Tulonge

Huu ndiyo uwanja wa maoni.Unaruhusiwa kumtwanga maswali,kumpa ushauri,kutoa lalamiko lako kwake,kuomba chochote toka kwake nk kwa kuzingatia maadili mema. Kazi kwako.

Views: 1998

Replies are closed for this discussion.

Replies to This Discussion

1. Kwanza niambie siri ya urembo wako

2. Nimeona jibu lako kuwa hujaolewa, je una watoto wangapi?

3. Umewahi kutoa mimba, jibu swali hili huku ukijua Mungu anakuona. Ukidanganya ni sawa na kujingezea dhambi mara dufu.

4. Dini zetu (Uislam na Ukristo) haziruhusu mtu kufanya tendo la ndoa kabla ndoa, je wewe umeweza kutimiza hili? Kama hujaweza, kwa nini?

 - Hayo ni maswali ya utangulizi, nitarudi tena na maswali zaidi ya hayo.

Angel kwanza unaishi mkoa gani? Umeshaolewa? wafanya kazi au wasoma?

habari za siku mpendwa ANGELA, natumaini unaendelea vizuri na maisha,

nina mashwali machache kwani mengi umeshaulizwa na vijana wenzio waliotaka kukuposa na kusema hauko tayari kwahilo,

1)angela unangoja nini kuolewa au unatafuta uewenyekiti wa makapera?

2)kutokana na hali ngumu ya maisha tulionayo watanzania tulio wengi, mpaka kufikia hatua ya wazazi wengine kushindwa kuzilea familia zao na kuzitelekeza na kuzalisha watoto wa mitaani na wengine kuwa ombaomba je ungepewa jukumu hili la kulitatua tatizo hili na serikali je ungefanyaje ili kulitatua janga hili?

2)MICHEZO, kutokana na nchi yetu kuwa nyuma kimichezo na kuitwa kichwa cha mwendawazimu, ili hali hatupendi kuwa hivyo, je angela ungeishauri nini TFF na serikali kwa ujumla, ili tuweze kusonga mbele kimichezo,

3)USAFI, naamini kwamba jiji letu la dar linaongoza kwa uchafu, na naamini kwamba wadau wa usafi wanajitahidi sana kwa kuliweka jiji hili katika hali ya usafi lkn wanachemka, je kama wewe ni mdau wa dar, ungetoa changamoto gani ili kulinusuru jiji hili, liwe na hadhi ya udar,

Pia unamchumba? na unaishi mwenyewe mwenyewe au na wazazi, au mwanaume?
Hongera Angela wangu kuwa mdau wa wiki. Itabidi nimwambie baba Malaika anunue Kalashnikov na tufuge na nyuki kabisa wa kukulinda maana macho yamekuwa mengi sasa. Ha haa haaaa

Ndugu yangu Emanuel Kibassa naishi Dar es salaam, bado sijabahatika ndoa kaka yangu na mimi ni mfanyakazi.

pia napenda kukujibu swali lako lingine la kwamba naishi na nani, mimi naishi na wazazi wangu na kuhusu mchumba yupo njiani anakuja.

Emmanuel Kibassa said:

Angel kwanza unaishi mkoa gani? Umeshaolewa? wafanya kazi au wasoma?

UMEONA MAMA EEEE MWAMBIE BABA AISEEE YANI NITAKUWA SICHEZI MBALI NALO ILI MTU AKIJA TUU ANAINGIA MTEGONI MWENYEWEEEEEEE
Mama Malaika said:
Hongera Angela wangu kuwa mdau wa wiki. Itabidi nimwambie baba Malaika anunue Kalashnikov na tufuge na nyuki kabisa wa kukulinda maana macho yamekuwa mengi sasa. Ha haa haaaa

KAKA SEVERINI LOL UMENITOA JASHO ILE  SANA ILA NI VIZURI NAANZA KUKUJIBU KAMA IFUATAVYO:

1. UREMBO WANGU SIRI YAKE NINATUMIA VITU VYA ASILI KAMA VILE MAFUTA YA KUJIPAKA NA SABUNI ZA KUOGEA NAMAANISHA SIJICHUBUI NA NDO MANA KAMA UONAVO NINA NGOZI AMBAYO WEWE MWENYEWE UMEITHIBITISHA KUWA NI YA UREMBO.

