Asha Musa (katikati) akiwa na bibiu yake na mtoto wake. (Picha na Shakira Nyerere,mwananchi)
Siku ya tarehe 20 Jan 2013 tovuti ya www.mwananchi.co.tz ilitoa habari ya msichana mwenye ulemavu wa viongo vya mwili karibu vyote ambaye alibakwa. Binti huyo analelewa na bibi yake na ana mtoto mmoja wa kiume(6) ambaye pia alimpata baada ya kubakwa siku za nyuma.Bofya hapa kusoma zaidi.
Habari hiyo nilii-share hapa tulonge, ndipo Grace Kamonga ambaye ni mdau wa tulonge.com alipoguswa na habari hiyo na kuamua kujitolea kumtunza na kumsomesha mtoto wa binti huyo. Licha ya Grace kuthibitisha hilo kupitia comment yake hapa tulonge, pia niliwasiliana na nae kwa njia ya simu na akathibitisha hilo.
Jitihada za kuwasiliana Mwananchi Comm Ltd nilizianza hivi:-
1. Jana niliwaandikia barua pepe kuwaeleza hili lkn kwa bahati mbaya iligoma kufika, sikujua kama kulikua na tatizo upande wao au vipi. Niliituma kwa webmaster@mwananchi.co.tz ambayo ndiyo email address iliyopo kwenye tovuti yao.
2. Leo baada ya kugundua email niliyo watumia haikufika, niliamua kuwapigia simu kwa namba +255 713471195 ambazo ipo kwenye tovuti yao lkn haikupokelewa.
Baada ya simu kutopokelewa nilipokea ujumbe toka kwao 'Mwananchi', na majibizano yalikua hivi:-
Mwananchi: Andika sms plz
Tulonge: Mimi ni administrator wa www.tulonge.com, kuna member wangu ameamua kutoa msaada wa kumtunza na kumsomesha mtoto wa dada mlemave wa Kondoa. Habari yake mliitoa tar 20 Jan yenye kichwa "Mlemavu anayeteseka baada ya kubakwa". Kinachotakiwa ni kumuunganisha na familia hiyo.Sheria zote zifuatwe ktk kufanikisha hili. Waweza nipigia kwa maelezo zaidi.
Mwananchi: Asante tutasaidiana kufanikisha hili.
Tulonge: Sawa, namba ya anayetaka kutoa msaada ni +255767882525 anaitwa Grace Kamonga wa Wizara ya Elimu, Kongwa,Dodoma.
Mwananchi: Asante, nimewapa wahariri wanashughulikia
Tulonge: Sawa Mkuu.
Tuliishia hapo, ujumbe wa mwisho niliutuma saa 6:12 mchana wa leo.Nitaendelea kufuatilia
Saa 6:27 mchana wa leo(January 23, 2013):
Nimepokea simu kutoka kwa Bw. Daniel Mwaijega ambaye ni Editorial Manager wa Mwananchi Comm Ltd. Ameushukuru Uongozi wa Tulonge na wadau wote wa tulonge kwa jitihada za kutaka mtoto huyu asaidiwe. Pia wamesema watawasiliana na Grace Kamongo ili kufanikisha suala hili.
Saa 7:24 mchana wa leo(January 23, 2013)
Mdau 'Grace Kamonga' amenipa taarifa kuwa amepigiwa simu na Mwananchi Comm Ltd ili kufuata taratibu za kisheria za kukabidhiana mtoto huyo.
Saa 9:30 mchana wa leo(Feb 05, 2013)
Nimewasiliana na Grace ili kujua kama Mwananchi wanaendelea na mchakato. Ameniambia mchakato bado unaendelea, mhariri (Daniel) alienda Manyoni ambapo huyo mtoto anaishi ili kuzungumzia suala hilo. Baada ya hapo mhariri huyo atarudisha ripoti Ofisi za Mwananchi ili wajue kinachofuata.
Saa 5:28 usiku wa leo(Feb 06, 2013)
Nimepokea sms toka kwa Grace, ikisema kuwa wana familia ya mtoto ambaye anataka kumsaidia IMERIDHIA kumtoa mtoto wao ili akatunzwe na Grace. Kesho Grace ataongea na Mwananchi kwa njia ya simu ili kujua nini kitafuata.
Saa 3:54 usiku wa leo (Feb 12, 2013)
Nimeongea na Grace kwa njia ya simu akanieleza kwa sasa anasubiriwa arudi nyumbani kwake Kongwa,Dodoma ili aweze kukabidhiwa mtoto huyo. Grace yupo masomoni Iringa, anategemea kumaliza masomo yake mwezi wa 7/ 2013.Ila kuna uwezekano wa kukabidhiwa mtoto huyo hata kabla ya mwezi wa 7.
Email toka kwa Grace baada ya kumuuliza walipofikia
Saa 5:17 usiku wa leo (Sept 30, 2013)
Najua wengi mtakua mnajiuliza mbona kuna ukimya juu ya tukio hili. Nilichat na Grace na akanieleza kuwa bado yupo Chuoni, kuna mambo anayakamilisha ndomaana hajakabidhiwa mtoto hadi sasa. Lakini kasema itabidi akabidhiwe mtoto ndani ya mwaka huu (2013) ili mwakani aweze anza shule. Ifuatayo ni Chat yetu.
Nitaendelea kuwajuza nini kinaendelea
Tags:
Hongera sana Kiongozi kwa kazi nzuri unayoifanya,Mungu atakulipa.
Pa1 mkuu Abasi
Abasi Mikidadi said:
Hongera sana Kiongozi kwa kazi nzuri unayoifanya,Mungu atakulipa.
tunashukuru kwa jitihada yako Disma mtoto huyo akisaidiwa jua kuwa ni baraka zako. endelea kutoa taarifa kama hizo najua watasaidiwa wengi
Nashukuru mkuu Babito, ila Dada Grace pia anastahili pongezi zaidi.
babito said:
tunashukuru kwa jitihada yako Disma mtoto huyo akisaidiwa jua kuwa ni baraka zako. endelea kutoa taarifa kama hizo najua watasaidiwa wengi
Pa1 sana Careen
careen mshindo said:
this is very good newz .....hongera sana kaka
Hongera sana Grace. Kutoa ni moyo wa mtu, wote tungekuwa na moyo huu tungekomboa watoto wengi masikini. Pia hongera kwa Dismas kwa kufanikisha mawasiliano. Mungu awabariki nyote, muwe mnatupa update
Pa1 mama
Mama Malaika said:
Hongera sana Grace. Kutoa ni moyo wa mtu, wote tungekuwa na moyo huu tungekomboa watoto wengi masikini. Pia hongera kwa Dismas kwa kufanikisha mawasiliano. Mungu awabariki nyote, muwe mnatupa update
© 2021 Created by Tulonge.
Powered by