Tulonge

Mnaonaje uongezeke mwezi mtukufu mwingine?yani ukiisha huu uanze mwingine. Hapo ndiyo utawajua waislamu wa kweli.

Utajisikiaje endapo mwezi mtukufu ukaongezwa muda na kuwa miwili mfululizo? Sema ukweli wako. Maana kuna wengine mnaombea uishe haraka haraka

Views: 604

Reply to This

Replies to This Discussion

Mimi naona uendelee tu mwaka mzima maana unanizuia nisifanye maovu na kuniwezesha kufanya mema..!!Yaani mtu unakuwa saint hata kudanganya unaogopa huu mwezi safi sana!
Hongera Alfan maana kuna wengi wanaomba uishe mapema ili warudi kufanya mambo yao!

unajua kila mwezi au kila siku iendayo kwa Mungu ni Tukufu hatimaye kutimia mwezi. sasa kwa wale wanaojizuia kufanya maovu @ kisa mwezi mtukufu wapo wrong kwani utakuwa hujafanya kitu bado kama ukiamua kuwa baridi kuwa na ukiamua kuwa moto kuwa moto namaanisha simamama pale unapoona unaweza kusimama hata kama ni kwenye tanuru la moto wewe simama tuu ili mradi unaweza kufanya hivo.

 

nina marafiki zangu ambao @ kwa mwezi huu ambao ni wa Ramadhani wanavaa hijabu na madera na baibui lakini ni watu wa kuvaa mibano ya kufa mtu huwa nawaambiaga waendelee vile daima hadi wanaiaga dunia wanasema haiwezekani ni kwa mwezi huu tuu basi huwa nawaambia ni bora wasifunge.

 

Kwa wenzangu waislamu huu ni mwezi wa toba  cha msingi maisha yako uwe unaishi maisha ya toba pale pindi unapoona umemkosea Muumba. lakini eti siyo kwa sasa huendi bar @ mwezi mtukufu kila siku ni tukufu ila itategemeana na imani yako na maisha yako ya kila siku na jamii inayokuzunguka.

 

Kwaherini nawatakia siku njema poleni na swaumu

Alfan naona humtakii mema Chaoga, mwaka mzima ukiwa mwezi mtukufu ina maana itabidi aache kunywa. LOL....

Teh teh hv wewe Severin huwa unafikiria nini sijui. Naona unataka kupigwa na baadhi ya waislamu. Kiukweli mwezi huu unaonekana kuwakosesha uhuru waislam wengi, hili linathibitishwa na maovu(ulevi,ngono nk) kibao yanayofanywa siku ya kwanza tu baada ya mfungo kwisha. Ni kama walikuwa kifungoni, na sasa wapo huru.

Pia wana kauli yao ya kuvunja jungu kabla ya kuingia kwenye mfungo. Yani wanamalizia kutenda maovu kabla ya kuingia kwenye mfungo.

Wengi wanafunga kwa mazoea na kuogopa kushangawa na waislamu wenzake endapo hatafunga. Bora mwenzenu OMARY kaamua kuwa muwazi. Kila siku tunakula naye kwa mamalishe hahaahaaaaa.

We dis vibaya hivyo kumtaja mwenzio kuwa hajafunga!!
Hapana bana, Omary kafunga ila huwa namzingua. Amelelewa ktk maadili ya kislam huyu jamaa, HAPENDI kabisa kutenda dhambi teh!

Reply to Discussion

RSS

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*