Tulonge

Kwanini makalio makubwa/mazuri ya msichana yamekuwa na sifa kubwa kwa msichana wa jamii ya sasa?

Ninashangazwa sna na jamii ya sasa.Makalio makubwa ya mwanamke yamekuwa ni jambo la muhimu sana katika kukamilisha urembo wa msichana/mwanamke.Kwa sasa bila ya kuwa na makalio makubwa basi hata wewe mwenye huwezi jisikia raha,ndiyo maana wanaamua kunywa/kupaka dawa za kichina ili kuyanenepesha.

Ukitaka kuthibitisha hili,utaona wasichana wengi ambao wanajiamini wana makalio makubwa/mazuri huwa wanapiga picha huku wakonesha makalio yao. Wale wasiyo nayo hawawezi dhubutu kugeuza makalio yao yapigwe picha.Naomba maoni yenu.

 

Views: 9916

Reply to This

Replies to This Discussion

ni kwa vile wanajua kuwa wanaume wengi wa afrika hupenda wanawake wenye makalio makubwa

hawa itakua wacheza picha za ngono tu
Tatizo nyie wanaume/wavulana mnayafagilia sana makalio makubwa ndomaana na kina dada wanazidi kuyapenda.Unadhani bila nyie kuyapenda yangekuwa dili??
coz man wanapenda sana hizo vitu

Me nashangaa?! hawa watu wanaopenda makalio makubwa ya nn? sasa haya mwanaume umeshapewa mzigo huo hapo 1wapo utaufanya nn? me naamini mwanamke ni yuleyule hayo makalio yasiwe kigezo kwanza ukiyafikiria sana unaweza kumkosea MUNGU maana utayatafutia kazi ambayo itakuwa kinyume na maandiko matakatifu

unaweza kuungana na sheitwan ukaingia motoni siwashauri kuyawaza sana hayo fanyeni ni viungo kama viungo vingine

ktk mwili wa mwanaadam kama vilivyokuwa vidole  vilefu na vifupi na vinginevyo kwa wanaume na wanawake

MUNGU atuepushe na sheitwan atatupoteza maana ndani ya asari kuna nyuki.

Severin una mambo leo umeamua kutuletea ya makalio. Babu zangu wa unyanyembe walikuwa wana kamsemo 'Mwanamke bila wowowo na mbigili bado hajakamilika'. Mbigili walikuwa wana maananisha matiti, wowowo ni makalio na neno hili limekuwa likitumika unyanyembe miaka mingi sana. Na hata kwenye kuchumbia, mahari ilikuwa inatozwa nyingi kwa mdada aliyejaza. 

 

Siku hizi watu wamezidi kipimo, makalio na matiti sio natural tena bali yananunuliwa dukani (sindano na vidonge). Kwa hawa wenzetu wamarikani weusi nafikiri Pop Culture ndio imechangia sana makalio sababu hata nyimbo zao nyingi wakuta wasichana dancers ni wale wenye makalio. Mie si mpenzi wa Hip Hop ila nimewahi sikiliza wimbo wa Sean Combs (Puffy Daddy - Big Ole Butt) kamsifia msichana mwenye makalio makubwa. Nakumbuka pia marehemu Christopher Wallace (Notorious B.I.G) naye baadhi ya nyimbo zake alikuwa akisifia makalio. Nafikiri ni kasumba waliyo nayo wanaume wengi weusi duniani ndio inayofanya wanawake wajisikie hawajakamilika bila ya kuwa na makalio makubwa.

Lilian umenena. Wanaume wangechukia makalio basi wanawake wala wasingehangaika na kuyapenda makalio

Lilian said:
Tatizo nyie wanaume/wavulana mnayafagilia sana makalio makubwa ndomaana na kina dada wanazidi kuyapenda.Unadhani bila nyie kuyapenda yangekuwa dili??

Reply to Discussion

RSS

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*