Tulonge

MIAKA MITANO YA SERIKALI YA KIKWETE,NINI MAONI YAKO?

Wote tumeshuhudia utawala wa Serikali ya Kikwete kwa kipindi cha miaka mitano. Una lipi la kuchangia? Unadhani aliyoyafanya yatamuwezesha kupata uraisi kwa kipindi kingine cha miaka mitano?

Views: 698

Reply to This

Replies to This Discussion

Miaka mitano ya kikwete haina tofauti na miaka mingine ya viongozi wa CCM waliyotangaza Tanzania... urasi atapata tu lakini si kwa aliyoyafanya
Mmmmh....! wizi mputu!
Wala sio MENTAL DISORDER, ana akili zake kabisa timamu. Toka lini mwizi akamsahau mwizi mwenzie? Alimkumbatia sababu na yeye ni mwizi wa kura pia kama Mwakalebela. Wanaiba kura, wanaiba mali ya umma na hadi kuiba maisha/roho za watu. Wanaiba hadi kodi yangu inayokuja bongo kwa njia ya misaada. Mungu atawalaani walafi na mafisadi wote. Ndio maana wengine wanaanguka anguka hadharani.Cha the Great said:
Ni mtu wa ajabu sana, amekuwa rafiki wa waharifu wa nchi hii. Majuzi katika taarifa ya habari pale ITV katika mikutano yake kule Iringa, alionekana akimkumbatia mtu anayejulikana kama MWAKALEBELA, mtu ambaye ana kesi mahakamani akituhumiwa kwa kutoa rushwa katika kura za maoni. Hii inaashiria nini kwa Wtanzania? Mtu anayejinadi kupigana vita dhidi ya Ruushwa then anaonekana akimkumbatia mtuhumiwa wa rushwa ina maana gani. Nilijiuliza maswali mengi sana bila majibu, nikabaki kujisemea au mtu huyu ana MENTAL DISORDER!! Watanzania ni wakati wa kufanya maamuzi sahihi na mazito. Huyu si mtu wa kurudishwa ikulu. Na kama litafanyika kosa la kumrudisha ikulu, basi kuna balaa kubwa sana linakuja mbele yetu. Mwenye macho aone na mwenye masikio asikie.

Mungu Ibariki Tanzania!
Yaani kwa kweli hilo kosa limeshafanyika ingawa kwa kiasi kikubwa sio sisi tuliofanya kosa hilo bali ni Tume ya Uchaguzi, imetoa matokeo yake yenyewe ingawa kura tulipiga sisi. Halafu nadhani waTanzania tumerogwa, inakuaje kule vijijini kwenye matatizo zaidi ndiko JK kachaguliwa zaidi, ina maana wameridhika na matatizo yao!! Mimi nadhani hawa watu ambao wako vijijini na ambao ni mzigo kwetu sisi tulio mjini, kwa kuwa tunawasomeshea watoto wao na kuwahudumia kuna haja ya kuwaacha wasaidiwe na serikali yao.

Reply to Discussion

RSS

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*