Tulonge

MIAKA MITANO YA SERIKALI YA KIKWETE,NINI MAONI YAKO?

Wote tumeshuhudia utawala wa Serikali ya Kikwete kwa kipindi cha miaka mitano. Una lipi la kuchangia? Unadhani aliyoyafanya yatamuwezesha kupata uraisi kwa kipindi kingine cha miaka mitano?

Views: 698

Reply to This

Replies to This Discussion

Mimi kwa mtazamo wangu wa haraka haraka, umaarufu alioingia nao JK mwaka 2005 umeporomoka ghafla sana. Mwaka huu ana kazi ngumu na ninahisi kuna wizi mkubwa wa kura utatokea na matokeo yatabadilishwa kwa kila namna. Kuporomoka kwa umaarufu wake (mtu aliyependwa sana kuja kuwa mtu anayechukiwa) kunatokana na ahadi nyingi zisizotekelezwa na serikali yake kujaa ufisadi wa wazi wazi. Ni hayo tu kwa sasa, nitarudi baadae na mengine zaidi.
Hakuna lolote alilofanya. Siwezi kupoteza muda wangu kumzungumzia sana.
Tunataka mabadiliko sasa. Tumechoshwa na ahadi za chama kimoja kila cku ambazo hazitekelezeki. Mimi sijaona alichofanya.
Jamani nitarudi soon! ngoja kwanza hasira zipungue.
Hahahhaaaa najua tu mzee Cha utakuja kuua.
Ni mtu wa ajabu sana, amekuwa rafiki wa waharifu wa nchi hii. Majuzi katika taarifa ya habari pale ITV katika mikutano yake kule Iringa, alionekana akimkumbatia mtu anayejulikana kama MWAKALEBELA, mtu ambaye ana kesi mahakamani akituhumiwa kwa kutoa rushwa katika kura za maoni. Hii inaashiria nini kwa Wtanzania? Mtu anayejinadi kupigana vita dhidi ya Ruushwa then anaonekana akimkumbatia mtuhumiwa wa rushwa ina maana gani. Nilijiuliza maswali mengi sana bila majibu, nikabaki kujisemea au mtu huyu ana MENTAL DISORDER!! Watanzania ni wakati wa kufanya maamuzi sahihi na mazito. Huyu si mtu wa kurudishwa ikulu. Na kama litafanyika kosa la kumrudisha ikulu, basi kuna balaa kubwa sana linakuja mbele yetu. Mwenye macho aone na mwenye masikio asikie.

Mungu Ibariki Tanzania!
Yaani hilo la Mwakalebela ndo limekamilisha kumbatia kumbatia yake ya mafisadi, wezi, waporaji na wabakaji wa mali za umma. Huyo jamaa alikuwa na miaka mitano ya mwanzo na akafanya mabaya yote haya akijua kabisa kwamba kuna kipindi kingine cha uongozi, je akipewa miaka mitano ambayo anajua kabisa itakuwa ya mwisho kwake si atatuuza kabisa. Jamani nawaombeni watu tufikiri sana sio kufanya ushabiki na kupiga kura kwa mazoea. Ni mara mia usipige kura kuliko kuchagua uozo.
mh asanteni kwa hoja!
huyu mkuu mi naona hajafanya jipya zaidi ya kuzindua miradi aliyoianza mzee wa awamu ya tatu,cha zaidi ni trip kwa sana.na sisi kazi yetu kumsifia ooh mara rais wetu handsome,hahaahahaa.kushinda atashinda hilo liko wazi nchi yetu vyama vya upinzani kwa upande wa urais havina nguvu,ila kwa huku visiwani ucpime.
Mm kwa mtazamo wangu naona amereta mabadiliko ila hata kama mtu ukimjengea nyumba ya gorofa 20 hawezi kuridhika hata ukimpa nini na kama huoni alicho fanya nenda kapige kuratiki jakaya kikwete.
tuwape wote chance kama vile simu za mikononi washindane huku ss tunapata faida utawala wa mseto
No comments

Reply to Discussion

RSS

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*