Tags:
Replies are closed for this discussion.
kwanza salaa alykm, then get prepared.......
Hongera kwa kuwa mdau wa wiki.
asalam alaikum kaka zangu na dada zangu na wadogo zangu kwanza napenda kutowa shukrani zangu za dhati kutoka ndani ya moyo wangu kwa kunipa heshma kubwa sana kwa kunichaguwa kuwa mdau wa wiki nami sina budi kuwaombea wadau wote mola awape kila la kheri baraka amani upendo ushirikiano na furaha tele moyoni mwenu. napenda kutowa shukrani zangu kwa kaka omary kwa mapokezi aliyonipa nilipofika dar kwa kweli amenipa mapokezi ya heshma kubwa sana amenipokea kama mzee wake na wadau niliokutana nao kama kaka michuzi dada angela dada jacqueline na dada latifa kwa kweli dada latifa ndiye mtu wa kwanza kunipokea nikishuka bus dar na kunipeleka hotelini kulala mola awabariki nyote nikimalizia nasema tuwe na moyo wa udugu kwa kupendana na kushirikiana na hapo mola atatupa baraka zake "AMEEN"

Maalim Hassan me naomba kufaham yafuatayo
1. majina yako kamili
2.ww ni mzaliwa wa wapi na mwenyeji wa mkoa gani?
3.kwa sasa unaishi wapi?
4.una miaka mingapi na je umeoa na una watoto wangapi?
5.ukipewa fursa ya kutoa ushauri kwa wanakijiji cha tulonge utatoa maoni gani yatakayowafaa kwenye maisha yao,na mazingira wanayoishi kwa ujumla?
5.ni kitu gani hasa kilichokupendeza humu Tulonge mpka ukaamua kujiunga kwenye social network hii?
6.katika kuboresha kijiji cha tulonge ungependa kumshauri nn Mr Tulonge ili afanye katika kuboresha hiki kijiji?
7.ni kitu gani ukikiona humu tulonge kinakukera sana,na ungependa kusema nn juu ya hicho kitu?
KWA LEO NI HAYO TU.........................................
Wadhaa salaam.......................
Hongera sana Bro kwa kuwa mdau wetu wa week.
Brather me nimebahatika kukutana na ww pale mombasa kiukweli umenifanya nijivunie kuijuwa mombasa
vizuri kwa kutembelea sehem mbalimbali za mombasa kuliko hata mwenyeji wa mombasa nimejifunza k2 kutoka kwako ww ni m2 wa watu pia una moyo wa kusaidia hupendi kuona m2 anakwama pale ambapo ww unauwezo napo huwa nimwepesi sana kusaidia hongara sana kwa hilo Mungu atakulipa inshaallah.
1 ww unaumli mkubwa kuliko cc wadogozako unatushauli nn? cc vijana wa sasa
2 watoto wa mitaani ni tatizo kubwa sana la hapa nchini kwe2 tz hata na kenya je ww unatoa mchango gani? kwao ama inakugusaje?
3 unafikiri tufanyeje? ili kufanya vijiji vyetu kama tulonge, fotobaraza visiishie hapa vipige ha2wa.
kwa leo naishia hapo nitaludi tena.
mimi kwa jina kamili naitwa HASSAN SALEH AHMED DAMNAN ni mtoto wa pili kwa tumbo letu na ni mtoto wa kiume wa peke nina dada watano. nilizaliwa mwaka wa 01/05/1960 katika kijiji cha kidunguni likoni wilaya ya mombasa. nilisomea shule ya BOMU PRIMARY SCHOOL mombasa mpaka darasa la saba na sikuweza kuendelea na masomo yangu ilikuwa mwaka wa 1972 hapo ndipo baba yangu mzazi aliaga dunia nikanza mihagaiko kwa sababu baba yangu hakuwa na kitu chochote cha kuweza kurithi nilianza kufanya vibaruwa nikiwa na miaka 13 mpaka mwaka wa 1977 nilienda uganda kufanya kazi mpaka mwaka wa 1979 alipopinduliwa idd amin dada nilirudi kenya nikaenda saudia mwaka wa 1980 kufanya kazi nilinyanyaswa na tajiri na nikagoma kufanya kazi na wenzangu tulifungwa mwezi moja na kuregeshwa kenya sikufa moyo nilirudi tena saudi mwaka wa 1983 nikafanya kazi miaka mitatu nikaona mshahara ni mdogo nikarudi kenya nakufanya kazi mbali mbali mpaka mwaka wa 1993 nilipata kazi na AMERICAN AIR FORCE mombasa base nikafanya kwa mwaka moja base ilifungwa na mola akanijalia kupata kazi kwa chuo kikuu cha nairobi/chuo kikuu cha washington nikiwa driver/logistic officer na ninafanya mpaka sasa niliowa mwaka wa 1985 nimejaliwa wasichana wanne wawili wameolewa na wawili bado wanasoma nimejaliwa na wajuku wanne, ninafanya kazi za kujitolea bila malipo kwa shirika la ST JOHN AMBULANCE kama naibu wa mwenyekiti katika mkowa wa pwani na KENYA SCUOTS kama mweka hazina wa mombasa na mweka hazina wa INTERNATIONAL CAMP SITE MIRITINI huo ndiyo wasifu wangu na maisha yangu mola awabariki nyote
Dixon Kaishozi said:
Hongera kaka.. Swali langu ni moja lakini lina upana mkubwa.. TUELEZE WASIFU WAKO!! Asante.
asante mama malaika i miss you my dear sister
Mama Malaika said:
Hongera sana kaka Damnan.
© 2023 Created by Tulonge.
Powered by