Tulonge

KATI YA WANAUME NA WANAWAKE NANI WANAONGOZA KWA MATENDO MABAYA?

Wanduugu wadau...nina swali dogo ambalo ningependa kupata jibu lake.

Swali lenyewe ni hivi....KATI YA WANAUME NA WANAWAKE NANI WANAONGOZA KWA MATENDO MABAYA?

Views: 1613

Reply to This

Replies to This Discussion

Wanawake ndo wanaongoza. Kazi kuvaa nguo za kubana matako tu ili kututamanisha

Hili swali lina mstakabali wa aina gani? Matendo mabaya/mazuri ndo nini? Wizi, ubakaji, kulawiti?

Me nafikiri swali hili lina nia ya kumhukumu mtu Mungu mweewe ndio anajuwa nani mzuri na nani mbaya si wanaadam hatuna uwezo huo na kamawataka kupata jibu jiangalie mwenyewe kuanzia mavazi mpaka matendo yako kisha jihukumu utapata jibu.

Hata mimi sijui swali limelenga matendo gani hasa, lakini kifupi matendo mabaya hayana mtu, jinsia, kabila au taifa fulani. Mfano unaweza kusikia Wahaya! ahh malaya sana lakini wote wanaojiuza ni wahaya? au wazalamo wanapenda sana ngoma wakati numesahau kuwa wewe unaishi Dar es salaam ambako ndipo makazi yao, ndio maana unashuhudia shughuli zao lakini bado ukienda kwenye mikoa mingine utashuhudia aina nyingine za ngoma zinazotokana na tamaduni za jamii husika. UBAYA HAUNA KWAO.

Ha ha ha ha wadau mbona wengine mnakwepa kujibu. Swali li wazi kabisa, hakuna sababu ya kujiumauma.
Mimi labda nijibu kwa kuanza kusema....Sisi wanaume ndio tunaoongoza kwa matendo mabaya hapa duniani.
Mfano wa kwanza; Katika simulizi ya kuteswa na kuuwawa msalabani kwa YESU KRISTU, inaonesha waliopanga mpango ule wa kumtesa, kumdhihaki, na hata kumuua walikuwa wanaume. Katika kisa kile sijaona sehemu akitajwa mwanamke kushiriki kumtesa, kumsaliti, na hata kumuua. Katika kisa kile wanawake walionekana kumhurumia YESU huku wakilia kwa uchungu alipokuwa msalabani.
Mfano wa pili; Mauaji ya viongozi wa kisiasa, wanaharakati, na watu maarufu hapa duniani. Kwa kiasi kikubwa wanaume ndio tulio mstari wa mbele. Laurent Kabila--aliyekuwa Rais wa Congo; aliuwawa na mwanaume. Martini Luther King--mwanaharakati aliyepigana vita dhidi ya ubaguzi wa rangi; aliuwawa na mwanaume.
Peter Tosh--mwanamuziki wa Reggae ambaye alikuwa anaunda kundi lile la The Wailers; aliuwawa kwa risasi na aliyetekeleza mpango ule ni mwanaume. Waliomuua Lucky Dube kule South Africa--walikuwa wanaume.
Mfano mwingine ni matendo ya aibu ubakaji, ulawiti, nk. ambayo hata hapa tulonge huwa tunayasoma; ni majuzijuzi hapa MKUU wa kijiji hiki alituletea ile post ya yule Mchungaji wa DODOMA kumjaza mimba mtoto wa shule.
Yapo mengine mengi sana ambayo nikianza kuyaelezea hapa, wengine watakosa nafasi ya kuandika maoni yao.

Ubaya wote tunao (wanawake/wanaume)--lakini kwa kiasi kikubwa sisi wanaume ndio tunaoongoza.

Hata mimi nikija kuuwawa aidha kwa bunduki, au kwa namna ingine atakayekuwa kaniua atakuwa ni Mwanaume.

**Tuepuke majibu rahisi kwa maswali magumu**.

PamoJah ktk kujenga kijiji.

Mkuu CHA the..... jina lako gumu bhana, Mie sikubaliani na wewe ukitaja kuchukuwa history ya bible anza kwa Adam na hawa nani alianzisha mambo mabaya? Kushawishi ni nani? Mpaka wakala tunda?, tukirudi kwa Irahim na mkewe Sara alimshawishi alale na mfanyakazi wake ili amzalie mtoto, nani mshawishi mkubwa?. Haya turudi kwa Esao Babu yake Omar Esao alivyokosa baraka za uzao wa kwanza kisa mama yao alipomsiki mumewe akimwambia Esao aende nyikani akamuwindie mnyama na amtengeneze vizuri kama afanyavyo ili alea ashibe ili ambariki, mama akamwambia mdogo akamate mbuzi zizini akamtengenezea hatimae mdogo akapa baraka za uzao wa kwanza na ndio vita hiyo isioisha mpaka sasa palestna na izirail mwanamke ndio chanzo cha vita hiyo. So ubaya hauna kwao wala rafiki jinsia wala jabila ba usianzie kwa Yesu anzia kwa Abraham au Ibrahim Baba wa imani kisha ndio ufike kwa Yesu mifano yako imeanzia katikati sio mwanzo. Usafi wa mtu anaujuwa Mungu pekee na sio wanaadam.
Severin ndio anaoongoza, kutwa macho kwa wanawake na mabinti wa jirani zake hadi house girls kawamung'unya wote. Teh teh teh teh.....

Hahahahah Mama Malaika kumbe Severin ndio zake hizo?! kamrithi Dis lol.

kaka ommy hata tuko pamoja, hata rutu wakati sodoma rutu alishawishiwa na wanae walewe ili atafute kizazi zaidi,

Hili swali linaupana mkubwa sana!!! Kila mtu anamtazamo wake na maoni binafsi jinsi aonavyo yeye.. Nadhani nikuheshimu maoni ya mwingine na kutoona wewe unamaoni bora kuliko mwingine.. Nijinsi kila mtu aonavyo..

Kwa upande wangu nimeangalia swali kwa makini.. Linauliza "KATI YA WANAUME NA WANAWAKE NANI WANAONGOZA KWA MATENDO MABAYA?"

Kwa hiyo sote tuna matendo mabaya... ila swali ni JE NANI ANAONGOZA ? Kipimo cha hilo swali kweli sikijiui ila Tujiangalie wenyewe binafsi ndiyo tujue .. Je Mimi kwa jinsia yangu Naongoza kwa matendo mabaya ? Jibu unalo mwenyewe...

Nukuta!!!

wanaume wamezidi bhana

Dah! Me naona kwa sasa wote sawa nakama sikosei wanaume tunakwenda kuwazidi wakina dada zetu, sory jaman Kwa yule atakaye ona nimemkwaza ila nawambia vijana wenzangu tubadlike tunapo kwenda sio!

Reply to Discussion

RSS

© 2023   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*