Tulonge

kwa nini mwanamke akijifungua, mwanaume anapunguza mapenzi?

nakwanini wanawake tukizaa tumbo linatepeta

 

Views: 4855

Reply to This

Replies to This Discussion

-Pia mwanamke huwa anapunguza mapenzi kwa mumewe kwasababu muda mwingi anakuwa bize na mtoto. Hali hii humpelekea mwanaume kupunguza mapenzi kwa mkewe bila kujijua.

-Kwa baadhi ya wanawake umbo zuri la mwanzo huupotea baada ya kujifungua,kama ulivyosema "tumbo kutepeta" nk. Hii husababisha mapenzi kupungua maana vile vigezo vya kimwili vilivyo mfanya mwanaume akupende hapo mwanzo hupotea baada ya kujifungua.

 

Tumbo kutepeta kunasababishwa na misuli ya tumbo ambayo hutanuka wakati wa ujauzito.Baada ya kujifungua misuli hushindwa kurudi ktk hali yake ya mwanzo.Hatimaye tumbo hubaki limetepeta.Hali hii hutofautiana kulingana na mwili mwanamke.

 

Note: SIYO wanaume wote wanaopunguza mapenzi kwa wake zao baada ya kujifungua.

 

Ngoja wakongwe wa mambo haya kama kina Alfan,Omary,Dunda,Kunambi nk waje kukupa pointi za maana zaidi,mimi nimevamia fani tu.

Sasa si anakuwa ameshakuwa mdebwedo, matiti kama kandambili. Sasa mapenzi yatoke wapi?
Severin unachosema sio kweli! hapo kuna factors nyingi sana! 1. unakuta mwanamke kujiweka safi, kama akishamaliza kunyonyesha anatakiwa kuoga au kujiosha c unajua maziwa huwa yana harufu? unakuta mwanamke ananyonyesha then cku nzima hajaoga unafukiria unaweza kuwa nae jirani kutokana na ile harufu!
Kwa kweli mi naunga mkono hoja ya kaka Tulonge kwa kiasi kikubwa ameeleza kiundani kabisa

Hapa kikubwa ni mwanamke kujitunza tu!! Hakuna kitu kingine.. Mwanamke ni "pambo" au niseme ni "UA" tena niseme ni UA  maalumu kwa mwanamme!! Sasa hilo UA bila "Matunzo" lazima litapoteza mvuto tu! Mwanamke asipo jitunza na kujiweka vizuri bila hata ya kujifungua.. akipoteza mvuto, vile vigezo vilivyopelekea kumpata huyo mme au bwana.. Basi mwanamme anapunguza mapenzi kama si kumkimbia kabisa!!

 

Kuna mifano "hai" ambayo tunaona wapenda nao mpaka wamefikisha umri wa uzee.. lakini mapenzi yao utadhani wamekutana LEO..  Mwanaume kupunguza mapenzi mwanamke anapojifungua ni hulka ya mtu binafsi, mwanamke nae huweza sababisha hali hiyo kutokea!!

 

Nimtazamo wangu tu!!!

Severin... Severin... ngoja nilete bakora. Nani alikwambia hivyo? Mbona wengine tumezaa na hatuna hizo kandambili? 

 

Wanawake wengi (hasa sie weusi) tunapojifungua muda mwingi tunajisahau na kusingizia kazi nyingi, kukimbizana na watoto hivyo mwanamke haujali mwili wake na pia hana muda wa kuwa na mumewe.

 

Mie ni mmoja wa wanawake waliojifungua, sikuwahi kuwa na msichana wa kazi (kama unavyojua mambo ya kuzalia watoto Uingereza) na bado sikuusahau mwili wangu na pia niliweza kuwa na muda na mume wangu. Na bado hadi leo mume wangu jicho lake halichezi mbali nami, na hata nikisema naenda sehemu peke yangu kiroho kinam-pwita na wakati mwingine anabadiri ratiba yake na kutaka kwenda nami huko nakokwenda. Mie ni mtu wa mazoezi na pia huwa niko makini sana kwenye chakula (sili junk food wala sinywi pombe) kitu ambacho kimesaidia sana kutunza mwili na ngozi yangu na Kipindi napojifungua huwa naendelea na mazoezi kama kawaida hasa ya tumbo kusaidia kukaza misuli. Na hiyo imenisaidia sana kutunza shape yangu na pia physical appearance kwa ujumla kwani watu wengi wanionapo wanafikiri mie bado kibinti kumbe mwenzao ni kijeba.   

