashoga. Nchi ambazo huenda zikafuatia hivi karibuni ni Uganda na Ghana. Cameron ameieleza BBC kuwa nchi zinazopokea misaada kutoka Uingereza zinapaswa kuachana na sheria kandamizi. Lakini akaeleza kuwa ingawa sio rahisi nchi kubadilika ghafla, ni bora zikaanza sasa mchakato wa mabadiliko hayo kuliko kuendelea kubweteka.
“Hili ni suala ambalo tunaendelea kulisukuma ili lifanikiwe na tumejiandaa kuwekeza hela pia katika kuhakikisha tunafanikiwa lakini ninashaka kwamba hatuwezi kutegemea mabadiliko hayo kuja mara moja,” alisema. Mjadala mzito ulioibuka katika bunge la Uganda mwaka 2009 kuhusu ndoa za mashoga, ni sehemu ya utekelezaji wa sera hiyo ya Uingereza.
Mwaka huu mwanaharakati wa kutetea haki za mashoga nchini Uganda David Kato alipigwa hadi kifo kutokana na kuongoza kampeni hizo. Bunge la Nigeria sasa linaendelea kujadili Muswada wa kuzuia ndoa ya jinsia moja ikiwamo kuweka adhabu kali kwa watu wanaosadia au kuhamishwa kufungwa kwa ndoa hiyo.

 

Views: 1031

Reply to This

Replies to This Discussion

daaah alaa kweli hili, watu tutaanza rushiana ngumi wenyewe kwa wenyewe, sijui itakuaje siku mtu anagonga kwako anakwambia yeye ni mshenga ametumwa kuleta posa, halafu huna mtoto wa kike una midume tupu...aisee
hahahahahah Chaoga yaani mtu kama huyo humuulizi unatandika tu mambo hayo hukohuko UK huku kwetu MARUFUKU.

Haya Ushoga ndio hivyo ulishahalalishwa kupitia misaada ya Uingereza. Na huyu bwana mdogo David Cameron hiyo misaada yake bora abaki nayo mwenyewe tujue moja na umasikini wetu kwani haiwafikii walengwa (walalahoi) inaishia tu juu kwa juu kwa wakubwa na familia zao.

Tanzania ni nchi tajiri sana sana kufananisha na Uingereza kwani 80% ya chakula tunachokula Britain chatoka nje. Tanzania ingekuwa na viongozi WENYE MOYO wa kujenga nchi na wenye MAADILI ya uongozi (na kazi) hata mdogo David Cameron asingetishia na kulazimisha sirikali za wenzie nini wafanye kwani Uingereza na Africa ina tamaduni na mila tofauti. 

 

Asante sana Babengwa kuturushia habari hii, nilisoma kichwa cha habari kwenye gazeti la Dailymail (UK) la October 8, baada ya kuona picha ya raisi wa Malawi juu ya habari.

 

Mimi binafsi ningekuwa kiongozi wa moja ya nchi hizi za Kiafrika ningekuwa wa kwanza kupinga tena kwa nguvu zote. Misaada yao siamini kama kweli ndo inafanya sisi tuishi; kwani wao mpaka wanafika hapo walipo nani aliwasaidia?

Lakini kwa jinsi hii mi-viongozi ya Kiafrika isivyo na akili nzuri na ilivyo dhaifu kiakili hata kimwili, itakubaliana na mawazo ya kipuuzi ya Cameroon. Na kwa jinsi hali ilivyo, Tanzania yaweza kuwa nchi ya kwanza kukubaliana na masharti ya kipumbavu kama hayo.

 

CHA... viongozi wa Africa hawana ujanja kwani kiasi kikubwa cha budget chategemea pesa ya wafadhili. Angalia MALAWI ilivyoathirika na wale mashoga wawili waliohukumiwa kufungwa mwaka jana for 14 years na baadae kuachiwa baada ya ubalozi wa Uingereza nchini Malawi kumkoromea mjomba Bingu wa Mutharika. Nilienda Malawi mwezi June mambo magumu mno hadi hospitals zote hazina dawa, mishahara wafanyakazi wengi wa sirikalini hawajalipwa miezi na shule waalimu migomo. Viongozi wa Africa hawana akili hata kidogo kutumia hiyo kodi wanayokusanya toka kwa wananchi wao ili waitumie ajili ya maendeleo ya nchi zao bali wanatumia pesa vibaya

Kimbembe cha ndoa za mashoga naona sasa imefikia watu watabakia kusali majumbani mwao tu na viongozi wa dini kuacha kusalisha. Hii link chini ni habari ya leo leo

 

http://www.dailymail.co.uk/news/article-2056609/Gay-marriage-Homose...

 

 

Kweli dunia imekwisha jamani tujitahidi kumrudia Muumba wetu! Mimi kwa maoni yangu binafsi.... KIongozi wa nchi atakayekubaliana na matakwa haya ya waingereza moja kwa moja ntamuweka kwenye kundi la MASHOGA na ntaamini naye ni SHOGA!!!
Tukumbuke hupaswi kumkosea Mungu kwa kumridhisha mwanadamu mwenzako, hata kama ana msaada wa aina gani kwako.

kauli ya Waziri wa mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh Benard Membe:-

 

“ Tanzania ni nchi maskini lakini hatutakubali kuruhusu upuuzi huo eti kwa sababu ya misaada yake na fedha zao, lakini ushoga si utamaduni wetu, hata sheria zetu zinakataa,”


Ha ha ha ha ha h Alfan, hapo umenena.
Alfan Mlali said:
Kweli dunia imekwisha jamani tujitahidi kumrudia Muumba wetu! Mimi kwa maoni yangu binafsi.... KIongozi wa nchi atakayekubaliana na matakwa haya ya waingereza moja kwa moja ntamuweka kwenye kundi la MASHOGA na ntaamini naye ni SHOGA!!!
Asante Dada yangu.

Mama Malaika said:

Kimbembe cha ndoa za mashoga naona sasa imefikia watu watabakia kusali majumbani mwao tu na viongozi wa dini kuacha kusalisha. Hii link chini ni habari ya leo leo

 

http://www.dailymail.co.uk/news/article-2056609/Gay-marriage-Homose...

 

 

Kelele za TULONGE huishia kwa TULONGE.

Cha MAANA sana nadhani, kutumia asasi mbali mbali na wadau wanaopinga 'HILI LIZUNGUMZWE msimamo wetu sote kutokuwa TAYARI kuingiza LAAANA hii.

Taasisi za DINI zifikishiwe ujumbe, watumie nafasi zao kulaani hili na kuiambia ,Serikali waziwazi KUPINGA hili.

Vyama vya siasa zipinge hili..

Vyuo au taasisi za ELIMU zipinge hili..

Ionekane UK inatuvunjia HESHIMA na INATAKA kutudhalilisha.Na, kumegadhibika - mtaji wa umaskini isiwe ni MTEGO wa kutuweka pabaya !!

Haya YAKIFANYIKA, Umma wa Watanzania itakuwa wamejilinda.

HAYA NI MAONI YANGU ,na mie ijumaa ya LEO natumia uwezo wangu wa kufikisha UJUMBE....

 

 

Reply to Discussion

RSS

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*