Tulonge

KWA NINI MISAADA KUTOKA NCHI ZA MAGHARIBI KWA AFRIKA ISIITWE 'DEAD AID' ?!Ndugu Mdau, leo hii naomba tulitizame Bara la Afrika.Tuzungumze walau kwa ufupi kuhusu Afrika. Kuna maudhui kibao yanayohusu bara la Afrika. Lakini hatuwezi kugusia maudhui yote.

Hivyo tutosheke na maudhui hii moja tu muhimu kuhusu bara hili lililobarikiwa zaidi kwa kupewa wingi wa dhahabu, almasi, shaba, madini ya uranium na mali asili kibao ambazo nitachoka nikianza kuzitaja sehemu hii!. Ningependa maudhui hiyo iwe ni maudhui ya misaada kwa bara la Afrika!.

Binafsi natatizwa na kukanganywa na suala la misaada kutoka G8 au taasisi zingine za Magharibi kwa ajili ya kuzisadia nchi kadhaa za bara hili la Afrika!.

Iko wazi kwamba: Mpango huo wa kuyasaidia mataifa ya Afrika yanayokumbwa na hali mbaya kiuchumi umeanza kitambo, lakini  pamoja na hayo bado nchi nyingi zinaendelea kunyemelewa na kuvamiwa  na umaskini tena ule umaskini wa kupindukia pamoja na kwamba kuna  mifuko mbalimbali ya misaada kwa ajili ya nchi hizo ndani ya bara la Afrika!.

Hilo hupelekea wengi waamini kuwa misaada hiyo haifanya kazi yoyote maana badala ya kusaidia kupungua kwa umaskini unaozikumba baadhi ya nchi za Kiafrika, inakuwa ni kinyume chake.! Je kuna tabu ipi ikiwa tutaisifu misaada hiyo kuwa ni misaada iliyokufa, maana kilichokufa kawaida hakifanyi kazi!.

Binafsi nathubutu kusema kuwa misaada toka nchi za Magharibi kwa  nchi za Afrika imekuwa ni sababu ya kuziletea umaskini na kuzidhoofisha nchi za Afrika!. Huo ndio mtazamo wangu. Na si mimi tu mwenye mtazamo kama huo peke yangu, bali hata wasomi wakubwa waliobobea katika masuala ya kiuchumi, wanathibitisha wakisema: "Western aid to Africa has not only perpetuated poverty but also worsened it".

Ndugu mdau, wewe kwa muono na kwa mtazamo wako, unadhani kwa nini mpaka sasa misaada hiyo ya nchi za Magharibi inashindwa kumaliza utata wa kiuchumi unaozikumba nchi pande za Afrika! bali pia misaada hiyo kuoenekana ni mwiba kwa nchi hizi za Afrika?.

Nina imani kuwa kwa kuwa sisi ni sehemu ya Bara tajiri la Afrika, basi bila shaka tutakuwa na fikra, wazo na hata ushauri kunako hali hiyo mbaya inayolikumba bara letu tajiri la Afrika linaloongoza kwa kupokea misaada toka pande za Magharibi!.

Ndugu mdau, unaweza kusaka kitabu kiitwacho: "Dead Aid: Why Aid Is Not Working and How There is a Better Way for Africa".

Kitabu hicho kimeandikwa na mwanadada mmoja wa Kiafrika ambaye ni msomi mkubwa wa uchumi kutoka Zambia. Msomi huyu kwa jina anaitwa: Dr. Dambisa Moyo.

Hali mbaya ya kiuchumi inayolikumba bara la Afrika yenye kusikitisha, imepelekea mwanadada huyo moto wa kuotea mbali katika fani ya uchumi kuandika kitabu hicho na kukiita: Dead Aid, akiuliza:"Why Aid Is Not Working and How There is a Better Way for Africa."

Bila shaka mtazamo wako unaweza kuleta mwanga na hatimaye kunisaidia mimi, huyu na yule kutegua kitendawili hicho kinachopatikana katika swali hili lifuatalo:

Why Aid Is Not Working and How There is a Better Way for Africa ?".

Na: Chalii IL_YA.

Views: 711

Reply to This

Replies to This Discussion

Hili gazeti naona hakuna aliyepita kulisoma, nimeona niweke kauli yangu hapa kabla hawajalibadili kuwa toilet paper!

Hahahhaaaa Eddie umepinda sana ww.

Sio kupinda @Dis!

Inaonekana wengi wetu humu wabongo mambo ya Africa kwa ujumla hayatuvutii sana hasa yakizingatia topic kama ya uchumi!

Wewe weka hapa topic ya under-blanket yaani hapatatosha hapa!

Eddie@ anasema kama ninavyomnukuu:

'Inaonekana wengi wetu humu (Yaani:Anakusudia wadau wa ndani ya Tulonge) wabongo mambo ya Africa kwa ujumla.......Wewe weka hapa topic ya under-blanket......"

***

Eddie@ kwa kauli yako hiyo umewadhalilisha na hata kuwavunjia heshima asilimia kubwa ya wanaTulonge,na kuwafanya waonekane akili zao siku zote ni akili zinazovutiwa na kukimbilia zaidi topic za UNDER BLANKET!.