 

Mwanamke unapojifungua iwapo unautunza mwili wako vizuri na kutojisahau daima mapenzi na mumeo yataendelea kama kawaida na yaweza ongezeka (kwani umemzalia mtoto), labda uwe tu una mwanaume kipepe mwenye macho juu juu tokea mwanzo.

USHAURI wangu ni kwamba usibwete na kujisahau. Mume anarudi toka kazini anakukuta unanuka maziwa na mijasho hapo hata kama anakupenda vipi hayo mapenzi yatapungua. Mwanamke daima kuupenda mwili wako hata kama umejifungua. Na pia usipende kufanyiwa kila kitu na msichana wa kazi (housegirl) au nduguzo kwani kuinama kupiga deki nyumba nzima huku umebana/kaza misuli ya tumbo ni zoezi tosha. Ndio mwanamke anapojifungua matiti huwa nayo yanabadirika lakini iwapo anavaa sindiria nzuri (size ya kumtosha na sio mama nibebe) inasaidia matiti yake kutobadirika sana (Kulegea na kuanguka). Hivyo hata kama mtoto ananyonya kila nusu saa usisahau kuvaa sindiria kwani yasaidia sana. Pia usikubali kuuchia mwili wako ukutawale, wewe ndio wapasa kuutawala mwili wako (usiuachie mwili uumuke na kuongeza size ya nguo). Vitu hivyo vidogo vidogo (sindiria, size ya nguo, mazoezi na chakula) vinachangia sana kwenye muonekano wako dhidi ya mwanaume wako baada ya kujifungua. Mie watoto wangu nimejifungulia kwa wazungu ambako hawana utamaduni kama Africa ambako mwanamke akijifungua anawekwa ndani wiki nzima na kushindiliwa mitori na vyakula. Hapa Uingereza ukijifungua hakuna lele mama, kazi za ndani wazifanya mtindo mmoja siku unaporuhusiwa toka hospital. Shughuli zote hizo zasaidia kutunza shape ya mwili wako. Midwives wa hapa wanakuhimiza kufanya mazoezi (the first 4 weeks) kwani misulu inakuwa bado flexible na hiyo ndio siri ya tumbo la mwanamke aliyejifungua kurudia hali yake ya kawaida upesi. Ukichelewa mazoezi hizo first 4 weeks ulipojifungua inakuwa vigumu sana kwa tumbo lako kurudia hali ya kawaida. 

Emmanuel kula tano. Nimependa sana comment yako. Kitu kingine ni kwamba wanawake wengi wanapojifungua wanajisahau kuwa mwanaume naye anapaswa kupewa muda wake na sio muda wote apewe mtoto tu. Mwanamke anapsa kukaa mezani kula na mwaume wake muda wa jioni, wengi wetu tuko busy hata muda wa kukaa na waume wetu hatuna lakini simu ikiita wakuta mama anapokea na kumuweka mtoto pembeni na kuongea na simu hata nusu saa. Ujue kuna siku nyingine mwanaume anakuwa na siku mbaya kazini/kwenye biashara hivyo anatamani muda wa kazi uishe arudi nyumbani akaongee na mkewe ingalau stress ipungue, tatizo mume akirudi nyumbani anapokelewa na kuhudumiwa na housegirl, kisa mama mwenye nyumba yuko busy hata muda na mume hana ingalau kuongea naye kidogo, kuangalia TVnews au kujihusisha naye kwa njia moja au nyingine hivyo yabidi mume asubirie hadi muda wa kuingia kitandani usiku. Kwa wanaume wengi hiyo ni adhabu tosha na ndio chanzo cha kumfanya mapenzi yapungue hasa kama mwanaume alizoea kuwa na mkewe muda wote atokapo kazini kabla mke hajajifungua.

Emmanuel Kibassa said:

Severin unachosema sio kweli! hapo kuna factors nyingi sana! 1. unakuta mwanamke kujiweka safi, kama akishamaliza kunyonyesha anatakiwa kuoga au kujiosha c unajua maziwa huwa yana harufu? unakuta mwanamke ananyonyesha then cku nzima hajaoga unafukiria unaweza kuwa nae jirani kutokana na ile harufu!
Duuh!! mama Malaika naona umeshusha essay,asante kwa kutujuza mengi.Huyo Severin usiwe unamkawiza. Akiongea pumba tu,unamshushia bonge la KONZI bila kumuuliza chochote.

Reply to Discussion

RSS

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*