Ninashangazwa sna na jamii ya sasa.Makalio makubwa ya mwanamke yamekuwa ni jambo la muhimu sana katika kukamilisha urembo wa msichana/mwanamke.Kwa sasa bila ya kuwa na makalio makubwa basi hata wewe mwenye huwezi jisikia raha,ndiyo maana wanaamua kunywa/kupaka dawa za kichina ili kuyanenepesha.
Ukitaka kuthibitisha hili,utaona wasichana wengi ambao wanajiamini wana makalio makubwa/mazuri huwa wanapiga picha huku wakonesha makalio yao. Wale wasiyo nayo hawawezi dhubutu kugeuza makalio yao yapigwe picha.Naomba maoni yenu.
Tags:
ni kwa vile wanajua kuwa wanaume wengi wa afrika hupenda wanawake wenye makalio makubwa
Me nashangaa?! hawa watu wanaopenda makalio makubwa ya nn? sasa haya mwanaume umeshapewa mzigo huo hapo 1wapo utaufanya nn? me naamini mwanamke ni yuleyule hayo makalio yasiwe kigezo kwanza ukiyafikiria sana unaweza kumkosea MUNGU maana utayatafutia kazi ambayo itakuwa kinyume na maandiko matakatifu
unaweza kuungana na sheitwan ukaingia motoni siwashauri kuyawaza sana hayo fanyeni ni viungo kama viungo vingine
ktk mwili wa mwanaadam kama vilivyokuwa vidole vilefu na vifupi na vinginevyo kwa wanaume na wanawake
MUNGU atuepushe na sheitwan atatupoteza maana ndani ya asari kuna nyuki.
Severin una mambo leo umeamua kutuletea ya makalio. Babu zangu wa unyanyembe walikuwa wana kamsemo 'Mwanamke bila wowowo na mbigili bado hajakamilika'. Mbigili walikuwa wana maananisha matiti, wowowo ni makalio na neno hili limekuwa likitumika unyanyembe miaka mingi sana. Na hata kwenye kuchumbia, mahari ilikuwa inatozwa nyingi kwa mdada aliyejaza.
Siku hizi watu wamezidi kipimo, makalio na matiti sio natural tena bali yananunuliwa dukani (sindano na vidonge). Kwa hawa wenzetu wamarikani weusi nafikiri Pop Culture ndio imechangia sana makalio sababu hata nyimbo zao nyingi wakuta wasichana dancers ni wale wenye makalio. Mie si mpenzi wa Hip Hop ila nimewahi sikiliza wimbo wa Sean Combs (Puffy Daddy - Big Ole Butt) kamsifia msichana mwenye makalio makubwa. Nakumbuka pia marehemu Christopher Wallace (Notorious B.I.G) naye baadhi ya nyimbo zake alikuwa akisifia makalio. Nafikiri ni kasumba waliyo nayo wanaume wengi weusi duniani ndio inayofanya wanawake wajisikie hawajakamilika bila ya kuwa na makalio makubwa.
Tatizo nyie wanaume/wavulana mnayafagilia sana makalio makubwa ndomaana na kina dada wanazidi kuyapenda.Unadhani bila nyie kuyapenda yangekuwa dili??
© 2021 Created by Tulonge.
Powered by