Tulonge

Michango ya harusi INANIKERA kweliiiiiiii.

Michango ya harusi ni moja kati ya vitu VINAVYONICHEFUA katika maisha yangu kwa sasa. Imekuwa ni kitu cha kawaida kwa watu kuchangisha wenzao pindi wanapotaka kuoa.Kwa nini usumbue wenzako kwa kutoa hela ambayo hawajapangia kwa starehe yako binafsi? Kwani ni lazima kafanya sherehe kubwa,unatakiwa ufanye sherehe unayoweza kuigharamikia mwenyewe bila kisumbua mtu then alika watu wachache tu.

Hapo hapo ukiwaambia watu wamchangie mgonjwa aliye mahututi hospitali watakuona waajabu sana. Mimi naona huwa tunatoa hela za harusi kinafiki (tunaogopa lawama) lkn si kutoka moyoni. Hata kama ni kutoka moyoni mimi sioni haja ya kuchangiana kwenye harusi pamoja na sherehe nyingine zisizo na lazima. Mtu asije akaniambia nimchangie harusi,nitamshushua hadi akome.

Wewe unaonaje?

Views: 1210

Reply to This

Replies to This Discussion

Wanadamu tumekuwa WATU wa ajabu sana! Tunaongozwa na hisia zetu kama wanyama, tumeondokana na uhalisia wetu sasa tunaendeshwa na mazingira na vishawishi vya nje! Kila mmoja anajaribu kuwa bora zaidi ya mwingine kwa kufanya jambo zaidi ya alilofanya mwenzake! Michango ya harusi, kipaimara, ubatizo, ubarikio, birthday, kitchen party, unyago, sendoff na sherehe zote za mtazamo wa aina hy ni kupoteza dira kwa cc wanadamu na kuckiliza hisia zetu kuliko kutazama UHALISIA. Mfano, juzi nimesikia harusi ya bwana mm

Duh, kali hiyo kwa hiyo sisi ambao hatujaoa umeshaweka kikwazo tusichukue mchango kutoka kwako, achilia mbali hayo dadangu huo ni mtazamo wa mtu binafsi. Kuna watu hufanya sherehe zao bila kutoza michango na wengine huchangisha, jambo hili limeshakuwa kama desturi kwani utakuta wengine wanaa hata umoja wao. Na ikifika zamu yako pia watakuchangia.

 

Mhimu ni weewe unaishi na jamii ya namna gani?? Na unamitazamo gani kuhusu maisha??? Kwani wengine huchangia kwa kuwa watapat mpunga na vitu vingine!!

 

Mi nafikiri kama mtu anaweza akafanya mwenyewe ni jambo zuri na mtu kama atampa isiwe lazima iwe ni kwa hiyari yake. Na hata hivyo kuwasaidia wagonjwa na wale wenye mahitaji nibora na utapata thawabu kuliko kuchangia shwerehe na tafrija.

 

 

Yaani dada yangu umesema kweli kabisa....sisi ni watu maskini, lakini harusi zetu balaa...angalia wenzetu Ulaya walioendelea na mali wanazo zakutosha lakini hawafanyi kabisa harusi tufanyazo Bongo, huwa najiuiza sana kuhusu swala hili, sijui ni ulimbukeni au? Nilishawahi kusema swala hili kule kwenye Blog ya Michuzi, watu walitaka kuniuwa na comment zao mbaya kunipinga kuhusu swala hili. Tukiambiwa tuchangie maswala muhimu ya Jamii tunakuwa wakali kama Mbogo...lakini kwenye mambo haya safi tu. Lakini wakati mwingine watu tunasadiki sana kuwa tukichangia tutakula na kunywa kwa sana...hili ndilo linalotusukuma sana mpaka tuchangie. Ila mimi binafsi sipendi kweli...nakuunga mkono sana tena sana Dada Belita kwa hoja yako hii.

Kaka Silas unaonekana kulifagilia kidogo suala hili la kuchangishana michango ya sherehe zisizo na lazima. Kinachotakiwa ni kuacha kabisa kuwaambia watu wakuchangie,maana wengine wanaweza kukuchangia kwa kuona aibu kukutosa lkn moyoni hawapo radhi.

Natamani serikali ianzishe sheria ya KUKATAZA vikali kuchangisha michango ya harusi na sherehe nyingine zisizo za lazima. Kiukweli michango hii inarudisha nyuma maendeleo,mfano toka januari hadi sasa mimi nimeletewa kadi za harusi zinazonihitaji nitoe  si chini ya sh 1,000,000.Sasa nikiamua kuonesha usamalia wa kipumbavu kwa kutoa hela zote hizo si hasara kwangu?

Michango ya harusi ni UPUUZI,hakuna cha kutetea wala nini.

