Tulonge

Huu ni uwanja wa kutoa maoni yako juu ya mdau wetu wa wiki.Kazi kwako.

Views: 912

Replies are closed for this discussion.

Replies to This Discussion

1. Ndiyo nimeoa

2.Nina watoto wa ndani ya ndoa "0" na wa nje ya ndoa "0"

3.Tendo la ndoa kabla ya ndoa ni makubaliano ya wawili wapendanao kufanya au kutofanya, lakini si vibaya kumjua mwenzi wako nje ndani kabla ya ndoa  ili utakaposema ndiyo usije juta baadae ohhhh ningejua!!!!!!!!. nisingesema ndiyo

4. Watoto ni zawadi toka kwa Mungu hivyo sina fixed number niitakayo maana naweza sema nataka mtoto mmoja wakaja watatu kwa mpigo je hao wawili niwatupe???. 

Severin said:

1. Umeoa au unaishi na msichana bila kumuoa? Maana huwa naona picha zako tu,za mwenzi wako sizioni.

2. Una watoto wangapi? Wa nje au ndani ya ndoa?

3. Unalizungumziaje suala la kufanya tendo la ndoa kabla ya ndoa?

4. Unampango wa kupata watoto wangapi?

 

Asante Omary kwa hongera zako.

1.Ngoja niwe mkweli kwa hili lakubeba box mtoni na TZ. sina uzoefu wa kutosha kwa kufanya kazi Tanzania maana nilifanya kazi TZ miaka 2 tu na hapa mamtoni nina miaka 10, katika kubeba Box inategemeana na aina gani ya box unalobeba eithet TZ au hapa Ughaibuni. Maisha ya kubeba Box hapa ughaibuni ni sawa na Robot, maana kila kitu kiko programmed na unapata mshahara kutokana na jasho lako kweli maana  siyo tu kama TZ watu wana sign muda wa kuingia kisha wanaenda katika misele yao na mwisho wa mwezi mshahara unaingia kama kawaida.

Hapa unalipwa kutokana na masaa unayokuwepo kazini hivyo ni lazima usign wakati unaingia na wakati unatoka na siyo unasign kwa kalamu katika daftari bali una chipcard ambayo inakuwa scaned na computer. Kwa kifupi naweza kusema maisha ya kubeba Box hapa mtoni ni magumu kwa wale wote wenye kasumba ya kutegea kazi lakini malipo yake ni mazuri ukilinganisha na malipo wapatayo wafanyakazi wengi wa kawaida hapo TZ:

2. Ugumu wa maisha ya huku unamfundisha mtu adabu ya maisha na jinsi ya kupanga budget ya maisha kama usemavyo ni kweli hakuna kumpiga mtu kirungu ukapata buku sana sana labda upate credit toka benki. Kuhusu kupata maisha bora hapa mamtoni narudia tena hii itategemea na aina gani ya Box(kazi) ubebalo, kuna kazi ambazo kwa kweli hata ukikaa miaka 50 hapa kamwe huwezi kupata maisha bora ila kuna kazi ambazo ukibahatika kuzipata hasa kama una elimu nzuri basi haikuchukui muda mrefu kuishi dream life.

3. Swali lako la mwisho ni gumu kwani linatokana na system nzima ya utawala wa TZ kuanzia katika elimu hadi katika soko la kazi nadhani kama system ingekuwa nzuri hakuna mtu ambae angekuwa na ndoto za kukimbilia mamtoni.

Omary said:

Hongera sana mkuu Don.

je unaonaje misha ya kubeba box ukiwa mamtoni na ukiwa tz?

na ukiangalia ugumu wa maisha umekuwa ukibana kotekote naweza kusema huko mamtoni ndio zaid kulingana na maisha yalivyo na bei za v2 watu wake cc huku ukikosa unaweza kumpiga kirungu Mr Tulonge akakupa buku maisha yakasonga but huko huwezi tembeza virungu je nafikiri unaweza kupata maisha bora kwa kubeba box?

unafikiri kwa hapa tz bila kukimbilia mamtoni vijana tufanyeje? ili tuwe na maisha mazuri? maana ajira za tz kama unavyozijuwa mshahara haufiki tarehe 7 umeisha kisha unaanza tena kukopa na tunatamani maisha bora tutayatowa wapi?


Asante eddie
eddie said:
Hongera Mkuu kwa kuchaguliwa kuwa mdau wa week. Mimi sina maswali zaidi ya kukutakia kila la heri katika shughuli zako ughaibuni!
Asante Bro kwa majibu yako mazuri God bless you cc 2po TZ tunakomaa.
Hongera sana Don M kwa kujitahidi kujibu vizuri maswali toka kwa wadau. Nahisi uliwahonga wadau ili wasikuulize maswali mengi,naona hujakadhamizwa maswali sana kama wadau wa wiki wengine waliopita.  Tunashukuru kwa majibu yako ambayo yametufanya tuweze kukufahamu zaidi ya mwanzo. Kaeni tayari kwa mdau wa wiki mwanzoni mwa mwezi ujao (Julai).

RSS

© 2023   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*