Tags:
Msanii kioo cha jamii ni kweli kabisa,lkn si wasanii wa hapa tanzania wamekuwa ovyo sana ktk shughuli zao na hata nnje ya shughuli zao za move.wanajichubua,wanasuka nywele zao na mambo mengi tu ya ajabu hawa ni kwa upande wa wanaume,Na upande wa wanawake ndio balaa kabisa mavazi yao yamekuwa hatari sana.
kuna wasanii wengine ni washamba tu,yaani wakifanikiwa kuingia katika ulimwengu wa sanaa wandhani basi huko ndio sehemu ya kushoboka na kuwademua mademu kwa fujo.na mademu nao wakifika huko basi wanacharuka na kudhani huko ndio sehemu ya kuchange mamen.badala ya kuwa kama kioo wanapokuwa katika fani hiyo ili waigwe wanaitumia nafasi hiyo kusaka magonjwa na udaku udaku.
wengine badala wakue kisanii wanazidi kuwa chini na kupoteza umaarufu wao.sijui ni ubongo ndio unaowasumbua au tatizo ni nini.
mi nadhani labda wengine wanavamia fani maana ninavyoajua fani hii ukiisomea huwezi kuw amcharuko kihivyo,maana utafundishwa katika shule ya fani hii maadili na heshima,silaha hizi mbili ukizizingatia wakati unaigiza utafanikiwa na siku zote utakuwa juu,jamii itajifunza kutoka kwako na kukufanya kioo cha jamii.
lakini ikiwa heshima mgogoro maadili tabu,unadhani nani atakuwa tayari kujifunz akutoka kwako.watu hatuko tayari kujifunza matatizo bwana.
© 2021 Created by Tulonge.
Powered by