2. KWELI SIJAOLEWA ILA NINA WATOTO 2 WOTE WA KIKE

3. MIMBA SIJAWAHI KUTOA

4. NI KWELI KUFANYA TENDO LA NDOA KABLA YA NDOA NI DHAMBI KUBWA SANA NA MIMI KWA KWELI KANUNI HII KAMA MKRISTO NIMEENDA NAYO KINYUME HILI NAKIRI NI KOSA. ILA KAKA SEVERINI SIDHANI KAMA MAISHA YA SASA MTU ATAINGIA KWENYE NDOA KABLA HAJAFANYA TENDO LA NGONO.

ASANTE SANA HAYO NDO YANGU MAJIBU
Severin said:

1. Kwanza niambie siri ya urembo wako

2. Nimeona jibu lako kuwa hujaolewa, je una watoto wangapi?

3. Umewahi kutoa mimba, jibu swali hili huku ukijua Mungu anakuona. Ukidanganya ni sawa na kujingezea dhambi mara dufu.

4. Dini zetu (Uislam na Ukristo) haziruhusu mtu kufanya tendo la ndoa kabla ndoa, je wewe umeweza kutimiza hili? Kama hujaweza, kwa nini?

 - Hayo ni maswali ya utangulizi, nitarudi tena na maswali zaidi ya hayo.

Nakupongeza Angela kwa kumujibu kaka Seve. kihufasaha zaidi,ila ningependa niulize kwani ni kanuni kwamba mtu hawezi kuvuta subira hadi siku ya ndoa bila kujaribu tendo la ngono? basi kama faida au asara zipo,zitanabaishwe!

KAKA KADIRIELI MIMI SIJAMBO KABISA NA NINAENDELEA VIZURI NA MICHAKATO YA MAISHA. NAPENDA KUCHUKUA FURSA HII KUJIBU KAMA IFUATAVO:

1. WALA SITAKI KUWA MWENYEKITI WA MAKAPERA ILA SUALA LINAITWA NDOA NI MAAMUZI AMBAYO HUTAKIWI KUKURUPUKA TUU, INAHITAJIKA KUMSOMA MWENZIO,NA MOYO WAKO KURIDHIA NA BILA KUSAHAU KUMSHIRIKISHA MUNGU KWANI MAAMUZI MAZITO KWA KWELI UKIZINGATIA ZAMA HIZI MAPENZI YA DHATI HAKUNA WENGI TUMEKUWA WAONGO NA MATAPELI WA MAPENZI.

MAJIBU YANGU YAMEKUWA MAREFU KUTOKANA NA UGUMU WA MASWALI YAKO ASANTE MKUU

2. KUHUSU HILI TATIZO LA BAADHI YA WAZAZI KUSHINDWA KUZILEA FAMILIA ZAO IPASAVO NA HATIMAYE WATOTO KUWA OMBAOMBA AU WATOTO AMBAO TUNASEMA WAPO KWENYE MAZINGIRA MAGUMU MIMI KAMA ANGELA NINGESHUGHULIKIA SWALA HILI KAMA IFUATAVO:

A) NINGEISHAURI SERIKALI IWEKE SHERIA YA KUFUNGA KIZAZI CHA WAZAZI WA YULE MTOTO AU WALE WATOTO AMBAYO IWE NI LAZIMA NA BILA MAJADILIANO INGAWA VITABU VITAKATIFU HAVIRUHUSU  SWALA KAMA HILI ILA KWA KUOKOA WASIZIDI HII NDO DAWA TOSHA. NA WATAJULIKANA VIPI NI KUFANYA KAMATAKAMATA MTAA HADI MTAA AU JIJI AHADI JIJI NA KUWAULIZA WAZAZI WAO WAPO WAPI NA PALE MZAZI ATAKAPOTHIBITISHA KUWA YULE AU WALE NI WATOTO WAKE PALEPLAE NYOTA YA KIJANI INACHUKUA MKONDO WAKE.

