Tags:
Replies are closed for this discussion.
Nimerudi na nina shukuru kwa uvumilivu wenu. Nitajibu maswali yenu niwezavyo ila wengine mmenitundika ya siasa wakati siijui uzuri. LOL...
1. Nitajie mlikutana wapi na Baba Malaika kwa mara ya kwanza. Je alipoanza kukusumbua alituma mtu au alikuja mwenyewe?
Nilikutana na baba Malaika England, na alipoanza kunisumbua alijikaza kiume na alisema mwenyewe.
2.Ndugu zako (hasa wazazi) walikuchukuliaje kuwa na mahusiano na mzungu? Walikubaliana moja kwa moja bila kikwazo?
Wazazi wangu hawakujali sana sababu wamesafiri na pia wanajua mapenzi yanatoka moyoni mwa mtu na hayahusiani na rangi ya ngozi. Kwetu ni kama mini united nations hasa upande wa mama yangu nina ndugu wa mataifa mengi.
3.Hakuna ubaguzi wowote huko UK hasa katika Mazingira ya kazi na mtaani? mfano ubaguzi wa rangi.
Ubaguzi upo popote pale hata Tanzania. Ubaguzi unaotusumbua hapa ni wa rangi ukizingatia England ni nchi ya wazungu. Na sio weusi peke yetu tunaobaguliwa kwani hata wahindi na wachina wanabaguliwa pia, uzuri kumekuwepo na sheria inayotetea haki za ethnic minority na serikali inatilia sana mkazo sheria hiyo.
Upande wa kazi kuna ubaguzi ila ndio hivyo silaha yetu kubwa ni ELIMU. Elimu ndio ngao yetu kubwa na kujiamini hivyo unapobaguliwa kwa rangi ya ngozi yako lakini unapokuwa na elimu nzuri ya kutosha na kujiamini waweza pata kazi kutokana na kiwango cha elimu yako. Wengi weusi wanakata tamaa anapoomba kazi ananyimwa na kuamua kufanya kazi za chini. Kupitia elimu watu weusi nchini Uingereza wameweza kuwa doctors kwenye leadin hospitals and research centres, wengine wametuliwa kuwa majaji wa mahakama wakiwemo wanawake (na mwana mama Linda Dobbs aliteuliwa mwaka 2004 kuwa judge wa kwanza mweusi kwenye mahakama kuu ya England & Wales). Kuna weusi wakufunzi wa vyuo vikuu, wabunge, waziri mweusi tena mwanamama ambaye pia ni member of House of Lords (Baroness Patricia Scotland), etc.
Asante sana Dixon. Mkwe wangu hajambo?
Nakujibu maswali kama ifuatavyo
(1). Ulikutana vipi na Baba malaika ?
Nilikutana na baba Malaika nikiwa masomoni abroad. Sijui nimekujibu sawa?
(2). Familia yako (wazazi na ndugu zako wengine ) walichukuliaje utambulisho wa baba malaika?
Nilipokuwa masomoni walipata habari za uchumba hivyo walikuwa na shauku ya kumuona na kumjua mkwe mtarajiwa. Baba Malaika alipokwenda Tanzania kujitambulisha na kuomba ruhusa ya kuoa binti yao (mie) walikuwa tayari walishamsikia sifa na tabia yake hivyo ndugu, jamaa na marafiki walimpokea kwa mikono miwili na kumpa baraka zote. Na kwa Baba Malaika hiyo ndio ilikuwa mara yake ya kwanza kwenda Africa.
(3) Kwenu wewe ni mtoto wa ngapi na familia yenu kwa ujumla mpo wa ngapi ?Mie ni mtoto wa kwanza, familia yetu imebakia na watoto wanne baada ya mmoja wa kiume ambaye alikuwa ananifatia kuuawa na majambazi Dec. 1999.
(4). Kuishi kwako NJE.. unatoa mchango gani kwa wale ulio waacha nchini kwako
Mchango wangu mkubwa kwa wale wote niliowaacha nchini ni kuwa nao karibu wakati wa raha na shida iwe kimawazo na kifedha.
(5). Tunatambua umuhimu wako ndani ya kijiji hiki kwa ushauri, ucheshi na mchango wako kwenye hii jumuia.. Unasemaje kwenye suala la katiba ya nchi yetu.. una maoni gani juu ya hii katiba ya sasa na katiba ijayo ?
Katiba ya nchi ya Tanzania imetungwa zamani, inapaswa ibadirishwe kuendana na wakati na pia kwa manufaa ya nchi na wananchi wote wa Tanzania.
Mimi nina swali,,,
Mchakato gani ulio wahi kupambana nao na uto usahau maishani mwako?
Ni hilo tuu dada ake
Kwa heshima na tahadima napenda kukupngeza kwa siku ya ko ya kuzaliwa
Asante sana kaka Eddie kwa birthday wishes!
