Tulonge

Kwa nini ni halali kwa muisilamu kuchinja kuku, na si halali kwa mkristu kuchinja kuku huyohuyo?

Point yangu ni kwamba; kuku akichinjwa na muisilamu mkristu anakula, lakini kuku huyohuoy akichinjwa na mkristu--muisilamu hali kwa madai kuwa ni haramu. Kwa nini?

Wakati ukijadili hilo, tembelea na hiyo link hapo chini.

http://www.faithfreedom.org/the-challenge/muhammad-the-rapist/

Views: 1841

Reply to This

Replies to This Discussion

Ha ha ha ha ha ha ha ha! Chaoga umenichekesha sana, inaonesha hata mbuzi kristu unakula weye!

chaoga said:

kuchinja ni kuchinja tu alimradi damu imetoka, tena siku hizi teknlojia imekuwa, watu wanachinja kwa mashine. huyo anaetafuta uhalali wa mchinjaji hana njaa KASHIBA huyo

No question about being "THE GREAT" whatsoever.Keep it up!Cha the Great said:

Asante Eddie kwa maoni. Maadili ya taaluma yangu yanafanya niseme hivyo nilivyosema. But I'm still and I will be the GREAT 4ever.

PamoJah

na heri ya mwaka mpya!

Ni kweli Chaoga siku hizi kuna hata baadhi waislamu wanaenda wenyewe machinjioni kununua "kiblaza" (nyama ya nguruwe). Maana ukianza kujiuliza kachinja nani .....kisu kama kimetumika kuchinjia nguruwe au wakati anachinjwa mchinjaji aligeukia magharibi au mashariki, alivaa kibagarashia au la nk!

Ukianza kujiuliza maswali haya umelala njaa!Chaoga wewe wasema kweli na haya mambo ya globalization leo uko mashariki kesho magharibi hivyo ukisema ufate uhalali wa mchinjaji utajikuta unaishia kuwa Vegetarian hasa sie tunaoishi nchi za west, waenda supermarket wakuta kuku/ng'ombe wote wamechinjwa kwa machine.

Mimi huwa nawashangaa sana hao wanaokataa kula kama kuku,mbuzi nk wakichinjwa na mkristo. Yani wanaona hiyo ndio dhambi kubwa wakati wanazini saaaaana, wanatoa mimba saaaaaaaaaaana,wengine wezi saaaaaaaana hayo yote wanaona sawa. Hebu kakojoeni mkalale kama mmekosa cha kuongea.

wewee cha... mie sichagui kitu kwenye kula ktk dunia hii labda kiwe kinanidhuru...wakwere wana msemo usemao CHONEKE GABWI

Hahahahah Chaoga inamaana gani? hiyo CHONEKE GABWI?

ila jamani hizi imani hebu tuziacheni kama zilivyo kila m2 angaalie anachokiamini

maana hakuna andiko lilisema kitimoto halali kuliwa watu ila wanaadam wanakula kwa kuvunja A kama wavunjavyo A nyengine ikiwemo ya 6 so hizi imani tusiingize sana humu kijijini si vyema sana kusema hawa ninani? wanakula nn? haina mana na inaleta uchochezi na chuki MWENYEZI MUNGU TULINDE.

Nimekupa salute CHAOGA.

chaoga said:

wewee cha... mie sichagui kitu kwenye kula ktk dunia hii labda kiwe kinanidhuru...wakwere wana msemo usemao CHONEKE GABWI

hizi hapali za udini, tazameni nigeria imeshakuwa mbaya, sisi tunamuamini mungu mmoja tu, tupendane,

@Bonielly, wa-Nigeria wakorofi sana, ni vichwa ngumu sana wale. Yaani wale wanahitaji kiongozi dictator.

Nadhani, majority hamjajiweka katika issue na uhalisia wa suali.

Suali hili lipo katika jamii yetu au laa!

Na kama lipo- jibu - kwanini ndio unalikuta suali halijajibiwa.

Sasa, mie nijaribu kama mtakubaliana na mie - IF NOT ,njia nyeupe..

Amri ya kuchinja katika uislamu iko wazi zaidi na ina maana yake.

Kwanza, kinyama kinachochinjwa lazima kielekezwe kibla.( ambako sala zote popote dunia its directions)

Kisu cha mchinjaji lazima kiwe kikali mno ili zoezi hili lisiwe gumu.

Lazima liwepo tamko la "BISMILAH RAHMANI RAHIM"yaani kinachochinjwa iwe kwa ajili ya MUNGU si mwengine yeyote, ndipo kihalalike kuliwa.

Na mchinjaji awe mwili safi ( hana JANABA)

NDIPO ,zoezi la kuchinja linakamilika.

HUKO EUROPE ,butcher nyingi zimeajiriwa waislamu kufanya kazi hiyo kwa makusudi kuondoa utata wa jambo hili.

Jee, tusaidieni UTARATIBU wa Ukristo unatoa maelekezo gani ya kuchinja ? NDIPO tuangalie njia ipi bora.

SI SUALA YA UBINAADAMU ILA HAPA MAELEKEZO YA KUHALALISHWA UCHINJAJI.

Hayo tu, nimependa kuweka maelezo yangu.

Kwaheri- HERI YA MWAKA MPYA....

