Inanikera sana,Imekuwa ni kitu cha kawaida sana kwa wanawake kuonekana malaya sana pale inapogundulika ametembea na mwanaume mwingine nje ya ndoa yake,hata kama ni mara moja tu. Lkn mwanaume akitoka nje ya ndoa hata mara 100 huonekana ni kitu cha kawaida tu,na hujiona wana haki ya kufanya hivyo. Hata jamii haiwezi mchukulia vibaya sana ukilinganisha na mwanamke akifanya hivyo.
Unaweza mfumania mumeo zaidi ya mara 10 lkn yakaisha juu kwa juu hata kama ukilifikisha suala hilo kwa wazazi wa pande zonde mbili.Lkn akifumaniwa mwanamke siku 1 tu huwa ni balaa,utasemwa na familia za pande zote mbili na majirani pia autadhani umeua mtu. Pia taraka itakufuata nyuma.
Hii ni haki?
Tags:
Pole mrembo!!!
hiyo ndio jamii tunayoishi......
yenyewe huwa inajiona iko sawa isipokuwa mwanajamii ndio mkosefu!
ok inanilazimu nielezee vizuri kidogo, kifupi ni hivi, kwanza ninavyofahamu mimi, kutokana na mazingira tuliojijengea zaidi, huwa mwanamke akiwa mzinzi huwa tunamuina malaya, mwanaume huwa tunamuita muhuni, kwahiyo, kuna tofauti hapo,
halafu mada ya mwanamke kutoka nje ya ndoa na kuitwa malaya kunasababu nyingi zinazoongelewa kwamba hatoshelezwi na mumewe, kumbe tulisha sahau, kwamba binadamu wote hatufanani kitabia, wapo wanawake hurka yao ni hiyo, kwamba yeye hata atoshelezwe vipi atatoka tu nje ya ndoa, wapo wasiotoshelezwa na akajua huyu ni mumewangu nifanye nini ili anitosheleze, nicheze nae vipi ili namimi nisijitie aibu kwenye jamii nikamzalilisha mumewangu au na mimi wakaniona malaya,
na kwa upande wa wanaume, nao kama nilivyoeleza hapo juu,
kwahiyo jibu ni kwamba, kukitoka nje ya ndoa kama ni mwanamke kama jamii itakuona lazima wakuite malaya, na kama ni mwanaume lazima wakuite muhuni, mzinzi, msaliti wa ndoa yako, wewe jitulize na mpenzi wako au mume wako mmoja uone kama watakuita hivyo,
binadamu huishi kulingana na mazingira aliojengewa tangu awali,,,
TAKE CARE UKIMWI UPO NA UNAUA,,
SASA HIVI KULIKO MALARIA
Hapa natoa macho tu na misikio kusikiliza wadau mnavyolonga. Ngoja nimalize kusoma habari ya uzinzi wa Arnold Schwarzenegger na pia yule boss wa IMF aliyetiwa ndani huko New York kwa tamaa ya ngono (uzinzi) halafu nitarudi baadae ku-comment.
Diana mpenzi !
Nasema kauli ya jibu lake - NDIO NDIO KABISA !!!
MWANAMKE kwenye ndoa hapaswi kabisa kutoka nje ya ndoa yake,kufanya hivyo ni UMALAYA ,LAANA na kila aina ya matusi anastahili kupata.
Haya yanajiri kwasababu 2 nzito ambazo kwakwe ni kufuli:
Kitendo chake cha kutoka nje ya ndoa ni dhulma na uhaini,kwani kutembea na mwanamme mwengine asiekuwa mume kuna haya yana nafasi ya kutokea :
Wito kwa wanawake wenye ndoa waheshimu mipaka yao.
Na huyu mwanamme anaetembea ovyo nje ya ndoa yake ana haya yafutayo:
Wito kwa wanaumme wenye ndoa ni vyema waheshimu ndoa zao.
Lakini majina mabaya hayamfiki mwanamme kwa vile yeye kwa yeye ajipotezea binafsi yake lakini mwanammke anavuruga na kuandaa hatari ya jamii yote inayomzunguka.
Ndio,(Allah S.W) AKATUHALALISHIA wanaumme kuoa zaidi ya mke mmoja kwa kuweka msingi imara wa ustawi wa jamii miongoni mwa watu na maisha yao.
DIANA ! mwanammke kuwa MALAYA - NOOOMAA! mwanamme -NOOMA KICHIZI
Huo ni mchango wangu kwa wanatulonge !!!!
© 2023 Created by Tulonge.
Powered by