Nitajitahidi kujibu masuala yako hapa chini
1) Hobbies zangu kubwa ni kupika, kusoma vitabu (lakini sio novels), hiking, travel, movies, kutizama Discovery Channel & National Geographic, music, hiking, travel, kutumia muda wangu wa ziada kufundisha historia yetu (BLACK HISTORY) mashuleni, etc.
2) Vyakula, matunda na vinywaji nipendavyo
Ugali wa mhogo kwa samaki, dagaa wa bichi na wakavu, makande ya maharage na nazi, mboga za majani (matembele, msusa, kisamvu), mananasi, maparachichi, etc. Upande wa vinywaji ni soft drinks.
3) Mji niupendao ni PRETORIA, nchi niipendayo ni SCOTLAND.
4) Actor nayempenda ni Adam Sandler (he is very funny) and Actress is Salma Hayek.
5) Filamu (movie) niipendayo kuangalia tena na tena ziko tatu; Dirty Dancing (RIP Patrick Swayze), The Notebook na Legends of the Fall.
6) Na tabia moja ambayo huwaudhi ndugu na marafiki nayo ni kutaka kitu kifanyike kwa ratiba/muda tuliopangwa. Iwapo nimekubaliana nawe kufanya kazi/shughuli fulani halafu isimalizike ujue hakutolalika hata uwe umechoka vipi hadi tumalize ndio nitaridhika.
7) Ndoto yangu kubwa ni kuona Africa inakukuwa na amani na kuacha malumbano ambayo yanasababishwa na WAROHO wa madaraka ambao wanairudisha sana nyuma AFRICA.
8) Kuna mambo mawili makubwa nimejifunza nje ya nchi
a) Wakati ni mali
b) Hakuna jambo lisilowezekana usipokata tamaa na kufanya juhudi
9) Jambo ambalo linaniudhi na halinipi amani ughaibuni ni CHAKULA
10) Una maoni gani kuhusu viongozi wa sasa nchini Tanzania?
Maoni yangu kwa viongozi wa Tanzania;
a) Viongozi wakumbuke kuwa Cheo ni DHAMANA. Viongozi wetu wanajisahau kuwa kuwa cheo ni dhamana ambayo wamepewa na wananchi wao.
b) Kiongozi anapaswa kuwa karibu na wananchi wake, kuwashirikisha wananchi wake kwenye maamuzi, kusikiliza wananchi wake, kiongozi apaswa kushirikiana na wananchi wake kutafuta ufumbuzi wa matatizo yanayowakabiri na sio kuwaacha au kuwatishia.
OMARY... pole sana kwani ice cream yako imeyayuka. LOL...... Ila usijali nitakuletea muda si mrefu nikija kwa kazi
Majibu ya maswali yako nitaanzia swali la 2 maana la 1 tayari limejibiwa, umenibana na maswali utasema wanipa interview ya kazi ya uwaziri mkuu au uraisi. LOL...
2) hebu tuambie myaka ileee uliokulia ww na hii yetu cc unaonaje?
Tanzania nimeondoka muda mrefu hivyo swali lako kidogo ni trick. Kuna tofauti kwani kipindi nilichokuwa nakulia mie hasa 1970s hadi 80s maisha yalikuwa simple. Watu hawakutaka vitu vingi kama sasa. Siku hizi hata mtoto mdogo wa miaka 11 humdanganyi kitu. Dismas anajua hilo. LOL...
3) unatushauli nini vijana i mean umekutana na Omary,Dis,Chaoga unataka umuas ungemwambia afanye nn ili awe mtt mwema na mwenye mafanikio?
Ningewaambia maisha ni mapambano na yataka discipline ya hali ya juu sana hivyo wasikate tamaa waendelee na mapambano hadi kieleweke.
5) ww tungekupa nafasi ya JK wa sasa ungefanya nn? kinachokukera?
Kuna vitu vingi sana vinanikera nchini Tanzania lakini nitataja vichache. Huduma ya afya ni mbovu na haifai yahitaji mabadiriko ya hali ya juu. Huduma ya maji safi hasa mijini ni mbaya. Usafiri hasa Dar ni wakusikitisha, watu wanamaliza muda mwingi njiani kuzidi wanaotumia kuwa na familia zao wamalizapo kazi. Hali ya usalama wa watu na mali zao ni mbaya na unatishia amani. Nchi kutokuwa na amani sio kuwa na vita peke yake, bali hata wananchi wake wasipokuwa na amani na usalama wao na mali zao na kutolala usingizi wakihofia majambazi au wezi kuvamia pia ni kukosa amani. Uongozi kusema ukweli ni mbaya, katiba yapaswa ibadirishwe. Ningepata nafasi ya uongozi ningebadirisha yote hayo yanayonikera hapo juu na pia ningebadirisha system nzima ya uongozi (haifai) na kufanya serikali/uongozi kuwa transparency na viongozi wangekuwa na mipaka, wale viongozi wazembe wasio na clear vision & sense of direction nisingewaonea haya.
