Napenda kuchuku fursa hii kukukaribisha kuhudhuria Tulonge Funga mwaka party. Hii ni kwaajili ya kutuwezesha wana tulonge kukutana na kuuaga mwaka 2011 na kuukaribisha mwaka 2012. Siyo tu hivyo bali kuajdili mambo mbali mbali kuhusu kijiji chetu cha Tulonge ili tuweze kusonga mbele zaidi.
Sehemu ya tukio: Cine Club (Karibu na kituo cha Kwa Warioba)
Muda : Saa 9 kamili alasiri.
Tarehe: 14/01/2012, Jumamosi
Karibu sana tushiriki michezo mbalimbali kama kufukuza kuku,kuvuta kamba,kucheza mpira,kombolela,kidali nk.
Kutokana na uchunguzi uliofanya na Mdau Cha, tumepata kufahamu kuwa bei ya vyakula na vinywaji ya Cine Club niya kawaida ambayo mtanzania wa kawaida kama mimi na wewe tunaweza kuimudu.
Vyakula: vinaanzia 1500 na kuendelea
Vivywaji: vinaanzia 1000 na kuendelea
Wasiliana na Cha (0715 822 269), Chaoga (0713 260 058) kwa maelezo zaidi.
**Kila mdau atajitegemea kwa kila kitu.
Tupo pamoja
Tags:
Replies are closed for this discussion.
Mimi nitakuwepo panapo majaaliwa...wewe je?
Na mimi lazima nitie timu kudadeki, nina imani Mungu atanijalia. Pole mkuu Baraka.
Alfan unaweza kucheza muziki lakini? sio kelele nyiiiiiiiiingi alafu uje unitie aibu
Christer muziki tutakaofungua ni ule wa slow kwa hiyo hauhitaji ufundi sana zaidi ya ziro distance...hahahahah
teheeteheteheteheteeeeeeee, we Alfan wewe zero distance utaiweza lakini?
Tutakuwa sote jamani, ubize nitauweka pembeni safari hii.
Hahhhahhhaaaaaaaaa. Belita nae atakuwepo!!! mi sipati picha siku hiyo. Alfan mi sisemi sana 7bb tusiandikie mate wkt jmosi itafika, sitaki kupewa excuse kbs!!
Japo sina uhakika sana,but nitajitahidi nifike maana wengine tuko mbali sana,kama mkitukosa mtatuwakilisha
Lazima niwepo.
PamoJah sana
© 2023 Created by Tulonge.
Powered by