Morogoro. Wasomi nchini, wamehimizwa kujifunza lugha ya Kichina, ili washiriki katika kukuza uchumi wa nchi kwa kuzingatia kuwa uchumi wa dunia unategemea sana bidhaa na mchango wa China kwa sasa. Rai hiyo ilitolewa juzi na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera, katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Saidi Amanzi. Hotuba hiyo ilisomwa katika uzinduzi wa ushirikiano wa ufundishaji wa lugha ya Kichina katika Chuo Kikuu cha Waislamu cha mjini Morogoro. Bendera aliwaasa wasomi kutumia fursa ya Kichina, kujifunza kwa bidii na kupanua wigo takaayowawezesha kuwasiliana katika kufanya biashara kati ya Watanzania na Wachina. Katika uzinduzi wa ushirikiano huo, Makamu mkuu wa chuo hicho, Profesa Hamza Ngozi, alisema kuwa ni vyema wanafunzi wakajifuza lugha hiyo na kuitumia kama nyenzo ya kutafuta maarifa zaidi katika dunia ya utandawazi. Alisema chuo kikuu hicho ni tatu nchini kuanza kufundisha lugha ya Kichina, baada ya Chuko Kikuu cha Dar es Salaam na Chuo Kikuu cha Dodoma. Wanafunzi wa chuo kikuu hicho walisema ushirikiano huo ni mzuri na upaswa kuigwa na vyuo vikuu vingine.
Chanzo: www.mwanachi.co.tz
[English yetu iko poor! Kiswahili chetu chenyewe, hatukijui vizuri bado wanahimiza kujifunza Kichina--kama si upuuzi huu ni nini]?
Haya ndio matatizo ya mtu kukurupuka--yaani mtu anaongea jambo bila kutafakari. Mtu unashauriana na mke wako then unaamka asubuhi na ku-present kwa jamii.
Tags:
Asante dada kwa maoni yaliyoshiba, msalimie Malaika na Denzil. Waambie nina mpango wa kuanzisha kozi ya Kiswahili kwenye mtandao--kwa hivyo basi wajiandae kujifunza Kiswahili. ha ha ha ha ha!
Mama Malaika said:
Na huyu bwana hapo juu alipasa kusema kuwa "uchumi wa Africa unategemea sana bidhaa na mchango wa China". Inapasa atoke nje ya Africa na aingie nchi kama Germany, hatoona baiskeli, TV, radio, Fridge Freezer or computer inayouzwa kutoka China. Na hapo bado sijaongelea magari na vifaa vya ujenzi. Wachina wafanyabiashara wakubwa wanakuja west Europe nunua vitu na kwenda uza kwao kwa watu wenye uwezo.
In economic point of view, hata huko US ambako ndio walikuwa waingizaji wakubwa wa bidhaa toka China, US suppliers wengi wamefunga business activities in China na kuhamia Latino & South America sababu ya costs of raw materials, wage, shipping cost na umbali wa kusafirisha ili kumfikia mteja upesi. Na hii ndio sababu ya kupanda kwa unemployment and social unrest in China. Na soko la West Europe sio la kumwaga takataka au kuuza bidhaa za majafibio, hivyo China sasa macho yao yote Africa.
Ha ha ha ha ha ha ha ha! Watu mia moja wa kwanza kujiunga na kozi hiyo watasoma bureeeee!
Asante sana.
Mama Malaika said:
Ha ha haa haa haaaa.... Ukija kwenye kishwahili fasaha, hata mie utanishika tena sana tu iwe kuandika au kuongea. Na hiyo kozi ya kiswahili unayotaka kuanzisha kwenye mtandao mie nitakuwa wa kwanza kujiunga. Ha haa haaaa.....
Jamani Magere kapotelea wapi? Yule apasa aje kwenye huu mjadala, anakijua kiswahili na kakisomea chuo (profession). Nakumbuka alikuwa akianza kukosoa comments za watu zilizoandikwa kwa kiswahili Fotobaraza na mwanzoni humu Tulonge, ndio hapo unatambua kuwa watanzania wengi hatujui kiswahili ingawa tuna kitumia kwa kuongea na kuandika. Na vivyo hivyo kiingereza. Lol....
Ha ha ha ha ha! Magere itabidi atafutwe kwa simu. Dismas atusaidie namba ya simu ya Magere.
Mama Malaika said:
Ha ha haa haa haaaa.... Ukija kwenye kishwahili fasaha, hata mie utanishika tena sana tu iwe kuandika au kuongea. Na hiyo kozi ya kiswahili unayotaka kuanzisha kwenye mtandao mie nitakuwa wa kwanza kujiunga. Ha haa haaaa.....
Jamani Magere kapotelea wapi? Yule apasa aje kwenye huu mjadala, anakijua kiswahili na kakisomea chuo (profession). Nakumbuka alikuwa akianza kukosoa comments za watu zilizoandikwa kwa kiswahili Fotobaraza na mwanzoni humu Tulonge, ndio hapo unatambua kuwa watanzania wengi hatujui kiswahili ingawa tuna kitumia kwa kuongea na kuandika. Na vivyo hivyo kiingereza. Lol....
Naposema hatujui Kiswahili au English ninamaanisha--maneno yangu yanajidhihirisha katika maoni ya dada yangu Habiba.
Dada Habiba, wewe mwenyewe Kiswahili hujui, narudia tena kwa msisitizo dada Habiba Kiswahili hujui vizuri, ndio maana basi umekosa neno au msamiati wa Kiswahili wa neno "comment" ndio maana basi umeishia kusema "unacomment" hakuna neno katika lugha ya Kiswahili kama hilo la "unacomment". Vilevile hakuna neno "kingereza" (rejea maoni yako) katika lugha ya Kiswahili, badala yake kuna neno "Kiingereza". Mengine namezea tu.
Amani iwe nawe dada.
PamoJah.
habiba mustafa mlawa said:
huyo aliyocoment hapo juu kanikera sana kama wewe hujui kiswahili au kingereza ni wewe usitujumuishe wote wakati unacomment uwe unatafakari kwanza

© 2022 Created by Tulonge.
Powered by