Tulonge

 Vipi nyie kinadada mmepata wapi kuingia katika zama za ujinga za kuchubua  ngozi kwa kutak kubadili rangi ya mwili.Eti! kisababu cha kuvumta mpenzi au kubadili mazingira.

Tafadhalini, tusaidie kitendo chenu hiki hasa kinakusudia nini hasa na nini lengo ? - TUELIMISHENI WAJINGA - TULONGEEEE !!!!

Views: 1275

Reply to This

Replies to This Discussion

Baelezee bakome benyewe
mimi hapo huwa sielewi kabisa maana rangi uliyopewa na mungu ndo nzuri.

Mie sio mpenzi wa mkorogo kwani mkorogo unazeesha sura, unakunja ngozi yako, unaleta mabaka mabaka kwenye ngozi na zaidi ya yote mkorogo una sumu, na mkorogo waweza leta skin cancer. Kuna lotion nyingi tu nzuri mwanamke aweza tumia iwapo anapenda ngozi iwe nyororo na rangi kung'ara uzuri. Na kama mtu hana pesa ya kutosha kuna vitu vya asili kama vile asali, mayai, etc. vyaweza fanya ngozi yake iwe laini.

Mungu alitupendelea sana kutupa ngozi nyeusi ila basi tu wengi sijui hatuelewi au ndio ugonjwa? Ngozi nyeusi isiyo na mkorogo ni nzuri sana na ina kinga ya asili juu ya magonjwa ya ngozi na ina tukinga na mionzi mikali ya jua inayoingia mwilini kupitia kwenye ngozi yetu. Hivyo mtu anapotumia mkorogo anapunguza melanin, mionzi (radiation) toka kwenye jua ikipiga kwenye ngozi inaingia moja kwa moja kwenye mwili na ngozi inashindwa kutengeneza Vitamin D. Na mtu mwenye kutumia mkorogo akitembea sana juani utaona jinsi ngozi inavyoathirika. Mume wangu wakati mwingine anatamani angekuwa na ngozi nyeusi kama zetu, na sio yeye tu wako wengi weupe wanapenda ngozi yetu sababu wanajua faida yake. Ngozi inapokosa melanin au inapokuwa na less melanin mtu unakumbukwa na viji-magonjwa vingi vya ngozi vya kipuuzi na wakati mwingine inam-bidi avae mashati ya mikono mirefu hata kuwe na joto kali na kofia na kupaka sun creams ili kujikinga na mionzi ya jua ambayo mie hainiathiri kutokana na ngozi yangu imejitoseheleza kinga ya asili. Wanangu nao wana matatizo kama ya baba yao ingawa ngozi yao ni mchanyiko hawaruhusiwi kutembea kwenye jua kali bila ya sun creams, kuvaa kofia na nguo za mikono mirefu ili kuzuia jua. Mie mama yao nadunda tu hata nikija Tanzania kwenye jua kali bado siathiriki.

Wenzetu weupe wengi wanashauriwa na doctors kutumia vidonge vya Vitamin D (as a supplement) sababu chakula peke yake haitoshi, mimi na wewe hatuhitaji sababu miili yetu imejaaliwa ngozi ambayo inasaidia ku-produce Vitamin D kutoka kwenye mionzi ya jua

Asante sana ,Mama MALAIKA.

Wape darasa hao kina mama wa taifa la leo.Tena kinachonishangaza unawaona magraduate ladies ,elimu zao wala haziwasaidii kujikuta wameingia kwenye mkumbo wa kuchubua ngozi kuutaka weupe bila ya kujua huo weupe si weupe ila ni tabaka la pili ya ngozi ambayo iko dhaifu kuliko tabaka la mwanzo wa ngozi na tabaka la tatu ni nyama ya mwili.

Mbio zangu, kuona asasi za kijamii AU taasisi ya kitengo cha afya na Ustawi wa Jamii - kupigia kelele hili ili kunusuru watumizi wa MKOROGO.

 

Endelea ......

Reply to Discussion

RSS

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*