Tulonge

KWANINI NDOA ZETU ZINAHARIBIWA NA WAKWE ZETU AU WAZAZI WETU

kwa kweli kama mdau hichi kitu kinaniumiza kweli!!!.... kama kweli ww unanipenda kwa nini umpe nafasi mzazi wako aitawale ndoa yetu.

Views: 1192

Reply to This

Replies to This Discussion

Huko vijijini bado wako wakwe wengi tu wana gubu hasa wakija mjini kuwatembelea wanakuwa na kale katabia ka kizamani. Pia kuna makabila wakwe wana tabia mbaya sana. LOL....

Severin said:
Itakuwa ni tabia mbovu ya wazazi/wakwe husika. Ila sIdhani kama siku hz wazazi/wakwe wanachangia sana kuharibika kwa ndoa. Wengi wao wameshaachanga na mambo ya kujishikirikisha kwenye ndoa za wanao. Ishu kama hii ilikua inatokea kipindi cha nyuma kidogo.

I strongly agree with you. Mama wakwe wengi kwetu Africa hawapendi kuona wakwe zao wanaenda kutafuta riziki (kazi za kuajiriwa). Hata ile kupendeza ukanona tu kwa mama wakwe wengine ni kero. Na mambo ya kutoka na mumeo outings wengi wanaona kama mke ni wa kukaa ndani muda wote kulea watoto wake na sio kurudi usiku na mumewe.

 

Mie niko kwenye ndoa muda mrefu sasa na sina shida na mama mkwe bahati nzuri mume wangu anaamini ndoa ni ya watu wawili. Tamaduni ya wakwe zangu hata kuja nyumbani hawaji hadi wapate mualiko ingawa wanaishi dakika 30 toka nyumbani kwetu. Maisha yangu na mume wangu ni yetu hawaingilii chochote kile iwe masuala ya pesa au watoto.   

 


Babengwa said:

Kabla ya kufunga, ndoa nadhani jambo la msingi kuanza maisha ,mukiwa mko mbali na wazazi.

 Fitna iko , kwa wanawake wanapoishi pamoja na visa mamkwe husema au tutenda akiisahau nafsi yake kuwa yeye ni mama mzazi wa bwana na mamkwe kwa bibi.

 

Haina maana kabisa kuwatenga wazazi lakini hakutakuwa na shida zozote pindi BA mKWE mkiishi pamoja- hii ionekane - shida ipo kwa wanawake.

NDOA inafanyika hali ya kuwa ni watuwazima mkiwa na mfumo au sera zenu nje na "longolongo" ya kwenu( familia asili).

Kitendo cha mke kuangana na mume aenda kazini inatosha mamamkwe akajitia kati " anampumpaza mwanangu- sijui kama hamrogi ...."

Kitendo cha kutoa na wife kwenda super market - MAMKWE...." bibi anamfilisi mwanangu " Almradi kila hatua au move ndani ya maisha - mama huyu ataweka mdomo au malalamiko dhidi ya maisha ya watu.Mama bado yuko mbali kifikra bado yuko ' chama kushika hatamu..." kitu hakipo ukale na usasa vina msuguano....

 

HIZO NDIO ZANGU FIKRA BINAFSI....

 

 

Reply to Discussion

RSS

© 2023   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*