Michango ya harusi ni moja kati ya vitu VINAVYONICHEFUA katika maisha yangu kwa sasa. Imekuwa ni kitu cha kawaida kwa watu kuchangisha wenzao pindi wanapotaka kuoa.Kwa nini usumbue wenzako kwa kutoa hela ambayo hawajapangia kwa starehe yako binafsi? Kwani ni lazima kafanya sherehe kubwa,unatakiwa ufanye sherehe unayoweza kuigharamikia mwenyewe bila kisumbua mtu then alika watu wachache tu.
Hapo hapo ukiwaambia watu wamchangie mgonjwa aliye mahututi hospitali watakuona waajabu sana. Mimi naona huwa tunatoa hela za harusi kinafiki (tunaogopa lawama) lkn si kutoka moyoni. Hata kama ni kutoka moyoni mimi sioni haja ya kuchangiana kwenye harusi pamoja na sherehe nyingine zisizo na lazima. Mtu asije akaniambia nimchangie harusi,nitamshushua hadi akome.
Wewe unaonaje?
Tags:
Hapa mezani kwangu nina kadi 6 natakiwa nitoe michango ya harusi. Na hizo harusi zenyewe ni kuanzia mwezi October hadi December na zafanyika Dar.
Kuanzia mwezi January mwaka huu hadi sasa nimetumiwa kadi za michango ya Harusi, Ubatizo na Kipaimara na zote kwa ujumla zimefikia kadi 32. Na mwaka mzima sijachanga hata shilling sana sana nimechangia Misiba, Ada za Shule za watoto na matibabu.
Kusema ukweli imefikia wakati watanzania tupunguze makubwa, tufanye yale tu ambayo yako chini ya uwezo wetu na sio yaliyo juu ya uwezo wetu.
© 2022 Created by Tulonge.
Powered by