Tulonge

Kumbe ukweli nao una ulimi, unaweza kuzungumza !

Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Kijeshi na mshauri wa zamani wa dikteta aliyeuawa wa Libya Kanali Muammar Gaddafi amesema kuwa Imam Mussa Sadr aliuawa na kiongozi huyo wa zamani wa Libya. Muhammad al Khidhar ameiambia televisheni moja ya Misri kwamba, kiongozi huyo wa kidini wa Lebanon aliuawa kwa amri ya Gaddafi ambaye alikuwa amemwalika nchini humo.

Muhammad al Khidhar amesema kuwa alimsikia kiongozi mmoja wa ngazi za juu wa utawala wa Libya akisema kwamba aliamrishwa na Gaddafi kumuua Imam Mussa Sadr, baada ya kujiri mjadala na mabishano makali baina ya Musa Sadr na Muammar Ghadafi , dikteta wa zamani wa Libya ambaye kwa sasa ni marehemu.

Mjadala huo ulihusu itikadi potofu ya Ghadafi ya kutaka kubadili baadhi ya aya za Qur'ani. Mshauri wa zamani wa Gaddafi amesema kuwa, katika mjadala huo mkali dikteta wa Libya alisema:

"Kama utume usingehitimishwa basi mimi pia ningekuwa mtume!".

Al Khidhar ameongeza kuwa baada ya kuuawa Imam Sadr, vyombo vya usalama vya Libya vilichukua hatua ya kuficha mauaji hayo kwa kutuma mavazi yake nchini Italia ili kuudanganya ulimwengu utambue kuwa Imam huyu hakuuawa nchini Libya.

Al Khidharna ameongeza kwamba, kuuawa kwa dikteta Gaddafi kutatatiza utafiti na kazi ya kuweka wazi zaidi taswira halisi ya mauaji ya Imam Mussa Sadr.

 

Ripoti hii inaweza kuleta huzuni kubwa katika nyoyo za wale wenye upendo kwa Shakhsia hii kubwa ya Kiislamu, si  kwa wa-Lebanon tu , bali pia kwa watu  wote wema wa duniani kote, waliokuwa wakisubiria kwa hamu kubwa kumuona tena Imam Musa Sadr akiwa huru uraiani.

Inafaa kuashiria hapa walau kwa ufupi kuwa Imam Musa Sadr aliingia nchini Libya Agosti 5, 1978, akiwa pamoja na Sheikh Muhammad Yaaqub  na Mwandishi 'Abbas Badr al-Din'.Walienda kukutana na Viongozi wa serikali ya Libya wakiitikia mwaliko rasmi uliotolewa na serikali ya Libya.

Imam Musa Sadr alitakiwa kukutana na Gaddafi tarehe 29 au 30 ya mwezi huo wa Agosti.

Lakini,watatu hao,kamwe hawakusikika tena tangu siku hiyo.

Maafisa wa Libya baadae walidai kwamba Gaddafi aliamua kuhairisha kukutana na Imam Musa Sadr,kisha Sadr akasafiri zake kuelekea Italia.

Lakini leo hii ukweli nao umeonyesha kuwa una ulimi,na unaweza kuzungumza,hasa baada ya Muhammad al Khidhar kuiambia televisheni moja ya Misri kwamba, kiongozi huyo wa kidini wa Lebanon aliuawa kwa amri ya Gaddafi ambaye ndiye aliyemwalika nchini humo.

 

Na Chalii a.ka IL-YA

Views: 917

Reply to This

Replies to This Discussion

Wanasema ulimi kiungo kidogo lkn matatizo yake makubwa

Ujue hakuna kitu kibaya kama kuua kiongozi wa dini kwa ajenda zako. Ukiwa unafatilia vyombo vya habari vya nchi za kiarabu utashangaa jinsi Gadafi alivyokuwa na sifa ya uuaji na ndio maana waarabu wenzie walimtenga. Nimekuwa nikisoma magazeti ya warabu kipindi Libyan Revolution ilipoanza, Gadafi alianikwa sifa zake zote mbaya.

Tatizo vyombo vya habari vya kiafrika vimekuwa viki-mpamba kumpa sifa nzuri na hata siku moja hutosikia habari kama hizi kwenye za Gadafi.

Hivi IL-YA mkwe wangu, ugomvi wa Gadafi na mfalme wa Saudia uliishaga kweli?

Mkwe,mara nyingi hata mimi nimekuwa nikisikia Ghadafi akisifiwa sana na nchi za Afrika,najiuliza hivi kwanini Africa wanashindwa kumsoma Ghadafi na kumtambua.Lakini nilichokuja kukigundua ni kuwa Ghadafi alikuwa mjanja sana kwa kuanzisha miasasa mbali mbali katika nchi hizi za africa na kuwateka akili baadhi ya wanaokubali kutekwa akili zao kupitia ushawishi wa misaada ili kwa kufanya hivyo aweze kujisafisha jina lake na kujifanya mtu mwema.Tanzania zama hizo vikosi vya ghadafi viliua sana watanzania vikimsaidia IDI AMINI DADA,baadhi ya askari wake walitiw ambaroni na vikosi vya Tanzania vilivyo ukomboa mji wa Kagera,kisha baada ya vita Ghadafi akajifanya Rafiki wa Tanzania na kuja kujenga miskiti kama ule uliopo mjini DODOMA unaoitwa kwa jina la MSIKITI WA GHADAFI.Hii yote ni kujiosha tu na kuficha maovu yake hana lolote,angelikuw ana utu asingeliua kw akulipua watu karibi 250 waliokuwa kwenye ndege ambapo baadae alikuja kutoa mabilioni ya Dola ili kufidia vifo hivyo kwa wamarekani.

 

Kuhusu waarabu ,ni kwamba yeye hakuwa na urafiki na waarabu wenzake,bali alikiwazunguka na wakati mwingine kusaidia waasi ili wapambane na serikali zao kama alivyokuwa akifanya huko sudan,na rais wa sudan kafichua wazi kuwa sudan iliwasaidia wanamapinduzi wa Libya silaha ili waendeleze mapambano dhidi ya Ghadafi kwa kuwa na yeye alikiwasaidia waasi ili waiangushe serikali ya Sudan.

 

Si sudan tu bali pia mataifa menigine ya kiarabu yanamchukia kupita kiasi ,yeye ndiye aliyekuwa akisaidia wafuasi wa chama cha BA-ATHI cha sadamu husein huko Iraq ili waendeleze milipuko na mapambano dhidi ya mashia na serikali ya sasa ya Iraq.

 

Saudia huko nako alikuwa hatamaniki,ndio maana tangu nizaliwe siwajawahi kusikia kashiriki katika IBADA YA HIJA YA KILA MWAKA maana anajua yeye na utawala wa Saudia hazipandi wanaweza kumkata kidefu ikiwa atakwenda maeneo hayo.

 

kwa ujumla Ghadafi alistahiki  kupata alichokipata  kabla ya mapinduzi haya ya Walibwa.

Reply to Discussion

RSS

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*