B) KWA SASA KUNA VITUO VYAO SPECIAL VYA KUWAANGALIA HAWA WATOTO INGAWA WENGINE WAMETOROKA VITUONI HAPO NINA MAONI 2  KAMA IFUATAVO INABIDI KWA WALE WALIOTOROKA VITUONI WAPELEKWE JELA ZA WATOTO KULE WAWE NA KITENGO CHAO MAALUM AMBACHO WANASAIKOLOGIA WATAKUWA WAKIWAPA MASOMO TARATIBU WAO WANAELEWA JINSI YA KUDEAL NA MTU WA NAMNA HII. NA MWISHO NINGEISHAURI SERIKALI KUTENGA FUNGU KUBWA LA PESA ILI KUWEZA KUPUNGUZA WIMBI HILI NCHINI NA KUWABORESHEA MAZINGIRA YAO NA KUWEKA VITUO HIVI VYA WATOTO YATIMA KWA WINGI PIA KUWAAJIRI WATAALAMU WA KUWEZA KUWAPA WAATHIRIKA CANCELLING.

3) KUHUSU MICHEZO SIKU ZOTE NYUMBA INAANZA MSINGI NA MSINGI SI ILI MRADI MSINGI TUU UNAHITAJI VITU MUHIMU ILI UWE MSINGI IMARA USIJALI GHARAMA FANYA TARATIBU NA MSINGI UTAKUWA BORA, NAISHAURI TFF KUANZA KUCHEKI VIPAJI VYA WATOTO KUANZIA MASHULENI NA KUWEKA WATAALAMU WA KUWAFUNDISHA KANUNI NA TARATIBU ZA MICHEZO MTOTO HUYU ATAPENDA MICHEZO NA MCHEZO UTAKUWA KWENYE DAMU YAKE.

4) KUHUSU JIJI LETU LA DAR KUKITHIRI KWA UCHAFU NA HARUFU MBAYA HAPA MIMI KAMA MDAU WA USAFI NINGESHAURI SERIKALI IWEKE MAPIPA YA TAKA KILA MAHALI NA KILA BAADA YA HATUA FULANI KUWE NA PIPA LA TAKA NA PIA KUWE NA ASKARI KANZU WA JIJI AMBAO MTU AKIFANYA UCHAFUZI WA MAZINGIRA ACHUKULIWE HATUA YA KWENDA MAHAKAMANI BILA FAINI AKATUMIKIE KIFUNGO CHAKE KISICHOZIDI MIEZI SITA NA BAKORA TATU TUU UONE HUU MFANO AKIFANYIWA MTU MMMOJA KAMA WENGINE TUTAFANYA UCHAFUZI WA MAZINGIRA, MBONA MOSHI WAMEWEZA NI KWA VILE WAPO MAKINI NA WAMEAMUA.
kadirielly@yahoo.com said:

habari za siku mpendwa ANGELA, natumaini unaendelea vizuri na maisha,

nina mashwali machache kwani mengi umeshaulizwa na vijana wenzio waliotaka kukuposa na kusema hauko tayari kwahilo,

1)angela unangoja nini kuolewa au unatafuta uewenyekiti wa makapera?

2)kutokana na hali ngumu ya maisha tulionayo watanzania tulio wengi, mpaka kufikia hatua ya wazazi wengine kushindwa kuzilea familia zao na kuzitelekeza na kuzalisha watoto wa mitaani na wengine kuwa ombaomba je ungepewa jukumu hili la kulitatua tatizo hili na serikali je ungefanyaje ili kulitatua janga hili?

2)MICHEZO, kutokana na nchi yetu kuwa nyuma kimichezo na kuitwa kichwa cha mwendawazimu, ili hali hatupendi kuwa hivyo, je angela ungeishauri nini TFF na serikali kwa ujumla, ili tuweze kusonga mbele kimichezo,

3)USAFI, naamini kwamba jiji letu la dar linaongoza kwa uchafu, na naamini kwamba wadau wa usafi wanajitahidi sana kwa kuliweka jiji hili katika hali ya usafi lkn wanachemka, je kama wewe ni mdau wa dar, ungetoa changamoto gani ili kulinusuru jiji hili, liwe na hadhi ya udar,

okay, unamaana gani unavyosema anakuja, means upo single ama?

asalam alaikum dada hongera kwa kuwa mdau wa wiki mie nakuliza dada una mipango gani ya kusaidia jamii na kuwasaidia wazeee kama sisi na unataka dada wenzako wafanye nini ili kuendeleza gurudumu la kijiji kwa mfano kuwa na kikundi cha kina dada kitakacholeta umoja kijijini na kuwasaidia mayatima na wasiojiweza hapo tosha dada

RSS

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*