Tulonge

Huu ndiyo uwanja wa kumtwanga maswali,kumpa ushauri,kutoa lalamiko lako,kuomba msaada nk kwa mdau wetu wa wiki kwa kuzingatia maadili MEMA. Kazi kwako

Views: 586

Replies are closed for this discussion.

Replies to This Discussion

Mkuu Gratious: Mimi naishi Cesena nchini Italy. Nafanya kazi za harakati za hapa na pale kutafuta mkate wa kila siku.

Gratious Kimberly said:

Chibiriti   big up.......mimi swali langu dogo tuu broooo........Unaishi wapi kwa sasa na unafanya nini huko?

 

Karibu sana Mkuu Boniface Msami, mi nipo tuu...!!!!

Boniface Msami said:
habari kaka chibiriti, mungu akipenda, kesho nitakuswalika,

Asante sana Mkuu Alfan.

1). Swali la kwanza...jibu lake ni; Mama Malaika ni ndugu yangu kama ulivyo wewe na wote wote kabisa katika kijiji hiki na kile cha Fotobaraza, kwakweli wote ni ndugu zangu...mimi binafsi najisikia hivyo. Hata kama sio wa kuzaliwa au wa ukoo mmoja.....naamini utaelewa kabisa  kwa jibu hili.

 

2). Swali la pili....jibu lake ni; Bado nipo nipo kwanza, kama ulivyosema (Bachelar). Bado sijampata wangu wa moyo, hivyo naomba sala zako kwa sana Mkuu Alfan, si unajua tena Dunia ya sasa jinsi ilivyo?

 

3). Swali la tatu.....jibu lake ni; Kashule kidogo, halafu juu kwa juu nilijifunza zaidi wakati wa kufanya kazi hiyo, nikiwa na mzoefu wa kazi hizo, ndugu Peter kutoka nchini Austria....huyu ndiye alikuwa mwalimu wangu mkubwa wa kila kitu kuhusu maswala ya kazi na maisha pia, nilijifunza kazi nyingi sana mpaka kuendesha malori makubwa kupitia kwa jamaa huyu.

 

4). Swali la nne....jibu lake ni; Kwanza kabisa mimi naishi nchini Italy, siishi Ujerumani. Pili kuishi kwangu Italy ni katika kupata elimu kidogo ya maisha na maswala ya kazi, katika kutafuta maisha...si unajua tena maisha ya kwetu jinsi yalivyo?

 

5). Swali la tano....jibu lake ni; Mimi binafsi ningemteuwa aliyeanzisha Kijiji hiki, kwasababu ana mawazo ya kuona mbali sana, kuanzisha kitu kama hiki ambacho kinatuunganisha sana, tunafaamiana mno, tunajifunza mengi sana kupitia hapa Kijijini. Wengine tumekuwa kama ndugu kabisa. Kula zangu zitamwangukia Mkuu Tulonge.Alfan Mlali said:

Kwanza kabisa, Hongera kwa kuwa mdau wa wiki!!

 

Mimi nina maswali machache sana.

1. Una undugu na Mama malaika?

2. Sijawahi kuona picha ya shemeji yetu,vipi bado uko bachelar?

3. Elimu ya kuchimba visima uliipatia wapi?

4. Kipi kilikufanya ukachagua kuishi Ujerumani na sio nchi nyingine yoyote?

5. Ukipewa jukumu la kuteua mwakilishi wa kijiji hiki atuwakilishi bungeni ungemteua nani na kwa sababu zipi??

 

Ni hayo tu mkuu kwa leo.

Nakushukuru sana mkuu Chibiriti kwa kujibu maswali kwa ufasaha,pia shukurani kwa wadau wote mlio shiriki kuuliza maswali kwa kuzangatia maadili mema. Nadhani kwa sasa tumemfahamu vizuri zaidi ndugu yetu Chibiriti.Kaa tayari kumpokea mdau wa wiki ajaye tarehe 1/05/2011

RSS

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*