Hahahhahahahahaaa nawashukuru sana baadhi ya wadau waliyo umiza vichwa kwa kutafuta sehemu sahihi alipo paka na kunitumia jibu kwenye inbox yangu. Pia najua wapo wengi waliyo umiza vichwa kumtafuta paka alipo na kuamua kuuchuna kimyaaa baada ya kumkosa paka hahahahaaa.
Najua mtu kama Mama Malaika,Don M, Dixon, Chaoga,Omary,Kunambi,Mary,Agnes lazima walimtafuta sana, walipoona wamemkosa wakaamua kuchuna kimya bila kunitumia ujumbe wowote.
Mdau aliyefanikiwa kumuona paka ni JOHNSON tu, hongera sana mkuu.
Hii ni changamoto kwetu, tuwe tunakula mchicha kwa wingi tuweze ona vizuri kama mwenzetu Johnson. Nasikia huwa anamaliza tenga moja la mchicha kwa siku mbili.
Angalia kwa makini sehemu iliyo zungushiwa DUARA hapo chini utamuona paka mwenye rangi nyeupe na mabaka meusi. Anatembea, kichwa chake kina baka jeusi. Tena ana afya sana, nahisi ni mjamzito.
Angalia baadhi ya wadau waliyo jaribu kuonesha paka alipo hapo chini.
Tags:
hii mie ilinitoa njee kabisaaaaaaaaaaaaaaa.. watu mnatoa macho kama mnaweka mda wa maongezi ? LOL Hongereni mlio patia na kupatia patia
hahahahahahah watano? yeye kazid ila kweli angalia kushoto baada ya bati hilo lenye pembe 4
hizi skrepa dili, ziko tue tuongee biznes....
Hongera kwa kutupatia zoezi la upimaji macho bureee! Sasa tunajijua akina nani tunapaswa kula mchicha kwa wingi!
HATA ULIYETUONYESHA HAPO WALA SI PAKA NI SCRAPER TUU ILA. BORA HATA ALFAN PALE ALIPOCOMMENT NYAU NAHISI YULE NDO PAKA ILA ALIPOCOMMENT PAKA HAMNA KITU HA HA HA
Hahahahaaaaa yani wewe Angela pa1 na kukuonesha paka alipo ila bado hujamuona, inabidi tuchange tukununulie miwani sasa.
ANGELA JULIUS said:
HATA ULIYETUONYESHA HAPO WALA SI PAKA NI SCRAPER TUU ILA. BORA HATA ALFAN PALE ALIPOCOMMENT NYAU NAHISI YULE NDO PAKA ILA ALIPOCOMMENT PAKA HAMNA KITU HA HA HA
MIMI NILITOA MACHO HAPO NIKACHOKA, NAJIPA MAZOEZI YA KUNYWA JUICE YA MCHICHA KWA SASA.
hapo nakataa hadi kesho hamna paka zaidi ya scraper na hapo ulipoonyesha paka wala si paka huyo acha kunidanganya Tulonge nakukataliaaaaaa complete
Mtoto mbishi sana wewe, huyo umpendaye sijui alitumia ujanja gani kukupata.Nahisi alikuroga wewe.Yani unabishana na picha hahahhaahaaaaa.
ANGELA JULIUS said:
hapo nakataa hadi kesho hamna paka zaidi ya scraper na hapo ulipoonyesha paka wala si paka huyo acha kunidanganya Tulonge nakukataliaaaaaa complete
Hahahahahahah tehtehtehteh yaani Angela karogwa? na shemeji! ila Dis kweli unatuchakachuwa mshkaji wangu paka huyo umuone ww tu?
© 2022 Created by Tulonge.
Powered by