Tulonge

Jee,W'Tanzania tumejipangaje na HABARI HII MBAYA YA HAKI ZA MASHOGA ??

UK yataka Tanzania itambue haki za mashoga

Written by Mrfroasty (Ufundi)  //  31/10/2011  //  Habari  //  26 Comments

PERTH, Australia UINGEREZA imetoa shinikizo la kutambua haki za mashoga kwa nchi zinazoendelea na kutishia kusitisha misaada yake kwa nchi zinazokiuka agizo hilo. Waziri Mkuu David Cameron amesema Uingereza ina mpango ya kusitisha misaada yake kwa nchi ambazo sheria zake hazitambui ndoa za jinsia moja na mashoga.
“Nimeshawajulisha baadhi ya wakuu wa nchi kuhusu suala hilo kwenye mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Madola unaofanyika jijini Perth, Australia,” alisema Cameron kupitia BBC.Nchi 41 kati ya nchi 54 wanachama wa Jumuiya ya Madola, zina sheria zinazopinga ndoa za jinsia moja.
Suala la haki za binadamu ni moja ya agenda ambazo viongozi kadhaa walishindwa kuafikiana katika mkutano huo ambao rais Kikwete pia alihudhuria. Cameron alisema: “Tunasema hii ni moja ya vitu vinavyoongoza sera yetu ya misaada kwa mataifa mbalimbali na tayari tumeanza kuitekeleza katika maeneo kadhaa,” alisema.
Aliendelea: “Nchi zote zinazopata misaada kutoka kwetu (Uingereza), zinapaswa kukubaliana kikamilifu na sera hii ya haki za binadamu,” alisema. Cameron alisema ameshazungumza na nchi mbalimbali za Afrika kuhusu suala hilo na utekelezaji wake utafanywa na Waziri wa Mambo ya Nje ya nchi hiyo, William Hague.
Kukomesha vizuizi vya ndoa ya jinsia moja, ilikuwa moja ya mapendekezo yaliyomo katika ripoti ya ndani ya matarajio ya baadaye ya Jumuiya za Madola. Katika mkakati huo, Uingereza imetishia kusitisha sehemu ya misaada ya bajeti kuu kwa nchi zisizokubaliana na msimamo huo lakini imeahidi kwamba haitaondoa bajeti yote.
Nchi ya Malawi imeshaathirika na mpango huo wa Uingereza kwa sehemu ya misaada yake kusitishwa kutokana na misimamo yake kuhusu haki za mashoga. Nchi ambazo huenda zikafuatia hivi karibuni ni Uganda na Ghana. Cameron ameieleza BBC kuwa nchi zinazopokea misaada kutoka Uingereza zinapaswa kuachana na sheria kandamizi. Lakini akaeleza kuwa ingawa sio rahisi nchi kubadilika ghafla, ni bora zikaanza sasa mchakato wa mabadiliko hayo kuliko kuendelea kubweteka.
“Hili ni suala ambalo tunaendelea kulisukuma ili lifanikiwe na tumejiandaa kuwekeza hela pia katika kuhakikisha tunafanikiwa lakini ninashaka kwamba hatuwezi kutegemea mabadiliko hayo kuja mara moja,” alisema. Mjadala mzito ulioibuka katika bunge la Uganda mwaka 2009 kuhusu ndoa za mashoga, ni sehemu ya utekelezaji wa sera hiyo ya Uingereza.
Mwaka huu mwanaharakati wa kutetea haki za mashoga nchini Uganda David Kato alipigwa hadi kifo kutokana na kuongoza kampeni hizo. Bunge la Nigeria sasa linaendelea kujadili Muswada wa kuzuia ndoa ya jinsia moja ikiwamo kuweka adhabu kali kwa watu wanaosadia au kuhamishwa kufungwa kwa ndoa hiyo.

 

Views: 1060

Reply to This

Replies to This DiscussionMama Malaika said:

Haya Ushoga ndio hivyo ulishahalalishwa kupitia misaada ya Uingereza. Na huyu bwana mdogo David Cameron hiyo misaada yake bora abaki nayo mwenyewe tujue moja na umasikini wetu kwani haiwafikii walengwa (walalahoi) inaishia tu juu kwa juu kwa wakubwa na familia zao.

Tanzania ni nchi tajiri sana sana kufananisha na Uingereza kwani 80% ya chakula tunachokula Britain chatoka nje. Tanzania ingekuwa na viongozi WENYE MOYO wa kujenga nchi na wenye MAADILI ya uongozi (na kazi) hata mdogo David Cameron asingetishia na kulazimisha sirikali za wenzie nini wafanye kwani Uingereza na Africa ina tamaduni na mila tofauti. 

 

Asante sana Babengwa kuturushia habari hii, nilisoma kichwa cha habari kwenye gazeti la Dailymail (UK) la October 8, baada ya kuona picha ya raisi wa Malawi juu ya habari.

