Wanduugu wadau...nina swali dogo ambalo ningependa kupata jibu lake.
Swali lenyewe ni hivi....KATI YA WANAUME NA WANAWAKE NANI WANAONGOZA KWA MATENDO MABAYA?
Tags:
Wanawake ndo wanaongoza. Kazi kuvaa nguo za kubana matako tu ili kututamanisha
Me nafikiri swali hili lina nia ya kumhukumu mtu Mungu mweewe ndio anajuwa nani mzuri na nani mbaya si wanaadam hatuna uwezo huo na kamawataka kupata jibu jiangalie mwenyewe kuanzia mavazi mpaka matendo yako kisha jihukumu utapata jibu.
Hata mimi sijui swali limelenga matendo gani hasa, lakini kifupi matendo mabaya hayana mtu, jinsia, kabila au taifa fulani. Mfano unaweza kusikia Wahaya! ahh malaya sana lakini wote wanaojiuza ni wahaya? au wazalamo wanapenda sana ngoma wakati numesahau kuwa wewe unaishi Dar es salaam ambako ndipo makazi yao, ndio maana unashuhudia shughuli zao lakini bado ukienda kwenye mikoa mingine utashuhudia aina nyingine za ngoma zinazotokana na tamaduni za jamii husika. UBAYA HAUNA KWAO.
Ha ha ha ha wadau mbona wengine mnakwepa kujibu. Swali li wazi kabisa, hakuna sababu ya kujiumauma.
Mimi labda nijibu kwa kuanza kusema....Sisi wanaume ndio tunaoongoza kwa matendo mabaya hapa duniani.
Mfano wa kwanza; Katika simulizi ya kuteswa na kuuwawa msalabani kwa YESU KRISTU, inaonesha waliopanga mpango ule wa kumtesa, kumdhihaki, na hata kumuua walikuwa wanaume. Katika kisa kile sijaona sehemu akitajwa mwanamke kushiriki kumtesa, kumsaliti, na hata kumuua. Katika kisa kile wanawake walionekana kumhurumia YESU huku wakilia kwa uchungu alipokuwa msalabani.
Mfano wa pili; Mauaji ya viongozi wa kisiasa, wanaharakati, na watu maarufu hapa duniani. Kwa kiasi kikubwa wanaume ndio tulio mstari wa mbele. Laurent Kabila--aliyekuwa Rais wa Congo; aliuwawa na mwanaume. Martini Luther King--mwanaharakati aliyepigana vita dhidi ya ubaguzi wa rangi; aliuwawa na mwanaume.
Peter Tosh--mwanamuziki wa Reggae ambaye alikuwa anaunda kundi lile la The Wailers; aliuwawa kwa risasi na aliyetekeleza mpango ule ni mwanaume. Waliomuua Lucky Dube kule South Africa--walikuwa wanaume.
Mfano mwingine ni matendo ya aibu ubakaji, ulawiti, nk. ambayo hata hapa tulonge huwa tunayasoma; ni majuzijuzi hapa MKUU wa kijiji hiki alituletea ile post ya yule Mchungaji wa DODOMA kumjaza mimba mtoto wa shule.
Yapo mengine mengi sana ambayo nikianza kuyaelezea hapa, wengine watakosa nafasi ya kuandika maoni yao.
Ubaya wote tunao (wanawake/wanaume)--lakini kwa kiasi kikubwa sisi wanaume ndio tunaoongoza.
Hata mimi nikija kuuwawa aidha kwa bunduki, au kwa namna ingine atakayekuwa kaniua atakuwa ni Mwanaume.
**Tuepuke majibu rahisi kwa maswali magumu**.
PamoJah ktk kujenga kijiji.
Hahahahah Mama Malaika kumbe Severin ndio zake hizo?! kamrithi Dis lol.
kaka ommy hata tuko pamoja, hata rutu wakati sodoma rutu alishawishiwa na wanae walewe ili atafute kizazi zaidi,
wanaume wamezidi bhana
© 2023 Created by Tulonge.
Powered by