Utajisikiaje endapo mwezi mtukufu ukaongezwa muda na kuwa miwili mfululizo? Sema ukweli wako. Maana kuna wengine mnaombea uishe haraka haraka
Tags:
unajua kila mwezi au kila siku iendayo kwa Mungu ni Tukufu hatimaye kutimia mwezi. sasa kwa wale wanaojizuia kufanya maovu @ kisa mwezi mtukufu wapo wrong kwani utakuwa hujafanya kitu bado kama ukiamua kuwa baridi kuwa na ukiamua kuwa moto kuwa moto namaanisha simamama pale unapoona unaweza kusimama hata kama ni kwenye tanuru la moto wewe simama tuu ili mradi unaweza kufanya hivo.
nina marafiki zangu ambao @ kwa mwezi huu ambao ni wa Ramadhani wanavaa hijabu na madera na baibui lakini ni watu wa kuvaa mibano ya kufa mtu huwa nawaambiaga waendelee vile daima hadi wanaiaga dunia wanasema haiwezekani ni kwa mwezi huu tuu basi huwa nawaambia ni bora wasifunge.
Kwa wenzangu waislamu huu ni mwezi wa toba cha msingi maisha yako uwe unaishi maisha ya toba pale pindi unapoona umemkosea Muumba. lakini eti siyo kwa sasa huendi bar @ mwezi mtukufu kila siku ni tukufu ila itategemeana na imani yako na maisha yako ya kila siku na jamii inayokuzunguka.
Kwaherini nawatakia siku njema poleni na swaumu
Teh teh hv wewe Severin huwa unafikiria nini sijui. Naona unataka kupigwa na baadhi ya waislamu. Kiukweli mwezi huu unaonekana kuwakosesha uhuru waislam wengi, hili linathibitishwa na maovu(ulevi,ngono nk) kibao yanayofanywa siku ya kwanza tu baada ya mfungo kwisha. Ni kama walikuwa kifungoni, na sasa wapo huru.
Pia wana kauli yao ya kuvunja jungu kabla ya kuingia kwenye mfungo. Yani wanamalizia kutenda maovu kabla ya kuingia kwenye mfungo.
Wengi wanafunga kwa mazoea na kuogopa kushangawa na waislamu wenzake endapo hatafunga. Bora mwenzenu OMARY kaamua kuwa muwazi. Kila siku tunakula naye kwa mamalishe hahaahaaaaa.
© 2021 Created by Tulonge.
Powered by