------------------------------------------------------------

  

Asante sana mama mkwe kwa Comment zako nzuri.naweza kusema umeniwakilisha kwa pointi zako.Nikweli bora tubaki maskini kuliko kudhalilishwa na kiumbe dhaifu David asiyekuwa na utamaduni.Anadhani Tanzania ni maskini kihivyo kiasi kwamba tutakuja kumpigia magoti na tumsaada twake,hajui kwamba sisi ni matajiri,aje kwanza tumtembeze maeneo ya huko mwadui akajionee ardhi inatapika dhahabu,huko wingereza kuna sehemu ina dhahabu au harufi ya dhahabu???????????ala!!!!!


Halafu misaada yake hiyo kwa tanzania mbona mimi sijawahi kuiona???? yaani sijawahi kufaidika nayo ukiacaha na kutoiona.Kila siku tanzania barabara zetu hovyo misaada hiyo iko wapi wakati barabara zinapasuka hovyo,kila siku tunapitia madishani kupanda daladala pale maeneo ya kongo ili twende zetu homu mioda ya jioni,wengine tunakatikja viuono kwa tabu ya usafiri na uchache wa magari na barabara,hizo misaada zake kama zipo kwa nini zisisaidie kuongeza barabara za chini au za madaraja ili tuepukane na msongamano wa magari , au kwanini serikali isinunue magari kwa ajili kurahisisha suala la usafiri kwa raia wake kama nchi zingine.hiyo misaada ya UK ni misadaaaaaaaaaaaaa au matatizo na mikosi.

Asante sana kaka Babengwa:Taasisi hizi ulizozitaja naona zimesikia maoni yako.Ni siku ya idi Tanzania imeshuhudia Taasisi ya Kidini ikitoa majibu makali kwa kauli ya kidharau ya UK,na kusema hakika watanzania hatuko tayari kuingiza upuuzi huo Nchini Kwetu:

Hebu zama katika habari hii ,ambayo chanzo chake ni Kiswahili.irib.ir

----------------------------------------------------------------------

 

Viongozi wa Kiislamu Tanzania walaani ushoga; wasema bora kukosa misaada.

Viongozi wa Kiislamu nchini Tanzania wamesema, ni bora Watanzania wakakosa misaada yote kutoka serikali ya Uingereza kuliko kusujudia shinikizo lilitolewa na kiongozi wake la kutaka kuruhusu sheria inayotambua mashoga na kuhalalisha ndoa za watu wa jinsia moja.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti kwenye ibada ya Eid El Hajj viongozi hao wamewataka Waislamu kuungana na kupinga kwa nguvu zote udhalimu huo ili dunia ifahamu kwamba Waislamu na Watanzania hawako tayari kuona Mungu akichezewa.

 Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Musa Salum alisema haiwezekani dini ya Mwenyezi Mungu ikachezewa kwa maslahi ya watu wachache.

Kwa upande wake, Kaimu Mufti wa Tanzania, Sheikh Ali Muhidin Mpoyogole amesema kama hakuna uadilifu kutoka kwa viongozi, amani ya nchi haiwezi kuwa ya kudumu.

Aidha hotuba nyingi za Sala ya idi nchini Tanzania zilitawaliwa na misimamo ya makhAtibu kulaani hatua ya Uingereza ya kuitaka Tanzania itambue haki za mashoga. Msimamo huo wa masheikh umekuja siku chache baada ya Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron kutamka kwamba nchi yake ina mpango wa kusitisha misaada yake kwa nchi ambazo sheria na katiba zao, hazitambui mashoga na ndoa za watu wa jinsi moja.

-=---------=====================--------------=====-=-====---------------

 

 Babengwa said:

Kelele za TULONGE huishia kwa TULONGE.

Cha MAANA sana nadhani, kutumia asasi mbali mbali na wadau wanaopinga 'HILI LIZUNGUMZWE msimamo wetu sote kutokuwa TAYARI kuingiza LAAANA hii.

Taasisi za DINI zifikishiwe ujumbe, watumie nafasi zao kulaani hili na kuiambia ,Serikali waziwazi KUPINGA hili.

Vyama vya siasa zipinge hili..

Vyuo au taasisi za ELIMU zipinge hili..

Ionekane UK inatuvunjia HESHIMA na INATAKA kutudhalilisha.Na, kumegadhibika - mtaji wa umaskini isiwe ni MTEGO wa kutuweka pabaya !!

Haya YAKIFANYIKA, Umma wa Watanzania itakuwa wamejilinda.

HAYA NI MAONI YANGU ,na mie ijumaa ya LEO natumia uwezo wangu wa kufikisha UJUMBE....

 

 

Reply to Discussion

RSS

© 2023   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*