Tulonge

Huu ndiyo uwanja wa kumtwanga maswali,kumpa ushauri,kutoa lalamiko lako,kuomba msaada nk kwa mdau wetu wa wiki kwa kuzingatia maadili MEMA. Kazi kwako

Views: 586

Replies are closed for this discussion.

Replies to This Discussion

Kwanza kabisa, Hongera kwa kuwa mdau wa wiki!!

 

Mimi nina maswali machache sana.

1. Una undugu na Mama malaika?

2. Sijawahi kuona picha ya shemeji yetu,vipi bado uko bachelar?

3. Elimu ya kuchimba visima uliipatia wapi?

4. Kipi kilikufanya ukachagua kuishi Ujerumani na sio nchi nyingine yoyote?

5. Ukipewa jukumu la kuteua mwakilishi wa kijiji hiki atuwakilishi bungeni ungemteua nani na kwa sababu zipi??

 

Ni hayo tu mkuu kwa leo.

Poa kaka, nitajitahidi kutafuta wakati nikuelezee. Ila kwa kifupi tu, Tanzania iko katika mchakato wa kuunda katiba mpya ya nchi. Maoni ya wananchi yanakusanywa ili kujua ni katiba ya namna gani wanaitaka (ila muda wa kukusanya maoni rasmi bado).
habari kaka chibiriti, mungu akipenda, kesho nitakuswalika,

Chibiriti   big up.......mimi swali langu dogo tuu broooo........Unaishi wapi kwa sasa na unafanya nini huko?

 

Unafanya kazi gani mkubwa,maana naona speed yako ya kukwea pipa si ndogo.
Kaka yangu mwanamke mwenye sifa zipi kiumbo? Au kama huyu http://tulonge.ning.com/photo/kaka-zangu-endeleeni-kuumia?context=user

Mkuu Maza yangu ni mgogo. Wanyambwa nimewahi wasikia mkuu,nasikia huwa mnakula sana panya..... haahhhaaaa ni kweli? Au huwa ni uzushi wa watu?


BARAKA FRANCO CHIBIRITI said:

Mkuu Tulonge....kumbe wewe ni Kamwene au? Mjomba kabisa! Mimi ni wa Miyuji nje kidogo sana ya Mji wa Idodomia kama unaelekea Vyeyula to Kondoa, karibu sana na Sekondari ya Msalato, hata kwa miguu unaenda kabisa mjini kati Dodoma. Ila orijino yangu kabisa ni Singida Wilaya ya Manyoni....tabaka languni gumu sana kulitambua, maana halitambuliki sana...maana linachanganyikana na makabila kibao ya Singida na Dodoma ( WANYAMBWA) naamini hujawahi kusikia kabisa kuhusu kabila hili. Lakini maneno mengi sana ni ya Kigogo kabisa, hivyo sisi ni wagogo tuliopo mkoani Singida. Lakini wenyewe halisi huwa hawatutambui kuwa na sisi ni wagogo. Kazi kweli kweli!!!!

Ndugu yangu CHIBIRITI.. heheheee, nimekupata ulipo sema wewe ni miongoni mwa kabila la WANYAMBWA!!! (wagogo wa singida).. Mimi nimeishi Dodoma na ninawapata vizuri wagogo kwa ujumla. Nauliza hivi..

Wagogo wanautamaduni wa kuwakeketa watoto wa kike. Je WANYAMBWA mna mila hiyo? kama mnayo wewe unatoa mchango gani kuteketeza mila hoyo ?..

 

Ni hilo tu ndugu yangu!

Mkuu Dixon: Swala la ukeketaji kwa watoto wa kike hata kwetu lilikuwepo tena kwa sana tu...na bado kwa chini chini lipo tu! Kama nilivyokuambia karibu sawa kabisa mila na desturi na wagogo, yaani kwa msemo wa haraka sisi ni wagogo tu.

Mimi nalipinga sana swala hilo, na sipendi hata kulisikia...lakini ndo hivyo tena lipo. Ila kwakweli niseme ule ukweli kwetu kijijini kwangu, sasa limekomeshwa sana, yaani hamna kwa sasa labda mtu afanye kwa siri sana, sio kama zamani ilikuwa hadharani tu, labda vijijini kule ambako bado hamna hata barabara ili uweze kufika, huko ndiko nasikia sikia tu kwa mbali, bado wanaendeleza mila hizo.

Mkuu Tuonge acha zako hizo wewe, unanichekesha sana...ha ha ha haaaa....!!!!! Inawezekana, ila mimi sijawahi kuona hivyo na wala sijawahi kula banya, labda nimekula bila kujua. Pia mimi maisha yangu zaidi nimekulia Tegeta - Dar, kwahiyo sina uhakika 100 kwa 100.  Wahehe je ni kweli wanakula mbwa?

Mimi sioni ajabu kabisa.....kama unakula kitu kwa kupenda roho hakikudhuru kitu, acha wengine waseme tu...kwani shida ipo wapi? Mbona hapa nilipo Ulaya tunakula kila aina ya takataka kama vile vyula, konokono, mijusi nk....

Lilian jibu lako ni; huyo sio wangu mimi kabisa. mimi napenda umbile la kwaida tu!

Lilian said:
Kaka yangu mwanamke mwenye sifa zipi kiumbo? Au kama huyu http://tulonge.ning.com/photo/kaka-zangu-endeleeni-kuumia?context=user
Mkuu Severin: Mimi ni mfanyakazi wa kawaida tu, mlalahoi kabisa! kukwea pipa isikutishe sana.....nipo katika kitengo cha uchapaji magazeti ( Printing Press) kitengo kidogo sana cha mji wa hapa Cesena. 

Severin said:
Unafanya kazi gani mkubwa,maana naona speed yako ya kukwea pipa si ndogo.

RSS

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*