We,Zaiban nawe maarifa yako kuhusu hilo ni haba,nani alikwambia si halali mkristo kuchinja??? Dini haijasema hivyo si ya ukristo wala uislaam,Muhimu atakayechinja akiwa anajua kuchinja,namaaanisha kama anajua masharti ya kuchinja si lazima achinje muislaam ndio kuku awe halali kuliwa.Kuchinja kuna sharti zake na si sahihi kwamba anayejua sharti hizo ni muislaam tu,sijui unanielewa pointi yangu.Tambua kwamba kuchinja kuna sharti zake kama vile kutaja jina la Mwenyeezi Mungu kabla ya kuchinja,na sharti zingine,na hizo sharti anaweza kuzikosea muislaam na akizikosea ni haramu kula nyama yoyote iliyotokana na kuchinjwa na muislam aliyekosea sharti za kuchinja,hivyo hata muislaam akichinja kuku kwa kukosea masharti ya kuchinja kuku atakuwa si halali,na ikiwa mkristo atachinja kwa kujali masharti hayo kuku ataliwa tu tena kwa mrija.

Ninavyozungumza hivyo sibahatishi bali natoa kwa vitabu vinavyozungumzia mas-ala ya kuchinja tena vya dini.zile kauli tulizozizoea kuziskia kwa wachache wa welimu ati lazima achinje muislaam si sahihi,mbona tukienda hotelini tunakamua makuku na kuagizia manyama tena bila kuuliza nani kachinja.???

Hivyo wale wote wenye fikra dhaifu kama hizo waziondoe kabisa maana ni fikra zilizooza.Mtu ambaye akichinja si halali kula nyama aliyochinja ni YAHUD TU,Huyo ndio utaweka ngumu kula vichinjo vyake,si Mkristo.

Yahudi ana kasoro zake zinajulikana,hata kwa vitabu vya dini,yahudi ni adui wa muislaam na mkristo na ni adui wa waumini wenye kuamini.Mayahudi ndio ambao Mwenyeezi Mungu kawaponda sana katika vitabu vyake na kuwahaidi adhabu kali mno,kwa kosa lao la kuwaua manabii wa Mungu,wamechuinnja sana manabii na walikigoma kuwakubali Manabii na kusema Manabii hao ni waongo.


Ama Muislaam na Mkristo ni watu wamoja kijamii na Mwenyeezi Mungu kawasifu wawilihawa kuwa wako karibu zaidi katika maisha yao.Mwenyeezi Mungu (s.w) kathibitisha hilo katika Qur'ann Tukufu pale aliposema:


"You will surely find the most intense of the people in animosity toward the believers [to be] the Jews and those who associate others with Allah ; and you will find the nearest of them in affection to the believers those who say, "We are Christians." That is because among them are priests and monks and because they are not arrogant".


Hii ni kwa kizungu ama kwa Kiswahili Aya ya Mungu inasema:

"Hakika utawakuta walio shadidi kuliko watu wote katika uadui kwa walio amini ni Mayahudi na washirikina. Na utawakuta walio karibu mno kwa "mapenzi" ni wale wanao sema: Sisi ni Wakristo. Hayo ni kwa sababu wapo miongoni mwao makasisi na wamonaki, na kwa sababu wao hawafanyi kiburi".


((Tazama Aya hiyo katika SuratulMaida:Aya ya 82.))

Katika Sura hii hii Aya ya 78,Mayahudi hao Mungu anazidi kuwalaumu na kuwaponda akitoa habari zao mbaya  akisema na kwamba manabii wengi hawakuwa radhi nao akiwemo Nabii Isa:Yaani Jesus:


"Cursed were those who disbelieved among the Children of Israel by the tongue of David and of Jesus, the son of Mary. That was because they disobeyed and [habitually] transgressed."


Kwa kiswahili:

"Walilaaniwa walio kufuru miongoni mwa Wana wa Israili kwa ulimi wa Daud na wa Isa (yesu) mwana wa Maryamu. Hayo ni kwa sababu waliasi na wakawa wanapindukia mipaka".


Hapo hajatajwa Mkristo,bali hawa mayahudi Mungu Muumba anatupa habari kuwa Hata Nabii Isa ambaye wenzetu wanamuita Yesu Kawalaani Mayahudi kwa uovu wao uliothibiti kihistoria tangu huko nyuma na kwa kukufuru kwao na kumshirikisha Mungu na kwa kuua kwao Manabii wa Mungu Muumba pindi walipokuwa wakitumiwa Manabii.Mwenyeezi Mungu anatupasha habari walivyokuwa wakifanya Mayahudi hao akisema:

"We had already taken the covenant of the Children of Israel and had sent to them messengers. Whenever there came to them a messenger with what their souls did not desire, a party [of messengers] they denied, and another party they killed."


Kwa kiswahili:

"Tulifanya agano na Wana wa Israili, na tukawatumia Mitume. Kila alipo wajia Mtume kwa wasio yapenda nafsi zao wengine waliwakanusha na wengine wakawauwa".


Tazama aya ya 70 ya Suratul-Maidah utazikuta habari hizi.

Mada hii imenivuta mpaka kusema haya yote ili kuondoa vumbi lililotanda katika baadhi ya wasiokuwa na elimu na kusema sema hovyo ati wamekufuru na hivyo si halali kuliwa vichinzo vyao,hao ni wavivu wa kujua,bali Mungu Muumba anasema Mayahudi ndio waliokufu na kulaaniwa,si wakristo,Wakristo ni Marafi sana wa Waislaam na Mungu Mumba kathibitisha hilo katoika Qur'an.So Stop Talking.

Kama hujalizika na jibu niulize.

Reply to Discussion

RSS

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*