Tulonge

Huu ndiyo uwanja wa kumtwanga maswali,kumpa ushauri,kutoa lalamiko lako,kuomba msaada nk kwa mdau wetu wa wiki kwa kuzingatia maadili MEMA. Kazi kwako

Views: 592

Replies are closed for this discussion.

Replies to This Discussion

Hongera kwa kuwa mdau wa wiki kaka. Wewe ni kabila gani?
Hongera mkaka umeoa?
Mambo kaka Baraka hebu niambie ni kitu gani ambacho unachukizwa maishani huwa hukipendi
Karibu karibu kibarazani... Pumua kwanza.. nakuja mda si mrefu..

Asante sana Lilian, mimi ni mtoto wa Makao Makuu ya chama na serikali aka Mgogo.

We Mtemi wewe.....umeanza uchokozi wako. Bado nipo nipo kwanza ( Bado sijaoa). Lakini nafikiria sana na nina hamu sana tena sana, umerithika sasa Mtemi aka Saya. Jibu lako ndo hilo...uliza jingine.

 Jibu kwa Dada mpendwa Agnes; Poa kabisa! kinachonikera sana katika maisha yangu ni; watu kudharau UTU WA MTU ( HESHIMA YA MTU NI UTU WAKE...SI CHEO WALA MALI). Huwa nachukia sana tena sana, maana watu wote tena woteeeee duniani....wadogo kwa wakubwa, matajiri kwa maskini wote tunathamani sana katika hii dunia, hakuna mtu aliyezaliwa bila thamani yake..la sivyo asingezaliwa. Mtu akinidharau katika maisha yangu au ya mtu mwingine karibu yangu huwa nachukia sana, yaani sipendi sana hilo huwa linaniudhi zaidi na zaidi, na mengineyo mengi tu...lakini hili ndio kubwa zaidi kwangu. Mimi napenda sana watu wote, makabila yote na dini zote, na kuheshimu sana kila mmoja. Lakini mtu akinidharau huwa namsamehe...lakini naachana nae kabisa, tena nakaa naye mbali kabisa!

Asante asante Mkuu Dixon..... we njoo tuu mi nipo tayari kwa kila swali lako, utajibiwa tu!

Duh! kumbe wewe ni mjomba wangu kabisa. Niambie wewe niwa Dodoma kijiji gani? Mvumi,Mpunguzi,Matumbulu,Veyula,Nala au wap?
Hongera Mzee Chibiriti kwa kupata fursa hii ya kuwa mdau wa wiki. Mimi nataka kujua mtazamo wako kuhusu Katiba mpya na kama itakuwa na manufaa yoyote kwa taifa.

Mkuu Tulonge....kumbe wewe ni Kamwene au? Mjomba kabisa! Mimi ni wa Miyuji nje kidogo sana ya Mji wa Idodomia kama unaelekea Vyeyula to Kondoa, karibu sana na Sekondari ya Msalato, hata kwa miguu unaenda kabisa mjini kati Dodoma. Ila orijino yangu kabisa ni Singida Wilaya ya Manyoni....tabaka languni gumu sana kulitambua, maana halitambuliki sana...maana linachanganyikana na makabila kibao ya Singida na Dodoma ( WANYAMBWA) naamini hujawahi kusikia kabisa kuhusu kabila hili. Lakini maneno mengi sana ni ya Kigogo kabisa, hivyo sisi ni wagogo tuliopo mkoani Singida. Lakini wenyewe halisi huwa hawatutambui kuwa na sisi ni wagogo. Kazi kweli kweli!!!!

Asante Mkuu Jorge. Jibu lako Mkuu Jorge: Kwakweli sijafuatilia sana kuhusu katiba mpya, kwahilo utanisamehe. Maana kuishi nje ya nchi si unajua tena pilikapilika za hapa na pale, wakati mwingine tunashindwa kufuatilia mambo yote ya nyumbani. Kama una nafasi nitaomba unidokezee walau kidogo, la sivyo nikija mwezi wa sita nitafuatilia zaidi. Nilisikia sana kuhusu swala hilo...lakini kusema ukweli sijafuatilia sana.

 

RSS

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*