Tags:
Ni mtu wa ajabu sana, amekuwa rafiki wa waharifu wa nchi hii. Majuzi katika taarifa ya habari pale ITV katika mikutano yake kule Iringa, alionekana akimkumbatia mtu anayejulikana kama MWAKALEBELA, mtu ambaye ana kesi mahakamani akituhumiwa kwa kutoa rushwa katika kura za maoni. Hii inaashiria nini kwa Wtanzania? Mtu anayejinadi kupigana vita dhidi ya Ruushwa then anaonekana akimkumbatia mtuhumiwa wa rushwa ina maana gani. Nilijiuliza maswali mengi sana bila majibu, nikabaki kujisemea au mtu huyu ana MENTAL DISORDER!! Watanzania ni wakati wa kufanya maamuzi sahihi na mazito. Huyu si mtu wa kurudishwa ikulu. Na kama litafanyika kosa la kumrudisha ikulu, basi kuna balaa kubwa sana linakuja mbele yetu. Mwenye macho aone na mwenye masikio asikie.
Mungu Ibariki Tanzania!
© 2021 Created by Tulonge.
Powered by