Ndani ya Tulonge, kuna wasomi wakubwa,pia kuna watu kibao wenye busara zao,kuna watu kibao wenye fikra pevu,wenye mitizamo ya msingi,wasioendekeza mambo ya ajabu yasiyojenga kama hayo,hivyo wewe kama Eddie, unaposema kuwa:(( wengi wetu humu....)),tayari kwa kauli yako hiyo ushatuma  meseji kuwa wana Tulonge karibia wote  akili zao na fikra zao wanazitumia katika masuala ya kiajabu ajabu yasiyokuwa na faida kwa jamii kama vile kujadili masuala ya

Enewei,binafsi kama Chalii,simaini kama asilimia kubwa ya wadau wa Tulonge tuko hivyo kama ulivyotusifu ndugu Eddie!.

Kauli yako ni nyepesi kuizungumza kwa kukurupuka,lakini kuna watu ni wenye kuzingatia kauli na kuziweka katika fikra na kuzichambua,watu hao wakipitia kauli yako,hawataona ispokuwa meseji moja tu uliyokusudia kuwafikishia kuwa wao ni watu wa under Blanket la hakuna zaidi. Na si watu wote wanaoridhia kudhalilishwa,kuna watu wengine sometime hawana tabia ya kukubali kudhalilishwa kiwango hicho na kuipoteza heshima yao na hadhi yao.! Hivyo Mheshimiwa Eddie,@ itabidi uwaombe radhi wadau wa Tulonge,sawa sawa awepo katika wao anayekubali kudhalilishwa au asiwepo!.Nukta.

Eddie@ baada ya kuthibitika kosa lako la kuwavunjia wadau walio wengi (hapa Tulonge) heshima yao,narudi na kusema hivi:

"Forgive the shortcomings of {considerate people} because when they fall into error God raises them up".
Ikiwa kuna watu ambao asilimia kubwa ya akili yao huitumia kibusara,kihekima,na kuonekana mara nyingi kuwa ni watu wenye fikra,basi watu hao pindi wanapoteleza na kuanguka (kukosea) katika jambo lolote,iwe ktk fikra yao au mawazo yao,basi wasamehe watu kama hao,Sababu wanapoteleza na kuanguka (kukosea),Mola huwashika mkono na kuwanyanyua.

Na hii ni kwa sababu wao,asilimia kubwa ya tabia yao ni busara na ni watu ambao huitumia sehemu kubwa ya akili yao katika njia ya hekima na busara,hivyo kwa kuwa inatokea mara moja moja wanateleza katika ulimi wao na kuzungumza kilicho kinyume na hekima,basi usiwahukumu kwa kuteleza kwao na kuanguka,bali wasamehe tuuuuuuuuuuu, maana Mola wao huwatizama kwa jicho la huruma na kuwashika mkono na kuwanyanyua juu,na hatimae kuwafanya warudi katika ile sifa yao ya siku zote,nayo ni sifa ya watu wema,wenye busara na hekima katika kauli zao.
Na hivi ndivyo Mwanahekima Maarufu alivyonukuliwa katika kauli yake (amani iwe juu yake),ambapo alisema:
 "Forgive the shortcomings of 'considerate people' because when they fall into error God raises them up".

Brother Eddie@: Naamini wewe ni miongoni mwa wale watu ambao ni: {Considerate People}. Nukta.

Mwenye hekima alisema:

Unapo zungumza kauli nzuri,basi wewe ni mzuri zaidi ya kauli hiyo,na unapozungumza kauli chafu,basi wewe ni mchafu zaidi ya kauli hiyo chafu!.

"The doer of good is better than the good itself, and the doer of evil is worse than the evil itself."

Kama akitokea mtu ameona kama nimemtusi au kumdhalilisha kwa kauli yangu ntamuomba msamaha kwenye profile yake.

Naomba msamaha mkuu ILYA.

Najua wewe si mtu wa ugomvi...jina lako long form yake inasema yote.

I.L.Y.A.= I Love You All 

Nina dedicate wimbo huu wa Robert Nesta kwako mkuu.

http://www.youtube.com/watch?feature=player_detailpage&v=0sBrvh...

 

Mkuu Eddie@ nimefurahishwa sana reply yako iliyokuwa na nia nzuri,na moja kwa moja umenikumbusha kauli ya Jesus (P.b.u.h), maana "Jesus did not say we should forgive the offender when he or she is unwilling to apologize".

Hiyo kauli inaImply maana hii kwamba:Tunatakiwa kusamehe ikiwa tutaona dalili za kwamba mtu huyu ana nia ya kuomba msamaha,hii ni ikiwa sisi binafsi tutaona dalili hizo kwa mbali zinazoashiria suala hilo,ama ikiwa mtu mwenyewe ataomba msamaha,basi si kwamba tunatakiwa kumsamehe tu peke yake, bali pia ni wajibu kwetu sisi kumsamehe.

Naamini kwamba:All of human kind has an amazing capacity to forgive.Na hilo ni miongoni mwa sifa za kipekee za mwanadamu zinatomtofautisha  na kiumbe yeyote yule asiyekuwa mwanadamu.

Mwanafikra mmoja alisema:"The need for apologies permeates all human relationships."

There is one thing our lord  wants us to do it, and that thing is: We have to live each other in a good relationship.

 

Kaka Eddie@,pEEEEace!

Reply to Discussion

RSS

© 2023   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*