Tulonge

Huu ndiyo uwanja wa kumwaga lolote juu ya mdau wetu wa wiki kwa kuzingatia maadili mema.Kazi kwako mdau

Views: 791

Replies are closed for this discussion.

Replies to This Discussion

Habari dada Aggy, unapatikana wapi?
Mimi ni mjasiliamali. Swali. Je, naruhusiwa kukuonesha bidhaa yangu?
Mhhh... Onyesha tena biat V.A.T !!

Cha the Great said:
Mimi ni mjasiliamali. Swali. Je, naruhusiwa kukuonesha bidhaa yangu?

Asante sana kwa majibu yako, kumbe wewe ni mjomba wangu kabisa. Mimi napenda sana Iringa, nimekaa sana kijiji cha Migoli karibu na bwawa la Mtera kwa kazi mbalimbali, kila nijapo likizo lazima niende Iringa, Mafinga - makalala, huko kuna kituo cha watoto yatima ambapo mimi binafsi nakifuatilia kwa muda mrefu kwa ukaribu sana na kukipenda sana tena sana. kwakweli ni furaha sana moyoni mwangu kushirikiana kwa ukaribu na kituo hicho cha Makalala, sasa tuna watoto 38, ambao wanaendelea vizuri sana kwa kila huduma, karibu kila wiki napata taarifa kwa njia ya simu, pia mwanzilishi wa kituo hicho kwasasa yupo huku kwa likizo ya uzazi, tunaonana kila mara kubadilishana mawazo mbalimbali kuhusu Makalala Home Children. Karibu sana Makalala dada Agnes. Ujionee mwenyewe na utawapenda sana watoto, naamini.

Jinsi ulivyojibu maswali ya wadau wengi hapa, sina tena maswali zaidi ya kukuuliza...maana mengi walishanitangulia kukuuliza, ila nimependa majibu mengi ulivyojibu na kueleza vizuri, safi sana na hongera sana. Nakutakia kila laheri katika haya maisha. 

Agnes Nyakunga said:

nakujibu kaka Franco kama ifuatavyo:-

1) mimi ni mzaliwa wa Iringa, kabila langu mhehe

2) kitu nachokipenda sana katika maisha ni kubadilishana mawazo na watu mbalimbali wa rika lolote!

Ahsante kaka Franco nasubiri mawsali mengine kutoka kwako

BARAKA FRANCO CHIBIRITI said:

Haya sasa zamu yako dada; Na mimi nakutwanga maswali haya;

1). Wewe ni mzaliwa wa wapi? Kabila gani?

2). Kitu unacho kipenda sana katika haya maisha ni nini?

Ukinijibu haya nitakuuliza na mengine mengi tu mpaka uchoke.

Hongera dada Aggy kwa kuwa mdau wa wiki.

1. Unalichukuliaje suala la utoaji mimba?Nani wa kulaumiwa (mvulana au msichana)?

* Nina imani wewe ni mkristo wa kweli,endapo utadanganya kwenye jibu utakalo litoa ktk swali lifuatalo utakuwa unazidi kujiongezea mzigo wa dhambi zako.Ni bora usijibu kuliko kudanganya.

2. Umewahi kutoa mimba au hapana? Kama ulitoa, kwa nini uliamua kutoa?

....................................Agnes!!!! Mmmmmh.........................................

Rejea jibu lako la swali namba 5 uliloulizwa na Boniface Msafi "5. cjaolewa, ila na watoto mapacha".

1. Watoto ni wakike au wakiume? Wapo wapi kwa sasa?

2. Je unakaa na baba ya watoto au mlipata watoto then mkaachana?

3. Kama mmeachana,ni nini kilipelekea muachane?

4. Una mpango wa kuwa na watoto zaidi ukiwa nje ya ndoa? Au utasubiri hadi uolewe?

Rejea jibu lako la swali namba 3 uliloulizwa na mimi "3. kaka naye mpenda Mkuu (Tulonge) mwenyewe"

1. Ni sababu zipi zilizokufanya umchague Tulonge na siyo mwingine?

Jibu la swali la 9 limezingatiwa na linafanyiwa kazi. Hongera Agnes kwa kuendelea kupangua maswali kifasaha.

Agnes Nyakunga said:

niko salama

1. mimi mwenyeji wa Iringa

2. elimu yangu ni sekondari 'O' level na nimesoma chuo cha magogoni P/S (personal Secretary)

3. Kitu ni kipendacho kiko ndani ya moyo wangu natumai siku nikikipata nitafurahi sana

4. kitu nikichukiacho kuona wanawake wanaojiuza ovyo sasa hivi kila kona watoto wadogo sana wanajiuza nachukia sana

5. cjaolewa, ila na watoto mapacha

6. ningekuwa kiongozi wa nchi wa nchi hii yenye maziwa na asali nyingi, kwa mtizamo wangu kwanza ningewashauri wananchi wangu kuzalisha asali kwa wingi na kuwatafutia masoko mbalimbali ya kuuza, pili kuhusu maziwa yetu ambayo ndo mali ya wananchi wangu tungezalisha samaki kwa wingi na kuvuliwa kwa utaratibu ili kupata samaki wengi huku tukiwa na ulinzi madhubuti wa kuzuia wale maharamia wakuu wakuvua ovyo samaki angali wakiwa wachanga, pia ningefunguwa viwanda vingi vya kusindika samaki ili kupunguza uhaba wa ajira kwa vijana wetu.

