Kwa masikitiko makubwa napenda kuwapa taarifa kuwa nyumba ya mdau mwenzetu Hassan Damnani imeteketea kwa moto pamoja na vitu vyote huko Mombasa usiku wa tarehe 30/08/2012.
Naomba tumsaidie mdau mwenzetu kwa hali na mali katika kipindi hiki kigumu. Waweza tuma mchango wako kwa Tigo Pesa (0716 528842) au M pesa (0767 528842).
Namba ya simu ya muhusika Bw. Hassan ni (+254733724838), waweza mpigia kwa maelezo zaidi. Pia waweza wasiliana na muhusika kwenye ukurasa wake wa facebook hapo chini endapo utahitaji kumsaidia kwa njia nyingine.
https://www.facebook.com/hassandamnan
Angalizo:
Tulonge imefikia uamuzi huu wa kumchangia mwenzetu baada ya kukubaliana na muhusika mwenyewe. Wadau watakao mchangia watawekwa wazi hapa tulonge pamoja na kiasi alicho changia kama tufanyavyo kwenye michango ya watoto yatima, isipokuwa mdau akipenda jina lake lisitajwe.
*Nguvu ile ile tuitumiayo kwenye kuchangia HARUSI naomba tuitumie na hapa*
Picha zaidi za tukio:-
Hii ndiyo nyumba ya Mzee Hassan ambayo imeteketea kwa moto na vitu vyote. Ila wana familia wote wapo salama. Huyo aliyeipa mgongo kamera ndiye Mzee Hassan mwenyewe.
Tags:
Pole sana maalim wangu inshallah
DAH MACHOZI YAMENITOKA POLE SANA KAKA YANGU, TUPO PAMOJA CHA MSINGI WEWE NA FAMILIA YAKO MPO SALAMA
POLE sana kwa tukio hilo.Mungu akutie moyo na akupiganie ktk kuyarudisha maisha katika hali yake ya kawaida
asante mama malaika huo ni mtihani wa mola na inshallah kuna kheri mbele
hassan damnan said:
Mama Malaika asante sana dada zaidi ni kumshukuru mola tumetoka salamaDuh! Hadi nimeishiwa nguvu kusoma habari hii, pole sana kaka Damnan.
asanteni sana nyote kwa kunipa pole na kuniliwaza mola awabariki na awalinde nyote ndugu zangu
eddie said:
Pole sana kaka. asante kaka
asante sana kakangu
KUNAMBI Jr said:
Pole sana maalim wangu inshallah
asante sana dadangu mpendwa namshukuru maulana tumetoka salama
ANGELA JULIUS said:
DAH MACHOZI YAMENITOKA POLE SANA KAKA YANGU, TUPO PAMOJA CHA MSINGI WEWE NA FAMILIA YAKO MPO SALAMA
Hii ni hatari bin Danger,pole sana ndugu yangu,Mwenyezi Mungu akupe Moyo wa Subira,Mkumbuke Nabii Ayyubu alipata mitihani kibao kupita maelezo,akawa na subira na kumtegemea Muumba,hatimae Muumba akampoza na kumuodolea matatizo yaliyomkuba,hakika subira ni kitu muhimu sana,lakini si subira tu bali pia na kutawakkal kwa Mwenyeezi Mungu,hakika Mola huwapenda sana wanaosubiri na kuvumilia huku wakizidi kumuomba kwa wingi.
© 2021 Created by Tulonge.
Powered by