Tulonge

Huu ni ukumbi wa kumtwanga Mdau wetu wa wiki maswali,maoni,ushauri,malalamiko,msaada nk .Kazi kwako mdau.

Views: 1307

Replies are closed for this discussion.

Replies to This Discussion

Kaazi kweli kweli...!

Ndugu yangu Ramadhan naomba nikujibu kama ifuatavyo:

1. Mimi nina elimu ya chuo Stashahada ya juu ya sayansi ya computa niliyoipata mwaka 2007 pale IFM.
2. Nimezaliwa mkoani singida mwaka 1979 mwezi wa kumi tarehe 22.


3. Kwa sasa naishi Dar es Salaam wilaya ya Ilala nje kidogo ya jiji wanapaita Gongo la Mboto.

4. Nimeoa

5. Nina watoto wawili Handsome Boys.

6. Changamoto za kifamilia zipo kwa mfano watoto wakiugua inabidi ufanye jitihada wapte matibabu,inabidi ukomae familia ipate chakula na mavazi na vile vile kuishi na mke pia yahitaji ukomavu wa kifikira na maamuzi kiasi fulani uhuru unapotea...siku zote familia inakuwa mbele!!

7. Kuhusu Ukimwi nimepima mara nyingi kidogo na majibu yalikuwa mazuri kipindi hicho kwa sasa nina muda mrefu kidogo toka nimepima ila nina mpango wa kwenda kuchecki tena.

8. Kuhusu uchumi mimi niko katika kundi la watu wa wastani sio tajiri wala sio fukara,nadhani neno "masikini" linaweza kuingia kidoogo kwani kuna vitu ambavyo vikitokea ghafla siwezi kuhimili mpaka nipate msaada wa kifedha kwa wenye nazo.

10. Maisha ya mtanzania yamegawanyika katika makundi tofauti tofauti..Matajiri wapo,wanaojiweza wastani wapo,wanaojiweza kidooogo wapo,wasiojiweza kiasi wapo,masikini wapo na mafukara wapo pia. Ila kundi linalofaidi matunda ya nchi yetu ni MAFISADI wachache wanaojilimbikia mali na kusahau watanzania wenzao walio wengi wanateseka kwa maisha magumu!!

nadhani nimekujibu kama ulivyouliza mkuu wangu.

Ramadhan Ahmard said:

Habari kaka.

Napenda kujua kuhusu elimu yk, ulizaliwa wp, unaishi wp, umeoa na km umeoa una watoto wangapi na unapt changamt gani za kifamilia, kama bd unangoja nn au una "king'amuzi (mpenzi) na unajizuiaje na vishawishi, na kuhusu ukimwi  je, umepima?  c mby km tutapt majibu yk, vp kuhusu uchumi juu yk, je wewe ni tajiri, una nafuu ya maisha au fukara? Na unjua nn kuhusu maisha Mtanzania???

Naomba unijb kama nilivyokuuliza.

Ahsante!

unaionaje serikali ya sasa na kuhusu familia unatekelewaje majukumu yako bila kuitenga familia

NAOMBA UWE MKWELI JUU YA MAJIBU YA MASWALI HAYA.NINA AMINI WEWE NI MUISLAM WA KWELI.

1. Umewahi kukorofishana na mkeo kwa kukuhisi umetoka nje ya ndoa?

2. Ni kweli umewahi kutoka nje ya ndoa?

3. Roho huwa inauma (unajutia) endapo umetoka nje ya ndoa? Au huwa hujali kitu? kwa nn?

je kaka Alfan ukiangalia sasa hivi tuko katika janga hili kubwa la ukimwi wewe kama wewe huo unatoa elimu gani kwa vijana kuhusu gonjwa hili hatari?

Kwa kweli sina imani na serikali ya Chaka Chua Matokeo kwani imeingia madarakani kwa kuchakachua matokeo na wala haisikilizi shida za wananchi wake..kila kiti kimekuwa ni kero tupu si umeme,maji usafiri,matibabu.


Kuhusu majukumu na familia......Majukumu ni magumu sana muda mwingine nachelewa sana kurudi hm na hivyo kufanya muda wa kukaa na familia kuwa mdogo.Nafurahi kwamba mke wangu ni muelewa na hana tatizo kkuhusu mimi kutekeleza majukumu yangu kwani ndio yanatuweka mjini.Siku za weekend hasa Jumapili huwa siendi popote ili nipate nafasi ya kukaa na familia yangu!
saleh mkali baya said:

unaionaje serikali ya sasa na kuhusu familia unatekelewaje majukumu yako bila kuitenga familia

Hahahahahahahahahahaha! Unatafuta nini wewe Severin???


Ok,
1. Yap ni kweli nimewahi kukorofishana na wife mara kadhaa kwa kunihisi vibaya ila tunamanage kueleweshana na ugomvi unakwisha.

2. Duh, hili swali gumu halijibiki.

3. Mmmmh, sijui kwa kweli nadahani siku niifanya hivyo ntajua kama inaumma au la..lol

Severin said:

NAOMBA UWE MKWELI JUU YA MAJIBU YA MASWALI HAYA.NINA AMINI WEWE NI MUISLAM WA KWELI.

1. Umewahi kukorofishana na mkeo kwa kukuhisi umetoka nje ya ndoa?

2. Ni kweli umewahi kutoka nje ya ndoa?

3. Roho huwa inauma (unajutia) endapo umetoka nje ya ndoa? Au huwa hujali kitu? kwa nn?

Swali zuri sana Agness aka ........ Dismas anajua..lol

Ni kweli kuna janga kubwa la ukimwi ambalo linatishia maisha ya watu wengi sana.Wengi wetu tunajua uwepo wa gonjwa hili na kuchukua hatua za kupambana nalo ila wengi pia wanajua uwepo wake lkn wanaziba masikio na macho na kuamua kujitoa muhanga!!

Ushauri wangu ni huu hapa:

Ni jukumu la kila mmoja wetu kujua afya yake kwa kwenda kupima na kuchukua majibu (wengine huwa wanapima halafu majibu wanakimbia kama Dismas)..Kwa kufanya hivyo tutaweza kuchukua hatua sahihi baada ya majibu.

1. Kama umeathirika utajua ni jinsi gani ya kusihi ili usiambukize wengine na kuchukua hatua zitakazokufanya uishi muda mrefu zaidi.

2 Kama hujaathirika utajua uchukue hatua gani ili kujikinga usipate.Agnes Nyakunga said:

je kaka Alfan ukiangalia sasa hivi tuko katika janga hili kubwa la ukimwi wewe kama wewe huo unatoa elimu gani kwa vijana kuhusu gonjwa hili hatari?
halafu nyie wadau kumbe wa ajabu kweli kwel hiyo ni picha tu sio Diana mwenyewe lol
Alfan ww wangu me wala sikuulizi mkuu sitaki kukuumbua
hahahahahaha safi sana nitafute nikupigishe ulabu!!!

KUNAMBI Jr said:
Alfan ww wangu me wala sikuulizi mkuu sitaki kukuumbua

 Kaka Alfan kwenye historia yako umesema mpaka sasa una watoto wawili, je unampango wa kuongeza wengine? kama ni ndio,  wangapi?

Alfani sorry sikuwa na net nadhani uliniloga nisiulize miswali haya ni hivi

Una miaka mingapi?

umepanga kuwa na watoto wangapi?

Mengine yanakuja haya ni Private zaidi hahhah haha

RSS

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*