7. ushauri kwa wanawake wenzangu amabo wamejibweteka nawashuri kuwa waache kusingizia kuwa hawana elimu hata biashara wanaweza kufanya kwani sasa hivi mikopo ni mingi wanakopesha, tuache kuwategemea wanaume tu hali ya maisha ni ngumu ukijiwezesha nawe utawezesha tuamke wanawake!

8.Ningekuwa waziri wa jinsia na watoto, kwanza ningeunda kamati ndogo ambayo ingekusanya watoto wote wanaofanya biashara na kufuatilia maisha yao je wanaishi na wazazi na kama kuna wale yatima ningeanzisha vituo vya kulelea watoto yatima huku wakipata elimu ya awali na kuendelea, na kundi lingine ambalo nitakuta kuwa wazazi wapo wameamua tu kuwaacha watoto wafanye biashara wazazi watachukuliwa hatua za kisheria, kuhusu wale wanaofanya kazi majumbani nadhani wizara yangu ingeliweka wazi hili kwa wale wote wanawaajiri watoto kuwe na sheria ya kumlinda huyu (housegirl) nadhani unyanyasaji ucingekuwepo kabisa.

9. kwanza nampa hongera sana kaka Dismas kwa kuanzisha hii blog,  ushauri wangu kuhusu blog yetu ni kwamba kiundwe kama kikundi ambacho hata tukikutana kwa mwaka mara mbili si mbaya natumai hapo baadaye tunaweza tukaunda chama chetu tukapata hata wabunge nasi tukaingia bungeni vile vile kutetea haki za wananchi

10. Ahsante kaka Bon kwa maswali yako nawe nakutakia afya njema

Ahsante Aggy kwa kujibu maswali nami nimejishukuru

Boniface Msami said:

Habari dada nyakunga, natumaini ni mzima wa afya teletele,

Maswali yangu kama ifuatavyo,

1)wewe ni mwenyeji wa wapi?

2)elimu yako ya awali na ulipifikia,

3)ni kitu gani ukipendacho zaidi kuliko ukikipata utafurahi,

4)na kitu gani ukichukiacho ukikiona utachukia mpaka basi,

5)je umeolewa? unafamilia yani watoto, na kama wapo ni wangapi?

6)je wewe ungekuwa kiongozi wa nchi hii yenye maziwa na asali lkn hali ni ngumu, je ungefanya nini ili hali hii ngumu iwe nyepesi?

7) je una ushauri gani kwa wanawake wanaopenda kukaana kubweteka na kuacha kujituma kisingizio wakidai ni elimu wakati wanao uwezo wa kujituma nakuondokana na mfumo dume?

8)je ungekuwa waziri wa jinsia na watoto, ungewasaidiaje watoto wanaofanya biashara, au kutumikishwa majumbani bila ya kusoma na kuwa na maisha mazuri kama waajiri wao?

9)na unaushauri gani kuusu hii brog yetu ili izidi kuwa juu zaidi, na kiongozi wake dismas aende samunge kwa babu samunge akapate kikombe cha babu,

10) na mwisho nakutakia maisha marefu na afya njema ili uweze kunijibu maswali yangu vizuri,,,,aksante boni kwa maswali yako... nimejishukuru mwenyewe,

napatikana Muhimbili ndo kazini kwangu

Dada said:
Habari dada Aggy, unapatikana wapi?

Ahsante kaka Tulonge!
Tulonge said:

10) na mwisho nakutakia maisha marefu na afya njema ili uweze kunijibu maswali yangu vizuri,,,,aksante boni kwa maswali yako... nimejishukuru mwenyewe,1. watoto ni wakike na wakiume

2. mmh

3. huko mbali sana

4. sina jibu kwa sasa, maana bado nipo nipo kwanza

narejea ulizo lako la mwisho

sababu zilizofanya nimchague Tulonge kuwa ndo kaka naye mpenda ni

Anamtizamo wa mbali sana ukiangalia yeye ndo alofanya tuweze kulonga hadi leo naweza kuchat na wewe pasipo kukufahamu sura wala nini hapo tayari ni nusu kufahamiana, anapaswa kuheshimiwa unategemea pasipo yeye Tulonge kaka Severin ungenipata wapi ili uweze kunibamiza haya maswali yako ambayo mengine nashindwa hata kukujibu maana jasho tu linanitoka!

Ahsante kaka Severin

Severin said:

Rejea jibu lako la swali namba 5 uliloulizwa na Boniface Msafi "5. cjaolewa, ila na watoto mapacha".

1. Watoto ni wakike au wakiume? Wapo wapi kwa sasa?

2. Je unakaa na baba ya watoto au mlipata watoto then mkaachana?

3. Kama mmeachana,ni nini kilipelekea muachane?

4. Una mpango wa kuwa na watoto zaidi ukiwa nje ya ndoa? Au utasubiri hadi uolewe?

Rejea jibu lako la swali namba 3 uliloulizwa na mimi "3. kaka naye mpenda Mkuu (Tulonge) mwenyewe"

1. Ni sababu zipi zilizokufanya umchague Tulonge na siyo mwingine?

Alfani mbona umeishia kuguna nini tena maswali wamekuwahia wenzio?

Alfan Mlali said:
....................................Agnes!!!! Mmmmmh.........................................

RSS

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*