Tulonge

KWANINI NDOA ZETU ZINAHARIBIWA NA WAKWE ZETU AU WAZAZI WETU

kwa kweli kama mdau hichi kitu kinaniumiza kweli!!!.... kama kweli ww unanipenda kwa nini umpe nafasi mzazi wako aitawale ndoa yetu.

Views: 1192

Reply to This

Replies to This Discussion

Dada Latifa umefanya research juu ya hiyo ishu? Au imetokea kwa mtu mmoja tu.
Latifa wazazi ndo wanao wajua watoto wao,kama mkwe wake ni kimeo na hataki mwanae ahangamie lazima aseme,so mie nawatetea wazazi,na pia ni lazima tupime mawazo yao co kila jambo twakubali.
Mi nachojua mwanaume lazima uwe ngangari, siku zote wanaoharibu ndoa ni wanawake maana wana chochoko nyingi sana. sio mke wako sio mkwe maana wanawake wanapenda kufanyia kazi maneno ya watu, hawajui kuwa mengi hua batili hivyo bas jinsia ya kike acha umbea huaribu ndo sana.
@samson kwa kweli wanawake wakizidi zaidi ya 3 kunakuwa na chokochoko na pia nakubaliana na hilo kuwa mwanamume muwe ngagari
@emmanuel kaka ni kweli lakini kuwe na limitation ya haki ya wazazi , mkea na dadas napia kuna wazazi wanatokea kuwachukia wakwe zao kwa sababu nyingine zisizokuwa na msingi kama , mke hazai..........etc
@dismas believe me sio mmoja ni 65% ya ndoa kuvunjika ni wakwe hasa ndoa za pwani it ridiclous guys
kwa hilo sina cha kusema labda aulizwe baba Bright
In real akina dada ndio wenye kufanya mambo kuharibika ktk ndoa, na ndo wanamchango mkubwa wa kutengua ndoa kwa kufanya mambo yote kuwa makubwa, maana wanaume nao huambiwa maeno kibao na wazazi wao lkn huachana nayo yakapitia sikio la 2, japo hawabishi kitu lkn dada zangu huwa wakiambiwa jambo wanatamani hata waende redion ili dunia nzima isikie, na huwa hawakubali kushindwa au kutoa ushindi ili kuinusuru ndoa wao huwa wepesi kutoa maamuzi japo 90% ni hasara na 10% to ya hayo maamuzi ni noma, hebu kuwa mpole kama kondoo uone jinsi wakwe watakuogopa.
kifupi ni kwamba kwa mtazamo wangu, wanawake na wanaume ni 50% kwa 50% ukweli ni kwamba wapo wanawake waharibifu wa ndoa wapo wanaume waharibifu vilevile, na wapo wakwe ambao ni hivyohivyo, lkn malanyingi lazima kuna sababu ndizo zinazosababisha, kama vile mwanamke tangu aolewe ana miaka 6 hajazaa, manamke hajatulia mzee akitoka na yeye anatoka, kutokuipenda familia ya mumewe, na nk, naupande wa mwanamume, ulevi, kutokurudi nyumbani mapema, kitu kidogo ugovi kwa mkewe, kuwa na nyumba ndogo giza, na nk, hapo ndipo utawaona wakwe wakiingilia kati nakuvunja ndoa hao wanaona ni suruhisho, lknukiangalia kiundani hakuna anaehitajika lawama hakuna wazazi wanaowachukia wakwe zao kama wakwe watajenga heshima kwa wazazi wa mwezake ukijenga upendo, utaleta amani na furaha,

nakupeni mfn mmoja, mimi kaka yangu alikaa na mwanamke kama mwaka mmoja hivi, alikuwa hana mtt, ikaaza minong'ono ya chinichini yule si mke hafai hana mtt wenzake wote wamezaa, sasa sikumoja mama wa yule kaka yangu alilazwa, hapo ndipo yule mwanamke kakaa na mkwe wake hospital mpaka yule mama alipopona mtt wakike ajue mkwewe kala nini kanywa nini mpaka anatoka hospital leo nenda nyumbani mwambie mkwe hazazi hatufai, unaweza ukafukuzwa na kukanyaga hapo nyumbani usikanyage, yule msichana ndio mwanamke mzuri kuliko wote,

kifupi ndoa ni jinsi ya kujipanga na jinsi ya kuishi,
maisha ndio yanayochangia ndoa kuvunjika, au kuto vunjika, maisha ni jinsi unavyoishi, gud day
Itakuwa ni tabia mbovu ya wazazi/wakwe husika. Ila sIdhani kama siku hz wazazi/wakwe wanachangia sana kuharibika kwa ndoa. Wengi wao wameshaachanga na mambo ya kujishikirikisha kwenye ndoa za wanao. Ishu kama hii ilikua inatokea kipindi cha nyuma kidogo.
kwa hivyo wadau munacho sema kuwa sote tunahitaji tuwe imara tusilipe mwanya tatizo hili kwakukimbilia wakwe/wazazi wetu

Kabla ya kufunga, ndoa nadhani jambo la msingi kuanza maisha ,mukiwa mko mbali na wazazi.

 Fitna iko , kwa wanawake wanapoishi pamoja na visa mamkwe husema au tutenda akiisahau nafsi yake kuwa yeye ni mama mzazi wa bwana na mamkwe kwa bibi.

 

Haina maana kabisa kuwatenga wazazi lakini hakutakuwa na shida zozote pindi BA mKWE mkiishi pamoja- hii ionekane - shida ipo kwa wanawake.

NDOA inafanyika hali ya kuwa ni watuwazima mkiwa na mfumo au sera zenu nje na "longolongo" ya kwenu( familia asili).

Kitendo cha mke kuangana na mume aenda kazini inatosha mamamkwe akajitia kati " anampumpaza mwanangu- sijui kama hamrogi ...."

Kitendo cha kutoa na wife kwenda super market - MAMKWE...." bibi anamfilisi mwanangu " Almradi kila hatua au move ndani ya maisha - mama huyu ataweka mdomo au malalamiko dhidi ya maisha ya watu.Mama bado yuko mbali kifikra bado yuko ' chama kushika hatamu..." kitu hakipo ukale na usasa vina msuguano....

 

HIZO NDIO ZANGU FIKRA BINAFSI....

 

 

Reply to Discussion

RSS

© 2023   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*