Tulonge

Karibu kwenye Tulonge funga mwaka Party ndani ya CINE CLUB karibu na kituo cha Kwa Warioba

Napenda kuchuku fursa hii kukukaribisha kuhudhuria Tulonge Funga mwaka party. Hii ni kwaajili ya kutuwezesha wana tulonge kukutana na kuuaga mwaka 2011 na kuukaribisha mwaka 2012. Siyo tu hivyo bali kuajdili mambo mbali mbali kuhusu kijiji chetu cha Tulonge ili tuweze kusonga mbele zaidi.

Sehemu ya tukio: Cine Club (Karibu na kituo cha Kwa Warioba)

Muda : Saa 9 kamili alasiri.

Tarehe: 14/01/2012, Jumamosi

Karibu sana tushiriki michezo mbalimbali kama kufukuza kuku,kuvuta kamba,kucheza mpira,kombolela,kidali nk.

Kutokana na uchunguzi uliofanya na Mdau Cha, tumepata kufahamu kuwa bei ya vyakula na vinywaji ya Cine Club niya kawaida ambayo mtanzania wa kawaida kama mimi na wewe tunaweza kuimudu.

Vyakula: vinaanzia 1500 na kuendelea

Vivywaji: vinaanzia 1000 na kuendelea

 

Wasiliana na Cha (0715 822 269), Chaoga (0713 260 058) kwa maelezo zaidi.

**Kila mdau atajitegemea kwa kila kitu.

 

Tupo pamoja

Views: 1070

Replies are closed for this discussion.

Replies to This Discussion

Nitajitahidi nihudhurie

pouwa sana mkuu,itabidi tujipange ili tuje

hahaaaaaa ningekuwa dar nisinge kosa hiyo kombolela.

ANGELA JULIS NAYE ATAKWEPO JAMANI NATAFUTA WA KUCHEZA NAYE MUZIKI HA HA HA

Muziki utacheza na Chaoga, ucjal Angel. tehe!!!!!!!!

Duh nasikitika kukosa maana nitakuwa na majukumu mengine ktk sehemu ya ibada. Tuwakilisheni !

nilipanga kwenda visiwani, ila nimeahirisha nitakuwepo. ivi na bia zinaanzia buku au ?

nitafungua shoo kwa kucheza kiduku, tna nimeshanyoa nywele mtindo wa kiduku tayari

mmmmmmmmmh, safi sana saint.

Nipo teyari kucheza na wewe dada Angela.

ANGELA JULIUS said:

ANGELA JULIS NAYE ATAKWEPO JAMANI NATAFUTA WA KUCHEZA NAYE MUZIKI HA HA HA

Pascal wa Mabagala, long time no see you. I hope kesho tutakuwa PamoJah, ila kesho mimi nitakuwa na doze, hivyo usishangae kuona nakunywa juice ya azam.

Saint Pascal of Zanzibar said:

nilipanga kwenda visiwani, ila nimeahirisha nitakuwepo. ivi na bia zinaanzia buku au ?

RSS

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*