Tulonge

Huu ndiyo uwanja wa kumwaga lolote juu ya mdau wetu wa wiki kwa kuzingatia maadili mema.Kazi kwako mdau

Views: 791

Replies are closed for this discussion.

Replies to This Discussion

Haya sasa zamu yako dada; Na mimi nakutwanga maswali haya;

1). Wewe ni mzaliwa wa wapi? Kabila gani?

2). Kitu unacho kipenda sana katika haya maisha ni nini?

Ukinijibu haya nitakuuliza na mengine mengi tu mpaka uchoke.

Hongera kwa kuwa mdau wa wiki.

1. Umeolewa au bado single?

2. Nipe siri ya urembo wako

3. Ni mvulana gani unayempenda zaidi kama kaka yako hapa Tulonge?

Hongera dada,umependeza mno

nakujibu kaka Franco kama ifuatavyo:-

1) mimi ni mzaliwa wa Iringa, kabila langu mhehe

2) kitu nachokipenda sana katika maisha ni kubadilishana mawazo na watu mbalimbali wa rika lolote!

Ahsante kaka Franco nasubiri mawsali mengine kutoka kwako

BARAKA FRANCO CHIBIRITI said:

Haya sasa zamu yako dada; Na mimi nakutwanga maswali haya;

1). Wewe ni mzaliwa wa wapi? Kabila gani?

2). Kitu unacho kipenda sana katika haya maisha ni nini?

Ukinijibu haya nitakuuliza na mengine mengi tu mpaka uchoke.

Ahasante kaka Severin

1. Sijaolewa bado bado nipo nipo kwanza

2. siri ya urembo wangu nakula vizuri na kupumzika kwa wakati

3. kaka naye mpenda Mkuu (Tulonge) mwenyewe

Severin said:

Hongera kwa kuwa mdau wa wiki.

1. Umeolewa au bado single?

2. Nipe siri ya urembo wako

3. Ni mvulana gani unayempenda zaidi kama kaka yako hapa Tulonge?

kaka Remmy ahsante sana

Remmy Benson Mganga said:

Hongera dada,umependeza mno

Habari dada nyakunga, natumaini ni mzima wa afya teletele,

Maswali yangu kama ifuatavyo,

1)wewe ni mwenyeji wa wapi?

2)elimu yako ya awali na ulipifikia,

3)ni kitu gani ukipendacho zaidi kuliko ukikipata utafurahi,

4)na kitu gani ukichukiacho ukikiona utachukia mpaka basi,

5)je umeolewa? unafamilia yani watoto, na kama wapo ni wangapi?

6)je wewe ungekuwa kiongozi wa nchi hii yenye maziwa na asali lkn hali ni ngumu, je ungefanya nini ili hali hii ngumu iwe nyepesi?

7) je una ushauri gani kwa wanawake wanaopenda kukaana kubweteka na kuacha kujituma kisingizio wakidai ni elimu wakati wanao uwezo wa kujituma nakuondokana na mfumo dume?

8)je ungekuwa waziri wa jinsia na watoto, ungewasaidiaje watoto wanaofanya biashara, au kutumikishwa majumbani bila ya kusoma na kuwa na maisha mazuri kama waajiri wao?

9)na unaushauri gani kuusu hii brog yetu ili izidi kuwa juu zaidi, na kiongozi wake dismas aende samunge kwa babu samunge akapate kikombe cha babu,

10) na mwisho nakutakia maisha marefu na afya njema ili uweze kunijibu maswali yangu vizuri,,,,aksante boni kwa maswali yako... nimejishukuru mwenyewe,

Hongera dada Agnes Nyakunga..
Kwanza kabisa napenda kukupa hongera kuteuliwa kuwa mdau wa wiki dada Agness .Kamweneeeeeeee.Maswali mengi wadau wameshakuuliza mimi nikutakie kila la kheri katika wakati wako huu wa kua mdau wa tulonge kama nitapata swali la kukuuliza nitakutwanga hapo baadae dada.Ninakutakia majukumu mema

niko salama

1. mimi mwenyeji wa Iringa

2. elimu yangu ni sekondari 'O' level na nimesoma chuo cha magogoni P/S (personal Secretary)

3. Kitu ni kipendacho kiko ndani ya moyo wangu natumai siku nikikipata nitafurahi sana

4. kitu nikichukiacho kuona wanawake wanaojiuza ovyo sasa hivi kila kona watoto wadogo sana wanajiuza nachukia sana