6) TZ kunavijana wengi hawana ajira wanakaa mitaani wanavuta bangi na kunywa pombe za gongo,mnazi nk wakikuona ukipita wanaomba 500, 200 hayo ndio maisha yao wamekata kabisa tamaa je wa2 hawa ukikaa nao chini utawaambiaje? japo swali hili linashabiana na la namba 3
Vijana wengi wanataka njia za mkato katika maisha na wengi wao ni kutokana na background au malezi waliyokulia. Ningewashauri wasikate tamaa na maisha haraka haraka, lazima wajitume kwa moyo wao wote, watumie akili na juhudu. Huhitaji sh. laki tano kuanza biashara. Wakitumia ardhi wataepuka janga la umasikini.
7) sehem kubwa ya TZ imezunguukwa na mapori na hatuna faida nayo au niseme tunavyanzo vingi sana je ungekuwa muheshimiwa ungetafuta wawekezaji wawekeze kwenye nn?
Kwa upande wangu (as economist) nisingewekeza kwani mazingira hayaturuhusu. Tanzania haina sufficient economic policies ambazo zingeanda mazingira mazuri ya uwekezaji. Iwapo ningekuwa muhishimiwa na mazingira ya kuwekeza ni mazuri ningechagua sector ya KILIMO (mazao ya biashara, chakula, matunda na mifugo), POWER (umeme) & TOURISM. Ningechagua maeneo maalumu baadhi ya mikoa na kuwekezaji kwenye sector ya kilimo, hiyo ingesaidia nchi yetu kuwa na kilimo cha kisasa na wawekezaji wageni wana uwezo wa kutosha (in terms of logistic) kufikisha mazao sokoni kwa wateja na walaji kwani mazao mengi nchini Tanzania yanaozea vijijini/mashambani kwa kukosa usafiri kufika masokoni na pia hao foreign investors wangefikisha mazao yetu kwenye masoko ya kimataifa. Pia wakulima wadogo wadogo nchini Tanzania wangefaidika na utalaam toka kwa wakulima wenzao toka nje. Pia ningewekeza kwenye power (TANESCO) kwani bila umeme biashara na kazi/huduma (Hospitals, etc.). Pia ningewekeza kwenye TOURISM. Natural resources zetu yapasa tuzilinde na kuzitunza for future generations hivyo uwekezaji ni vizuri tuzingatie sustainable development. Nchi za magharibi wanahifadhi vya kwao for future generations huku wanakuja kuchukua vya kwetu. Tanzania kutokuwa na sufficient economic policies tumejikuta tuna attract insufficient investors (imperialists) ambao wanajali interests zao na nchi zao tu wakisha faidika baada ya miaka michache wanafunga office na kuiacha nchi yetu kwenye mataa.
8) TZ inawatoto yatima wengi sana wanalelewa katika vituo na mitaani watt hawasomi wanaishi kwa kuomba omba je unafikiri wakiwa wakubwa watafanya kazi gani? unaishauli nn? selikari ya tz? kuhusu watt hawa?
Suala la watoto wetu (Yatima) Tanzania ni la kusikitisha sana. Serikali imelisahau kabisa na kuwaachia wananchi na NGOs. Watoto wetu wanapasa kupendwa kama watoto wengine, wapewe elimu ya kutosha kama watoto wengine bila kubaguliwa ili tuwaandae kukabiliana na maisha kwani elimu ndio silaha kubwa kwa mtoto.
Nawaomba ndugu zangu wapendwa wote tuungane na kujihusisha na watoto wetu kwa njia moja au nyingine hata iwe kupitia NGOs, vituo vya dini (makanisa + Misikiti), etc. Huhitaji kuwa na pesa nyingi au tajiri kusaidia watoto yatima. Mfano mzuri ni mdau mwenzetu wa humu Tulonge anayitwa CHIBIRITI amekuwa mstari wa mbele kusaidia Yatima. God bless him…..
mama malaika nashukuru saana kwa majibu yako...maana maswali yangu mengi tiari umeulizwa na umejibu ki ufasaha...Inatoa changamoto kwa wadogo zako ambao tuko nasi nje tunatafuta "kieleweke" nina maswali mawili matu ya nyongeza kwa hayo ya wadau:
1) hivi wewe huko England umeishi muda gani hadi sasa?
2) mila za wazungu nazo unazionaje?....au kuna kitu gani kinakukera katika mila za Ughaibuni?
3) Unalifikiriaje swala la mtu akiwa ulaya na baada ya kupata makaratasi antosa passport ya bongo na kuchukua urahia wa nje ?
4) katika fikira zako (ukiwa kimya)....unatamani sana kuishi huko au bongo ndo penyewe?
Haya ndo hayo mama. salimia familia yako!!!
© 2021 Created by Tulonge.
Powered by