 

Silas A. Ntiyamila said:

Duh, kali hiyo kwa hiyo sisi ambao hatujaoa umeshaweka kikwazo tusichukue mchango kutoka kwako, achilia mbali hayo dadangu huo ni mtazamo wa mtu binafsi. Kuna watu hufanya sherehe zao bila kutoza michango na wengine huchangisha, jambo hili limeshakuwa kama desturi kwani utakuta wengine wanaa hata umoja wao. Na ikifika zamu yako pia watakuchangia.

 

Mhimu ni weewe unaishi na jamii ya namna gani?? Na unamitazamo gani kuhusu maisha??? Kwani wengine huchangia kwa kuwa watapat mpunga na vitu vingine!!

 

Mi nafikiri kama mtu anaweza akafanya mwenyewe ni jambo zuri na mtu kama atampa isiwe lazima iwe ni kwa hiyari yake. Na hata hivyo kuwasaidia wagonjwa na wale wenye mahitaji nibora na utapata thawabu kuliko kuchangia shwerehe na tafrija.

 

 

Dada Belita wewe umeshaolewa nini? Ila ni kweli,inakera sometimes.
Dah! dada Belita naona umeandika kwa machungu.Yani umekiweka hadharani kilicho moyoni mwako, kweli imekugusa hii ishu.Nitarudi kutoa maoni yangu.
Mi niseme kutoa ni MOYO na si UTAJIRI. Siungi mkono kuchangishana.. ILA... Mtu akipenda kuchangia mwenyewe BINAFSI.. sioni kama kunashida. Tatizo linakuja kwamba sasaivi TUNALAZIMISHANA KUTOA MICHANGO.. TENA KWA KUWEKEANA VIWANGO.. Mfano. Bwana na BIBI... 60,000. Bwana or Bibi 40,000. Sasa hihi ni nini?  Hii kitu inakera Sana!
dada Belita umenitisha kwa hiyo nisikupe kadi ya mchango utanishushua?
Mchango ni hiari na si lazima na hao wanaomtumia mtu ujumbe kwa kumlazimisha achange haifai. Mara nyingi nionavyo mimi mtu tangaza siku ya harusi wanaokupenda na kukujali wenyewe bila ya kuwasumbua watakupa zawadi tosha kabisa! Ni kama sadaka kanisani si kulazimishwa ulichonacho na unachoweza.!

Nipo pamoja na wadau wote ambao wanasema michango hii ya harusi sio kabisa. Mimi mwenyewe hapa nilikuwa nalipiga vita sana najamaa zangu nawaambia kabisa jamani kama unaenda kuoa ni wewe na mke wako kwanini mtuchangishe sisi pesa? Wakati kama kunakijana anashida ya kwenda shule hakuna hata mmoja anayeweza kuchanga kwakijana yule.

Tubadilike vijana kwani bila kubadilika maendeleo tz bado sana. Sidhani kufanya harusi ya mbwembwe nyingi ndo ufahari wakati wagonjwa wanakufa hakuna madawa/madaktari/mashule/vitabu na vitu kibao. Leo hii baada ya vijana wa tz tuungane nakuwa kitukimoja hili tuweze endeleza nchi yetu hasa hizi rasilimali zinavyowafaidisha wachache sisi tunabakia kufanya harusi na siku za kuzaliwa sherehe. Yani baba Dismas tupo pamoja nna wadau wote, ninauzika mm khaaaaa.


Hapo sas, utanipangiaje kwamba heti nitoe siochini ya kiasi fulani?
Dixon Kaishozi said:
Mi niseme kutoa ni MOYO na si UTAJIRI. Siungi mkono kuchangishana.. ILA... Mtu akipenda kuchangia mwenyewe BINAFSI.. sioni kama kunashida. Tatizo linakuja kwamba sasaivi TUNALAZIMISHANA KUTOA MICHANGO.. TENA KWA KUWEKEANA VIWANGO.. Mfano. Bwana na BIBI... 60,000. Bwana or Bibi 40,000. Sasa hihi ni nini?  Hii kitu inakera Sana!

Huu upuuzi huwa siupendi kwelii. Huwa naona noma kusema pindi ninapopewa kadi. Ila inarudisha nyuma maendeleo ya watu na inasababisha kuonana wabaya pindi unaposhindwa kutoa mchango. Mimi mtu aandae sherehe kwa gharama zake halafu awaalike rafiki/ndugu zake awatakao. Kama hawezi asifanye sherehe kabisa,atoke kanisani/msikitini arudi nyumbani kulala na mkewe wale tunda kihalali kwa raha zao.

 

Tena wenye tabia ya kupenda kuachangisha michango ya harusi zaidi ni WAKRISTO, wenzetu waislamu siyo sana kivile. Hawamaindi harusi kubwa kwa sana.

Reply to Discussion

RSS

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*