5. cjaolewa, ila na watoto mapacha

6. ningekuwa kiongozi wa nchi wa nchi hii yenye maziwa na asali nyingi, kwa mtizamo wangu kwanza ningewashauri wananchi wangu kuzalisha asali kwa wingi na kuwatafutia masoko mbalimbali ya kuuza, pili kuhusu maziwa yetu ambayo ndo mali ya wananchi wangu tungezalisha samaki kwa wingi na kuvuliwa kwa utaratibu ili kupata samaki wengi huku tukiwa na ulinzi madhubuti wa kuzuia wale maharamia wakuu wakuvua ovyo samaki angali wakiwa wachanga, pia ningefunguwa viwanda vingi vya kusindika samaki ili kupunguza uhaba wa ajira kwa vijana wetu.

7. ushauri kwa wanawake wenzangu amabo wamejibweteka nawashuri kuwa waache kusingizia kuwa hawana elimu hata biashara wanaweza kufanya kwani sasa hivi mikopo ni mingi wanakopesha, tuache kuwategemea wanaume tu hali ya maisha ni ngumu ukijiwezesha nawe utawezesha tuamke wanawake!

8.Ningekuwa waziri wa jinsia na watoto, kwanza ningeunda kamati ndogo ambayo ingekusanya watoto wote wanaofanya biashara na kufuatilia maisha yao je wanaishi na wazazi na kama kuna wale yatima ningeanzisha vituo vya kulelea watoto yatima huku wakipata elimu ya awali na kuendelea, na kundi lingine ambalo nitakuta kuwa wazazi wapo wameamua tu kuwaacha watoto wafanye biashara wazazi watachukuliwa hatua za kisheria, kuhusu wale wanaofanya kazi majumbani nadhani wizara yangu ingeliweka wazi hili kwa wale wote wanawaajiri watoto kuwe na sheria ya kumlinda huyu (housegirl) nadhani unyanyasaji ucingekuwepo kabisa.

9. kwanza nampa hongera sana kaka Dismas kwa kuanzisha hii blog,  ushauri wangu kuhusu blog yetu ni kwamba kiundwe kama kikundi ambacho hata tukikutana kwa mwaka mara mbili si mbaya natumai hapo baadaye tunaweza tukaunda chama chetu tukapata hata wabunge nasi tukaingia bungeni vile vile kutetea haki za wananchi

10. Ahsante kaka Bon kwa maswali yako nawe nakutakia afya njema

Ahsante Aggy kwa kujibu maswali nami nimejishukuru

Boniface Msami said:

Habari dada nyakunga, natumaini ni mzima wa afya teletele,

Maswali yangu kama ifuatavyo,

1)wewe ni mwenyeji wa wapi?

2)elimu yako ya awali na ulipifikia,

3)ni kitu gani ukipendacho zaidi kuliko ukikipata utafurahi,

4)na kitu gani ukichukiacho ukikiona utachukia mpaka basi,

5)je umeolewa? unafamilia yani watoto, na kama wapo ni wangapi?

6)je wewe ungekuwa kiongozi wa nchi hii yenye maziwa na asali lkn hali ni ngumu, je ungefanya nini ili hali hii ngumu iwe nyepesi?

7) je una ushauri gani kwa wanawake wanaopenda kukaana kubweteka na kuacha kujituma kisingizio wakidai ni elimu wakati wanao uwezo wa kujituma nakuondokana na mfumo dume?

8)je ungekuwa waziri wa jinsia na watoto, ungewasaidiaje watoto wanaofanya biashara, au kutumikishwa majumbani bila ya kusoma na kuwa na maisha mazuri kama waajiri wao?

9)na unaushauri gani kuusu hii brog yetu ili izidi kuwa juu zaidi, na kiongozi wake dismas aende samunge kwa babu samunge akapate kikombe cha babu,

10) na mwisho nakutakia maisha marefu na afya njema ili uweze kunijibu maswali yangu vizuri,,,,aksante boni kwa maswali yako... nimejishukuru mwenyewe,

Ahsante kaka Dixon

Dixon Kaishozi said:
Hongera dada Agnes Nyakunga..

Ahsant kaka Riziki, Kamwenee

Ahsante nasuburi maswali yako kaka!

riziki matitu said:

Kwanza kabisa napenda kukupa hongera kuteuliwa kuwa mdau wa wiki dada Agness .Kamweneeeeeeee.Maswali mengi wadau wameshakuuliza mimi nikutakie kila la kheri katika wakati wako huu wa kua mdau wa tulonge kama nitapata swali la kukuuliza nitakutwanga hapo baadae dada.Ninakutakia majukumu mema

RSS

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*